MIUJIZA YA QUR'AN TUKUFU
SEHEMU YA PILI.
Kabla ya kuendelea mbele zaidi katika mada hii inayozungumzia miujiza ya Qur'an Tukufu,nitapenda kutoa ishara ndogo katika kuelezea umuhimu wa somo liitwalo:{Physics} ambalo ndilo somo mama lililoufikisha Ulimwengu wa Elimu,Maarifa na Ufundi mahala hapa ulipofikia.
Neno (Physics) linamaana ya Elimu ya Hali na tabia ya vitu vyote,na ya nguvu zote zilizomo duniani,kwa mfano:Nguvu ya joto,nguvu ya sauti,nguvu ya umeme,nguvu ya Sumaku(Magnetism) pamoja na mabadiliko yanayofanyika kwa nguvu hizo.
Mnamo karne ya sita (6th century) kabla ya kuzaliwa kwa Nabii Issa (a.s) wataalamu waliobobea katika Elimu hii ya {Physics} kutoka Yunani{Ugiriki} walianza kuchunguza na kufuatilia asili ya vitu vyote,tabia na hali zake,ili kupata ukweli wa mambo hayo kuhusu chanzo cha Ulimwengu huu.Kabla ya wataalamu hao kuanza kufanya uchunguzi na kufuatili asili ya vitu vyote,walikuwa na maswali mengi sana katika nafsi zao kuhusiana na vitu hivi wanavyoviona kila siku katika uliwmegu huu,je vitu hivi vimekuwepo tu hivi hivi ghafla ghafla pasina kuwepo nguvu nyuma yake ambayo ndio sababu ya kuwepo kwa vitu hivi?Na hili ni swali alilokuwa nalo kila mwanadamu katika nafsi yake!.Jibu hupatikana mara tu baada ya kufanya uchunguz na kujua asili ya vitu hivyo.Hivyo wataalamu hao baada ya maswali kuwa mengi katika bongo zao,wakaamua kufanya uchunguzi na utafiti ili wajue ukweli wa mambo kuhusu chanzo cha ulimwengu na vitu vyote vilivyomo ndani yake.
Mmoja wa watafiti hao,baada ya kufanya uchunguzi wake aliamini kuwa maji ndio chanzo cha vitu ulimwenguni.Mtafiti huyo alijulikana kwa jina (TALIS).Mtazamo wa mtu huyu haukuachana sana na Qur'an Tukufu kuhusu maji kuwa chanzo cha vitu.Kwa Ibara nyingine tunaweza kusema kwamba:Mtazamo wa Talis haukuachana na mtazamo wa Qur'an Tukufu ambayo inasema kwamba Mwenyeezi Mungu (s.w) kakifanya kila kuwa hai kupitia maji.
Ama mtafiti mwingine aliyejulikana kwa jina la {ENKASMINS} aliamini baada ya kufanya uchunguzi wake kuwa Hewa ni chanzo cha tabia na hali katika vitu. Mtafiti mwingine ambaye ni mashuhuri sana duniani bwana {AROSTO} baada ya kufanya uchunguzi wake aliamini kuwa vyanzo vya tabia na hali ulimwenguni vine,navyo ni hivi hapa vifuatavyo:
1-Maji
2-Hewa
3-Udongo
4-Moto.
Huu ndio uchunguzi wa baadhi ya wataalamu wa karne ya sita kabla ya kuzaliwa Nabii Issa (a.s) ambao ndio wanaojulikana zaidi. Ama tutakapo rudi katika mtazamo wa Qur'an Tukufu kuhusu chanzo cha vitu vyote,tutaona kwamba hakuna chanzo tofauti na Mwenyeezi Mungu (s.w) Mfalme wa Wafalme,aliyeumba mbingu,ardhi na vyote vilivyomo ndani yake.
Bilal Mwana wa Rabah aliyekuwa Mtoa adhana wa Mtume (s.a.w) pindi wakati wa sala ulipokuwa ukifika,siku moja alikuja kumuamsha Mtume (s.a.w) kwa ajili ya sala ya Alfajri,alipofika akamkuta Mtume (s.a.w) analia sana kiasi cha machozi kudondoka hadi ardhi kulowa kwa wingi wa machozi.Bilal akashangaa sana na kusema:Ewe Mtume wa Mwenyeezi Mungu (s.w) hivi walia wakati Mungu kakusamehe madhambi yote yaliyotangulia na yajayo?
Mtume (s.a.w): Ewe Bilal hutaki niwe mja Mwenye kumshukuru Mwenyeezi Mungu (s.w)?Kisha Mtume (s.a.w) akaendelea kusema:Na kwanini nisilie wakati Mwenyeezi Mungu (s.w) kaniteremshia aya ndani ya usiku huu isemayo:
"Hakika katika kuubwa kwa Mbingu na Ardhi,na mapishano ya (kutofautiana kwa) Usiku na Mchana,zimo alama (dalili) (za kuwepo Mungu) kwa wenye akili*Ambao humtaja Mwenyeezi Mungu wakiwa wamesimama na kukaa na wakiwa wamezilalia mbavu zao na wakifikiria katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi (huku wakisema) Mola wetu! hukuyaumba haya bure,utakasifu ni wako,basi tuepushe na adhabu ya moto."
Vile vile tukirejea katika Tarekh (Historia) kabla ya Mtume (s.a.w) kukabidhiwa mikoba au majukumu ya utume,tutakuta kwamba Mtume (s.a.w) alikuwa na tabia ya kwenda kukaa katika pango la Hiraa(Jabali Hiraa).Kazi kubwa aliyokuwa akiifanya ndani ya pango hilo ilikuwa ni kuutazama ulimwengu,mbingu na ardhi na pia kufikiria kuhusu chanzo cha vitu vyote hivi.
Ndio maana tunakuta katika hadithi tukufu kwamba Mtume (s.a.w) aliwakuta maswahaba wakifikiria sana,akawauliza: Mnafikiria kuhusu nini? Maswahaba wakamjibu:Tunafikiria kuhusu Mungu.Akawakataza na kusema:Fikirieni katika vile vitu alivyoviumba Mungu(Mtamjua alivyo) wala msifikirie namna gani Mungu mwenyewe alivyo." Mwisho wa sehemu ya pili. Usikose kufuatilia sehemu ya tatu ijayo Inshaallah kuhusu Miujiza ya Qur'an Tukufu.
MWISHO