BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU. 2
THAMANI YA UADILIFU
Mafunzo ya dini ya Uislamu yameweza kuweka athari kubwa zenye thamani kwenye fikra za wanaadamu, mafunzo haya si tu yameweze kufungua milango mipya ya kielimu katika nyanja za kijografia na kibaiolojia pamoja na kijamii, bali mafunzo hayo yameubadilisha mfumo wa fikra za wanaadamu, na suala ni lenye umuhimu sana katika maisha ya mwanaadamu na jamii.
Ni bidii ya kila mwalimu kutoa mafuzo mapya yenye faida kwa wanafunzi wake, na kila mfumo unaokuja katika katika jamii hujaribu kutoa mafunzo mapya kwa ajili ya wafuasi wa mfumo huo, lakini ni mifumo michache inakuja na kuweza kuubadilisha mzima wa fikra za wafuasi wake na kuwafunza namna mpya kabisa ya kufikiri.
Mwanaadamu kwa kutokana na kua yeye ni kiumbe mwenye akili basi mawanaadamu huyu katika masuala yake yanayohusiana na nyanja zote mbili, za kielimu pamoja na kijamii, hua ni mwenye kuzisimamishia dalili na hoja zake, na katika dalili zake anazozisimamisha akitaka asitake hua ameitegemea misingi fulani katika kuzisimamisha dalili hizo. Na kwa kupitia misingi hiyo hiyo hua ni mwenye kukataa au kupitisha hukumu fulani. Na watu hutofautiana kifikra pale wanapokua ni wenye kutofautiana katika misingi hiyo, misingi ambayo hutumika pale mtu anapotaka kusimamisha dalili zake au kulihukumu suala fulani, kwa natija na jawabu ya kila katika fikra zake hutegemea ni misingi gani aliyoitegemea mtu huyo katika kufikiri kwake, hili ndilo linalosababisha watu kutofautiana kifikra.
Kwa kawaida katika katika masuala ya kielimu, hua hakutokei tafauti za kifikra baina ya wataalamu wa elimu fulani wanoishi zama moja, na ikiwa kuna tafauti fulani inayoonekana baina ya wataalamu wa elimu fulani, basi tofauti hiyo itakua imesababishwa na kutoka na kua wataalamu hao hawakua wakiishi katika zama moja. Lakini katika masuala ya kijamii utakutia kua watu wanaishi katika jamii moja na zama moja, lakini watu hao wanatafautiana kimaumbile, kitabia, kivazi, n.k,
Pale mwanaadamu anapokabiliana na tabia pamoja na masuala tofauti ndani ya jamii fulani, akitaka asitake atakua ni mwenye kutoa hukumu fulani nje au ndani ya akili yake juu ya jamii hiyo, na kila moja kati ya yale aliyokumbana nayo katika jamii hiyo atakua amelipa thamani hukumu maalum kwenye akili yake, pengine moja litakua ni zuri kwa mtizamo wake na jengine liwe baya, basi lililo baya kwa laweza kua ni zuri kwa mwengine, hii inatokana na watu kutofautiana katika ile misingi yao mikuu ya kufikiri.
Kwa mfano suala la kujisitiri kwa mwanamke pale anapokua katika jamii, bila shaka watu wametofautiana katika suala hili, kuna wale wanaoona kua suala hili ni la lazima mwanamke, na kuna wengine wanaodai kua suala hili halina umuhimu wowote katika kuijenga jamii.
Basi pale tunaposema kua Uislamu umeleta mapinduzi katika fikra za wanaadamu, tunakusudia kua Uislamu ulipokuja uliyakuta baadhi ya mambo yaliyokua hayapewi thamani ndani ya jamii ukayapa thamani, na kuna mengine yaliyoonekana kua ni yenye thamani ukayashusha thamani, moja kati ya yale yaliyopewa thamani na Uislamu ni Ucha Mungu, Uislamu ulipokuja ulilitilia mkazo suala hili na kulipa thamani ya hali ya juu kabisa, na Mwenyeezi Mungu akaahidi malipo yenye thamani kubwa kwa kila atakayelitilia mkazo na kushikamana na suala hilo, na moja ya yale yaliyoshushwa thamani na Uislamu ni ukabila, suala ukabila lilikua ni lenye kupewa kipau mbele sana kabla ya kuja kwa Uislamu, lakini Uislamu ulipokuja ulilishusha daraja suala hili hadi thamani ya suala hili ikagonga zero katika kushuka kwake thamani,pale aliposema:-
"يَا اَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَاُنثَي وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوباً وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ اَكْرَمَكُمْ عِندَ اللهِ اَتْقَاكُمْ إِنَّ اللهَ عَلِيمٌ خَبِير"ٌ[1]
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.
[1]. Alhujirati, 13
MWISHO