BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
HIJABU NDANI YA QURAN .2
Tukiendelea na mada yetu kuhusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, katika makala hii tutandelea kuelezea athari nyengine muhimu za kuvaa hijabu katika jamii.
ATHARI NYENGINE
Mbali ya hayo niliyokuelezea kuvaa hijabu kwa mwanamke wa kiislamu kunawasababishia wengine kutokana na mwanamke huyo kuwa karibu na Mola wake,wavutiwe na tabia za mwanamke huyo na wao wafanya yale ambayo Mola wao anataka, hivyo tunaweza kuwagawa watu katika makundi matatu.
1. Watu wema na wanadumu katika uongofu wao.
2. Watu aliokuwa sio wema ambao wanakubali makosa waliofanya na wanapojirekebisha huwa thabiti katika msimamo wao, watu walio katika makundi haya mawili ni kidogo sana.
3. Watu wa kundi la tatu wanategemea hali ya jamii ilivyo, ikiwa jamii iko katika tamaduni nzuri na wao hufuata namna ya utamaduni wao ulivyo,na ikiwa jamii haiko katika tamaduni nzuri na wao vile vile hufuata namna ya utamaduni wao ulivyo.
Kwa hiyo watu ndio wanayoifanya jamii iwe nzuri, na vile vile ndio wanayoifanya jamii iwe mbaya. Mtume (s.a.w) anasema:-
“ Mtu yoyote ataevumbua jambo jema, kisha akalizowesha kwa watu kiasi ya kwamba baada yake yeye kukawa na watu wengine wenye kuliendeleza jambo hilo,basi mtu huyo hulipwa thawabu kwa kila wanapolitenda watendaji wa jambo hilo, bila ya kupunguziwa kitu watendaji hao katika thawabu zao, mtu yoyote atakaeanzisha au kuvumbua jambo baya, kisha akazowesha watu kulitenda au akalieneza kiasi ya kwamba baada ya kuondoka kwake kukawa na watu wanaliendeleza jambo hilo basi mtu huyo atalipwa uovu kwa kila wanapotenda watu hao jambo hilo, bila ya kupunguziwa watu hao kitu chochote katika uovu wao (dhambi zao).
Kuhusiana na utafiti wetu sisi ni lazima tukubali kwamba wenye kuzingatia suala la hijabu na kulitekeleza kisha wakalipigia debe kwa wengine jambo hilo lenye kupendwa na Mwenyeenzi Mungu bila ya shaka watapata bahashishi maalum kutoka kwa Mola wao. Acha niongezee kwa kusema kwamba kufanya hivyo ni ujasiri mkubwa katika upande wa mtu kupigana na nafsi yake.
Unaelewa kwamba moja kati ya vigao vya nafsi inavyogawika navyo ni nafsi ya mwanaadamu ni (Nafsi ammarah) yaani nafsi yenye kuamrisha maovu,nafsi hii siku zote hua inamuamrisha mtu kufanya maovu, baadhi ya Maulamaa wanasema hivi “ mtu mwenye kuitii nafsi yake na kuzipa kichogo amri za Mwenyeenzi Mungu ni mfano wa mtu aliemuokota mtoto wa mbwa wa mwitu mwituni, akamuokota, na kutokana kwamba mtoto wa mbwa wa mwitu alikuwa mdogo, na akawa anamlisha kila aina ya chakula kizuri, huku akighafilika kwamba anamlea adui alie hatari, hali ya kwamba mbwa yule aliekuwa akimlea mtu wa kwanza atakayemla baada ya kuwa mkubwa ni mlezi wake aliyemlea, ingawaje mwanamke ndani ya nafsi yake ana matamanio ya kutokuvaa hijabu na kujionesha kwa watu, ama kwa ajili ya kutaka radhi za Mola wake, basi mwanamke huyo utamuona anajilazimisha kuvaa hijabu, hatua kwa hatua nafsi yake hupata nguvu ya kutenda mema mpaka hufikia kutumia akili na kuangalia vipi Mola anasema katika mambo yote, mtu wa aina hii kwa rahisi zaidi huweza kuimiliki nafsi yake na matamanio ya nafsi, kama vile kupenda ukubwa, kufanya husuda na mengineyo.
MWISHO