BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
HIJABU NDANI YA QUR_ANI
Katika makala zilizopita tulielezea umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, na tukaashiria baadhi ya masuala ambayo yanaweza kujitokeza akilini mwa kila mtu na tukayajibu baadhi ya masuala hayo kadri ya uwezo wetu, kwa kuthibitisha kwa Aya za Qur-ani takatifu. Tukiendelea na mada yetu hiyo, katika makala hii tutaendelea kuyajibu masuala hayo. Suala lilikuwa hivi:-
Dada mpendwa wewe uliuliza kwamba una malengo gani mpaka uvae hijabu, na usivae nguo za zinazokwenda na wakati na kujipamba?
Tukiendelea na majibu yetu tunasema kuwa:- Kuvaa hijabu kunaleta usalama wa watu na jamii.
KUWEPO KWA USALAMA WA WATU NA JAMII
Mwanamke ambaye havai hijabu, na mwenye kujipamba ndio chanzo cha kuwafanya wanaume wenye maradhi kumfata, na tatizo hili ndilo linasababisha jamii isiwe na usalama, kama ambavyo nilielezea mwanzo kwamba vijana wengi wa kiume walio wahuni ndio wanowaharibu wanawake wasiokuwa na hijabu. Basi kwa ajili ya kuhifadhi usalama wa watu na jamii hakuna budi kuelewa kwamba ikiwa wanawake watakuwa na malengo ya kuvaa hijabu jamii itakuwa iko katika hali ya usalama.
KUTOKUSAIDIA WENGINE KATIKA KUFANYA MAKOSA AU KUTO KUSHIRIKIANA NA WATU WENGINE KATIKA UPUUZAJI SHERIA.
Baadhi ya wanawake ambao hawavai hijabu na ni wenye kujipamba wakati wanapotembea njiani husema kwamba, “sisi sio kwamba tunawafanyia hiyana waume zetu,na wala sio kwamba tunataka kuleta ufisadi katika jamii, na wala hatuko tayari kuona watu wanaleta ufisadi katika jamii, na wala hatuko tayari kuona wanaume wanatufuata ili kututumia kama ni vyombo vya starehe, kwa wanawake kama hawa basi ni vizuri kuwambia kwamba nyinyi mnalinda heshima yenu na utu wenu mbele ya wanaume lakini ni lazima wazingatie maelezo haya yafuatayo:
Kabla ya kuanza kuzungumzia kuhusu maelezo hayo ni lazima tufahamu kwamba suala la kuvaa hijabu ni suala ambalo ameliamrisha Mola wetu, na sisi hatuna budi kumtii yeye, ikiwa suala hilo linapelekea uharibikaji wa jamii, au hata ikiwa haipelekei uharibikaji wa jamii, baadhi ya wakati unaweza kumuona kijana mwanamme anamfuata mwanamke ambae hakujistiri au hakuvaa hijabu lakini kwa vile mwanamke huyo anaweza kumtukana mwanamme kutokana na kumvunjia heshima, mwanamme huyo tayari anakuwa keshatiwa wasiwasi na shetani na baada ya kuwa kamkosa mwanmke huyo huenda kutafuta mtoto wa watu wa kike na kumharibia maisha yake, matokeo yake utakuta mtoto huyo wa kike anatengana na familia yake, na inakuwa ndio sababu ya mtoto huyo kuhitilafiana na wazazi wake, sababu ya yote haya chanzo chake ni Yule mwanamke wa mwanzo aliesababisha matatizo hayo. Hakuna budi kukuelezea kisa kimoja ambacho kimetokea, na nna hakika kwamba huwezi ukasahau hata siku moja, baada ya kuwa kijana mmoja mwaname tuliekuwa tukizungumza kuhusa hali ya maisha ya kila siku, kijana hayo alinambia kwamba kila ufisadi na kufuru unayoijuwa wewe chanzo chake kinatokana na mimi, maneno hayo alimtamkia baada ya kumuelezea matatizo yaliyomkuta mimi sikuelezea kwa sababu sio vizuri kumtangazia mtu aibu yake.
Dada mpendwa kama wewe utafikiria kwa makini utaelewa kwamba kama ingelikuwa sio Yule mwanamke ambaye hakuwa na hijabu basi madhambi yote haya yasingelimfika Yule kijana mwanamme aliemuona mwanamke huyo na akatiwa wasi wasi na shetani kumfata mwanamke huyo, lakini yeye hana habari na haya, na baadae anasema mimi sina kazi na mtu na wala sina nia ya kufanya ufisadi katika jamii, na siko tayari kuona mwanamme ananivunjia heshima yangu wakati yeye ameshiriki katika madhambi yote hayo na yeye ndio chanzo cha matatizo yote.
MWISHO