KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU 3
  • Kichwa: KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU 3
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 13:18:48 3-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

KAULI KUHUSIANA NA UADILIFU. 4

Katika makala zilizopita tulizungumzia kauli mbali mbali za Maulamaa  kuhususiana na uadilifu, na tukaashiria baadhi ya Aya za Qur-ani zinazohusiana na maudhui hayo, katika makala hiitunaendelea na mada yetu hiyo, na vile vile tutaashiria baadhi ya hutuba zilizomo ndani ya Nahjulbalagha zinazoelezea kuhusu uadilifu.

Ndani ya kitabu cha Nahjul-balagha mna hutuba iitwayo Shaqshaqiyya,

"أما والله لقد تقمصها فلان  وإنه ليعلم أن محلي منها محل القطب من الرحى. ينحدر عني السيل , ولا يرقى إلي الطير. فسدلت دونها ثوبا  وطويت عنها كشحا. وطفقت أرتإى بين أن أصول بيد جذاء , أو أصبر على طخية عمياء , يهرم فيها الكبير. ويشيب فيها الصغير. ويكدح فيها مؤمن حتى يلقى ربه , فرأيت أن الصبر على هاتا أحجى , فصبرت وفي العين قذى. وفي الحلق شجا , أرى تراثي نهبا حتى مضى الاول لسبيله فأدلى بها إلى فلان بعده"

ndani ya hutuba hii utakuta namna gani Ali (a.s) anavyoelezea masikitiko yake kutokana na ubovu wa siasa uliotokea katika serikali zilizopita, zama ambazo watu walikuwa wamechoshwa na matatizo ya siasa hizo, kiasi ya kwamba baada tu ya kuuliwa Othaman, watu walimsumbua Ali (a.s) kila wakati na kumtaka ashike madaraka, huku Ali(a.s) akijaribu kuyakimbia madaraka hayo yaliyo na majukumu mazito ndani yake, hasa hasa kwa kutokana na uharibifu uliokua umefanya na viongozi waliopita kabla yake,pamoja na fitina na khiana alizofanyiwa Yeye mwenyewe na watu wa jamii yake, hayo yote yalimfanyaYeye asiwe na hamu tena ya kushika uongozi. Lakini kwa kutokana na kuhofia kua iwapo Yeye hatoshika madaraka watu wa jamii yake watazidi kuteketea, huku baadhi yao wakilia njaa na wengine wakilia kutokana na dhulma pamoja na kukhofia jamii kutogawika sehemu mbili huku sehemu moja yenye madaraka kuwakandamiza wasio na madaraka, hayo kwa ujumla ndio yaliyomfanya Ali (a.s) kukubali kushika madaraka hayo. Na hapo Ali (a.s) alisema:-

"أما و الّذى فلق الحبّة ، و برأ النّسمة لو لا حضور الحاضر و قيام الحجّة بوجود النّاصر ، و ما أخذ اللّه على العلماء أن لا يقارّوا على كظّة ظالم ، و لا سغب مظلوم لألقيت حبلها على غاربها ، و لسقيت آخرها بكأس أوّلها ، و لألفيتم دنياكم هذه أزهد عندى من عفطة عنز" .

“Ingelikua si lile kundi la watu lililonishindikiza na kuniomba kushika madaraka, na ingalikua si wajibu juu yangu kulibeba jukumu hili, nisingekubali kuchukua jukumu hili. Lakini ni lazima juu ya wanazuoni na wenye elimu kuto nyamaza pindi waionapo dhulma itendapwo, na ingalikua sio hivyo, basi ningelikaa kando kama nilivyokaa kando katika zama za makhalifa waliopita”.

MWISHO