SIFA TUKUFU ZA QUR_ANI
  • Kichwa: SIFA TUKUFU ZA QUR_ANI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 13:22:6 3-9-1403

                                                                                                                            KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU

MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU NO.1.

Katika makala zilizopita tulielezea misingi ya kuifahamu Quran takatifu, na tukaelezea baadhi ya sifa za Suratul-Faatiha, katika makala hii tunaendelea kuzielezea sifa nyengine za sura hiyo hiyo.

Suratul-Fatiha.

Imeitwa kwa jina tukufu hili kwa ajili ya mnasaba na muwafka wake, kwani tamko la Fatiha katika lugha ya kiarabu maana yake ni chanzo (mwanzo_cha kila kitu kile- kikiwa maneno au kitendo, basi hii Suratul-Fatiha ndiyo dibaji na ndio utangulizi wa Qurani.

Wakati wa kuteremka kwake.

Imeteremka sura hii mwanzo wa kuja Utume. Na hii ndio sura ya awali kuteremka kamili. Kabla yake ziliteremka Aya tu zilizomo katika sura ya Iqraa na Suratul-Muddathiri na Suratul-Muzzammil.

Miongoni mwa sifa za suratul-fatiha ni hizi zifuatazo:-

3. Sura Al-Hamd ni Fahari Kubwa  ya Mtume (s.a.w.w).

Ubora mkubwa ulioje kwamba kwenye aya za Qur’ani Tukufu Sura Al-Hamd imejulishwa kwa Mtume (s.a.w.) katika namna ya zawadi kubwa, na imeanzishwa sambamba na Qur’ani Tukufu yote, ambamo Anasema:-

وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعاً مِّنَ الْمَثَانِى وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ[1]

“Na kwa hakika tumekupa (Aya) saba zisomwazo mara kwa mara na Qur’ani Tukufu (usemi huu unahusisha Sura Al-Hamd kuwa imeteremshwa mara mbili).”

Qur’ani Tukufu pamoja na umashuhuri wake wote, katika mfano huu imewekwa sambamba na Sura Al-Hamd, na kuwa imeteremshwa mara mbili pia ni kwa sababu ya umuhimu wake mkubwa sana.

Suala hili limetajwa kwenye simulizi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ambaye alisema, “Mwenyezi Mungu, Aliye Tukuka, amenipa upendeleo mahsusi kwa Wahyi wa Sura  Fatihah na Ameiweka sambamba na Qur’ani Tukufu Kuu, na Sura Al-fatihah ni miongoni mwa hazina zilizo thaminiwa sana kutoka kwenye hazina za Kiti cha Enzi (cha Mwenyezi Mungu)[2].”

4. Msisitizo wa Kukaririwa Sura hii.

Ikilengwa kwenye lugha ya ushawishi katika mazungumzo ambayo yanatupa mwanga kwenye sifa moja tu ya Sura Al-Hamd, inaonekana wazi kwamba kwa nini katika Hadithi za Kiislamu, kwenye makusanyo ya Shia na Sunni, msisitizo mkubwa umewekwa juu ya kukaririwa kwake.  Kukaririwa kwa Sura hii humpa mwanadamu zawadi ya kiroho na kiimani, humsogeza karibu zaidi na Mungu, huweka utakaso wa moyo na roho, huimarisha dhamira yake na huongeza haraka yake (ya kutembea) kwenye njia ya Mungu na muumbo. Na huweka kigingi kati yake na dhambi na kupotoka (kwenye njia iliyonyooka.)

Kwa sababu hii, tunasoma kwenye simulizi kutoka kwa watu wa Nyumba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w).

 “Shetani aliomba na kulia kwa huzuni akiwa katika mateso mara nne.  Mara ya kwanza ilikuwa mnamo siku alipofukuzwa asionekane mbele ya Mwenyezi Mungu, halafu wakati alipoondoshwa kwenye Bustani na kupelekwa duniani. Mara ya tatu ilikuwa wakati wa kuanza kwa misheni ya Muhammad (s.a.w.w) baada ya kutokuwepo kwa Mitume (a.s.), na kilio cha mwisho kilikuwa wakati Msingi wa Kitabu ulipoteremshwa[3].”


[1] Surat Alhijr Aya ya 87.

[2] (Tafsiri Burhan, Juz. 1, uk. 26)

[3] (Noor-uth-Thaqalayn Juz ya 1, uk. 3)

MWISHO