DALILI ZINAZOTHIBITISHA ELIMU YA ALLAH
  • Kichwa: DALILI ZINAZOTHIBITISHA ELIMU YA ALLAH
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 18:8:9 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

 KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

ELIMU YA MWENYEENZI MUNGU HAINA MPAKA 3

DALILI ZINAZOTHIBITISHA ELIMU YA ALLAH (S.W)

Katika makala iliyopita tulielezea elimu ya Mwenyeezi Mungu isiyo na mwanzo wala mwisho, katika makala hii tutazielezea dalili ambazo zinathibitisha elimu hiyo ya Allah (s.w).

Dalili mbili zinazothibitisha utukufu usio mpaka wa elimu ya Mwenyeenzi Mungu.

1- Muumba (uumbaji).

Hapana shaka yoyote kuwa viumbe vyote ulimwenguni vimeumbwa na Mwenyeenzi Mungu mmoja, naye akaviweka katika nidhamu maalumu,viumbe vyote duniani vinamhitajia Mwenyeenzi Mungu katika kila kitu, kiasi ya kwamba pindi nidhamu hiyo isipokuwa katika mfumo maalumu kutasababisha mparaganyiko katika nidhamu hiyo. Hivyo Mwenyeenzi Mungu Mtukufu anathibitisha hayo kwa kusema kuwa yeye hakughafilika wala hatoghafilika na viumbe vyake alivyoviumba.

وَلَقَدْ خَلَقْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعَ طَرَائِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ الْخَلْقِ غَافِلِينَ[1]

Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe.

Na katika aya nyengine anasema:-

اَلاَ يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ[2]

Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?

2- Siku ya hesabu (malipo).

Siku ya kiama (malipo) Mwenyeenzi Mungu atawalipa wanaadamu wote kutokana na yale waliyoyatenda, na hii ni dalili bora inayothibitisha elimu ya Mwenyeenzi Mungu. Kwa sababu Yeye ni mwenye elimu ya yote makubwa na madogo. Katika Qur-ani kariym tunasoma:-

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْراً يَرَهُ. وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرّاً يَرَهُ[3]

Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!

Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!

Maelezo kuhusiana na Aya

Na Aya mbili hizi zafahamisha kwamba Mwanaadamu atajaziwa kwa kila alitendalo, la kheri au la shari hata likiwa dogo sana kama uzani wa chungu mdogo pia.

Na kwa sababu hiyo basi Mwenyeenzi Mungu anasema:-

وَمَا تَكُونُ فِى شَاْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلاَ تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلاَّ كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُوداً إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِى الاَرْضِ وَلاَ فِى السَّمَاء وَلاَ اَصْغَرَ مِن ذٰلِكَ وَلا اَكْبَرَ إِلاَّ فِى كِتَابٍ مُّبِينٍ[4]

Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur'ani, wala hamtendi kitendo chochote ila Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnapo shughulika nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika Kitabu kilicho wazi.

Tabaka za elimu ya Mwenyeenzi Mungu

Mwenyeenzi Mungu mbali ya kuwa ana elimu yaa zati, vile vile ana elimu nyengine nyingi, kwa mfano:-

Yeye ni mmiliki wa kila kitu (ana elimu ya milki na malakuti).

Kufahamu uhakika huo (ya kuwa Mwenyeenzi Mungu ndiye mmiliki wa kila kitu), kunaleta athari nyingi katika akida na matendo ya wanaadamu, na inamuepusha mwanaadamu huyo na hatari ya kuwa na itikadi ya kuwa kila jambo ambalo mwanaadamu analifanya halifanyi kwa hiari yake bali Mwenyeenzi Mungu amemlazimisha. (hali ya kuwa atikadi hiyo haina ukweli wala usahihi wowote).

Katika kipengele hiki tutaelezea baadhi ya aya kataba za elimu za Mwenyeenzi Mungu.

Katika Qur-ani tunasoma:-

يَمْحُو اللّهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ وَعِندَهُ اُمُّ الْكِتَابِ[5]

Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote iko kwake.

Hekima na natija tunazozipata katika aya hiyo ni:-

1- Kuna nidhamu ya kimaumbile, nidhamu hii haina hiyari ndani yake kwa viumbe wote duniani, - sio binaadamu wala wanyama –

Kwa mfano mapigo ya moyo hayapigi kutokana na hiyari yake binaadamu.

Lakini kuvuta pumzi inawezekana ikawa ni hiyari ya mwanaadamu.

2- Kila kitu kilichoko duniani ni kivuli cha ukweli wa milki na ufalme wa Mwenyeezi Mungu, kwa hiyo milki na ufalme wa Mwenyeezi Mungu ndio chanzo cha kila kitu.

(ام الکتاب) و(لوح محو و اثبات)

Ufafanuzi wa maneno hayo:-

Ummu l-kitaab yaani ufalme na milki ya Mwenyeezi Mungu.

Lawhu- mahwu wa Ithbati yaani ni ubao wa kudhibiti au kutodhibiti mambo.

Kila kitu ambacho kinaweza kubadilika kinachukua amri kutoka kwa Mwenyeezi Mungu, na hakuna madhara yoyote katika ufalme wa Mwenyeezi Mungu.

Athari ya kuamini Mola mmoja katika kumuweka sawa mwanaadamu .

Ama ni lazima tuzingatie kuwa mwanaadamu anayafanya matendo yake kwa hiyari yake bila ya kulazimishwa. Basi natija tunayoipata katika kauli hiyo ni kwamba:-

- Matendo yote anayoyafanya mwanaadamu ikiwa kwa ameyafanya kwa nia njema au kwa nia mbaya anayafanya kwa hiyari yake.

Na mwanaadamu anafanya matendo yake kutokana na elimu aliyonayo, na sio kama wanavyofikiria baadhi ya kuwa mwanaadamu anafanya matendo kwa kulazimishwa na Allah (s.w).

Tabaka nyengine ya elimu ya Mwenyeenzi Mungu ni I ya imatendo, yaani kuthibitika kwa elimu ya Mwenyeenzi Mungu katika dunia, kwa mfano :-

Kuthibitika kwa kisa cha As-habi Kafi pale Allah (s.w) anaposema:-

فَضَرَبْنَا عَلـٰي آذَانِهِمْ فِى الْكَهْفِ سِنِينَ عَدَدا[6]. ثُمَّ بَعَثْنَاهُمْ لِنَعْلَمَ اَيُّ الْحِزْبَيْنِ اَحْصَي لِمَا لَبِثُوا اَمَداً

Tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa wa kadhaa.

Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili lilio hisabu sawa muda walio kaa. Kutokana na maelezo hayo basi imethibitika kuwa hakuna kitu chochote duniani kisichoeleweka na Mwenyeenzi Mungu.

Kuhusu shafaa Allah (s.w) anasema:-

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ مَا لاَ يَضُرُّهُمْ وَلاَ يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـؤُلاء شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللهِ قُلْ اَتُنَبِّئُونَ اللّهَ بِمَا لاَ يَعْلَمُ فِى السَّمَاوَاتِ وَلاَ فِى الاَرْضِ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَي عَمَّا يُشْرِكُونَ[7]

Nao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu! Sema: Je! Mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyo yajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Subhanahu wa Taa'la! Ametakasika na ametukuka na hao wanao mshirikisha naye.

Maelezo kuhusiana na Aya

Wanaonyeshwa kuwa tamaa yao hiyo itawatamauka siku ya kiama.

[1] Surat Muuminun aya ya 17

[2] Suratul-Mulk aya ya 17

[3] Surat Zilzala aya ya 7-8

[4] Surat Yunus aya ya 61

[5] Surat –Araad aya ya 39

[6] Suratul-Alkahf aya ya 11-12

[7] Surat Yunus aya ya 18

MWISHO