ELIMU YA ALLAH HAINA MPAKA
  • Kichwa: ELIMU YA ALLAH HAINA MPAKA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 13:12:59 3-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

 KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

ELIMU YA MWENYEENZI MUNGU HAINA MPAKA

* Elimu ya Mwenyeenzi Mungu ikoje? Na ina kiwango gani?

* Hivi kuna tofauti baina ya elimu ya Mwenyeenzi Mungu na elimu ya wanaadamu?.

Baada ya kuwa na akida na kuamini Mola mmoja, vile vile tunakiwa tuwe na imani ya elimu yake, kwani kuitambua elimu ya Mwenyeenzi Mungu kunaleta athari nyingi muhimu katika itikadi na matendo yetu.

Elimu ya Mwenyeenzi Mungu haina mwanzo wala mwisho, kiasi ya kwamba upeo wa elimu hiyo umekusanya vitu vyote alivyoviumba na asivyoviumba, hapana shaka Mwenyeenzi Mungu ana elimu ya kila kitu, ikiwemo elimu ya zama zilizopita na zijazo.

Katika somo hili kwa kutumia aya za Qur-ani kariym tutaelewa na kuifahamu elimu ya Mwenyeezi Mungu, na umahiri alioutumia Mwenyeezi Mungu katika kuviumba vitu vyote duniani na akhera.

Ufafanuzi wa neno elimu

Elimu ni kinyume cha jahili, na tunaweza kuifafanua elimu katika njia mbili zifuatazo, nazo ni:-

1- Elimu yaani kuwa na maarifa au kujua kuwepo asili ya kitu, kama vile ilivyokuja katika Qur-ani kariym:-

وَإِذِ اسْتَسْقَي مُوسَي لِقَوْمِهِ فَقُلْنَا اضْرِب بِّعَصَاكَ الْحَجَرَ فَانفَجَرَتْ مِنْهُ اثْنَتَا عَشْرَةَ عَيْناً قَدْ عَلِمَ كُلُّ اُنَاسٍ مَّشْرَبَهُمْ كُلُواْ وَاشْرَبُواْ مِن رِّزْقِ اللهِ وَلاَ تَعْثَوْاْ فِى الاَرْضِ مُفْسِدِينَ[1]

Na Musa alipo omba maji kwa ajili ya watu wake, tulimwambia: Lipige jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatimbuka chemchem kumi na mbili; kila kabila ikajua mahali pake pa kunywea. Tukawaambia: Kuleni na mnywe riziki ya Mwenyezi Mungu, wala msiasi katika nchi mkafanya uharibifu.

Elimu yaani kufahamu uhakika na sifa ya kitu, kama vile ilivyoelezewa katika Qur-ani.

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا جَاءكُمُ الْمُؤْمِنَاتُ مُهَاجِرَاتٍ فَامْتَحِنُوهُنَّ اللهُ اَعْلَمُ بِإِيمَانِهِنَّ فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلاَ تَرْجِعُوهُنَّ إِلَي الْكُفَّارِ لاَ هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلاَ هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ وَآتُوهُم مَّا اَنفَقُوا وَلاَ جُنَاحَ عَلَيْكُمْ اَن تَنكِحُوهُنَّ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ اُجُورَهُنَّ وَلاَ تُمْسِكُوا بِعِصَمِ الْكَوَافِرِ وَاسْاَلُوا مَا اَنفَقْتُمْ وَلْيَسْاَلُوا مَا اَنفَقُوا ذٰلِكُمْ حُكْمُ اللهِ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ وَاللهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ[2]

Enyi mlio amini! Wakikujilieni wanawake Waumini walio hama, basi wafanyieni mtihani - Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi Imani yao. Mkiwa mnawajua kuwa ni Waumini basi msiwarudishe kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni hao wanaume mahari walio toa. Wala hapana makosa kwenu kuwaoa mkiwapa mahari yao. Wala msiwaweke wanawake makafiri katika kifungo cha ndoa zenu. Na takeni mlicho kitoa, na wao watake walicho kitoa. Hiyo ndiyo hukumu ya Mwenyezi Mungu anayo kuhukumuni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.

Maelezo kuhusiana na aya:

Tazama uadilifu wa Uislamu. Kuwa wakija Madina wanawake wa kikafiri wanatoka Makka, na waume zao wako Makka, wakamwambia Mtume kuwa wamesilimu, basi asiwapokee tu Mtume; bali awafanyie mtihani barabara mpaka umdhihirikie Uislamu wao ndipo awachukue; na akiwachukua awapelekee mahari yao waume zao makafiri- awapelekee fedha walizowaolea.Kuna insafu zaidi kuliko hii? Na Mtume aliwafanyia.

Na mmoja katika wanawake hao ni Bibi Ummu Kulthum binti Ukba bin aby Muayt- baba yake alikuwa kafiri mwenye chuki kubwa kabisa juu ya Mtume na Waislamu wote.

Na makafiri wakaambiwa nao wakiowa wake wa Waislamu – walioko ukafirini huko – walete mahari yao. Lakini hawakukubali. Basi Mtume akawa anawalipa waislamu hawa  - walionyimwa haki ya mahari yao- alikuwa anawalipa katika pesa zinazopatikana katika ngawira, (nyara) kama ilivyo katika aya ya kumi na moja hapa.

وَإِن فَاتَكُمْ شَيْءٌ مِّنْ اَزْوَاجِكُمْ إِلَي الْكُفَّارِ فَعَاقَبْتُمْ فَآتُوا الَّذِينَ ذَهَبَتْ اَزْوَاجُهُم مِّثْلَ مَا اَنفَقُوا وَاتَّقُوا اللهَ الَّذِى اَنتُم بِهِ مُؤْمِنُونَ[3]

 Na akitoroka yeyote katika wake zenu kwenda kwa makafiri, tena ikatokea mkapata ngawira, basi wapeni walio kimbiwa na wake zao kiasi cha mahari waliyo yatoa. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mnamuamini.

Wala hakuwalipizia kisasi makafiri kuwa na sisi hatutakuleteeni mahari ya wake zenu waliokuja kwetu, maadamu nyinyi mnakataa kutoa. Hapana kulipa mabaya, mmoja katika hao wanawake waliomili ukafirini ni mke wa Omar bin alkhataab- Qureyba binti aby Umayya, mtoto wa shangazi lake Mtume ndugu wa kuumeni wamkewe Mtume, bibi Hind binti Aby Umayya. Katika wanawake waliokuwa wazuri sana wa sura. Mwisho alirejea uislamuni, akaolewa na Muawiya.

Tafauti baina ya elimu ya Mwenyeenzi Mungu na elimu ya viumbe wengine.

Elimu ya Mwenyeenzi Mungu zi zati (haina mwanzo wala mwisho), ama elimu ya viumbe wengine ina kiwango maalumu, kama vile Qur-ani inavyosema:

عَالِمُ الْغَيْبِ فَلاَ يُظْهِرُ عَلـٰي غَيْبِهِ اَحَداً
إِلاَّ مَنِ ارْتَضَي مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُ يَسْلُكُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ رَصَدا[4]

Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake. Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.

Maelezo kuhusiana na aya

Hii ni moja katika zile aya nyingi kabisa zinazovunja habari za utazamiaji.

Wapiga bao waongo                     Waongo sana kabisa

Yanapita kwao mambo                  Hawayajui kabisa

Kwa hiyo mwanaadamu anaweza akafaidika kwa elimu ya Mwenyeenzi Mungu kwa njia mbili, nazo ni:-

1- Elimu ya moja kwa moja inayotoka kwa Mwenyeenzi Mungu.

Kama vile anavyosema Allah (s.w).

وَعَلَّمَ آدَمَ الاَسْمَاء كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلـٰي الْمَلاَئِكَةِ فَقَالَ اَنبِئُونِى بِاَسْمَاء هَـؤُلاء إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ[5]

Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli.

Maelezo kuhusiana na aya Wamesema kuwa Al-as-maa,ni majina ya Mungu kama ilivyo katika Aya ya 180 ya Sura ya saba.

وَلِلّهِ الاَسْمَاء الْحُسْنَي فَادْعُوهُ بِهَا وَذَرُواْ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِى اَسْمَآئِهِ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ[6]

Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo. Na waacheni wale wanao haribu utakatifu wa majina yake. Hao watakuja lipwa waliyo kuwa wakiyatenda.

Tunawaambia itakuwaje majina ya Mwenyeenzi Mungu kutandazwa yakadhihirishwa? Hayo ni majina ya vitu vyenye roho na visivyokuwa na roho, vilivyowekwa mbele ya Nabii adam akaambiwa avitaje. Na hivyo kutumiwa “Him” badala ya “ha” ni kwa sababu vimechanganyika visivyokuwa na akili na vyenye akili,. Na hii ndio dasturi ya lugha ya kiarabu.labda hafahamu lugha barabara, anajua juu juu tu. Na hii ndiyo hatari ya lugha chache. Ilimu chache udhia: ilimu chache yadhuru. Na wanaona hapo imeandikwa: “ Asmai Haaulai” – majina ya hawa. Iko wapi majina ya Mwenyeenzi Mungu?

[1] Surat Albaqara aya ya 60

[2] Surat Mumtahina aya ya 10

[3] Suratt-Mumtahina aya ya 11

[4] Surat jin aya 26-27

[5] Suratul-baqara aya ya 31

[6] Suratul-Al-aaraf aya ya 180

MWISHO