BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
FAIDA ZA KUISOMA QUR_ANI:
Kuisoma Qur-ani kunaleta faida mbali mbali katika maisha ya mwanaadamu, miongoni mwa faida hizo ni :-
1. Mwenyeezi Mungu humuondolea mabalaa msomaji Qur-ani.
2. Kusoma Qur-ani ni kafara za madhambi.
3. Mwenye kusoma Qur-ani huepukana na moto wa jahannam na huwa katika amani na adhabu za Mwenyeezi Mungu.
4. Muumini mwenye kusoma Qur-ani Mwenyeezi Mungu humuangalia mtu huyo kwa jicho la rehema.
5. Mwenye kusoma Qur-ani siku ya kiama huwa pamoja na Manabii .
6. Mwenye kusoma Qur-ani siku ya kiama huvuka njia akiwa pamoja na Manabii.
7. Mwenye kusoma Qur-ani Mwenyeezi Mungu humpa mtu huyo ujira na malipo ya Mitume wake.
QUR_ANI KATIKA MAELEZO YA IMAM KHUMEINI (R.T.A).
Qur-ani ni ya wote na ni kwa ajili ya kuwapa saada watu wote duniani, Qur-ani ndio iliyowasababisha masultani muda wa nusu karne tu kuikubali dini ya kiislamu, na sisi (waislamu) pindi tutakapokuwa pamoja na Qur-ani tutaweza kupambana na maadui wa kiislamu, na pindi ambapo tutajitenga na Qur-ani tutawapa fursa maadui wa kiislamu wafanikiwe na mbinu zao ili kuiharibu dini ya kiislamu, kwani maadui hao wanafanya kila hila ili watutenge na kitabu hicho kitukufu, na wanajitahidi kufanya kila hila ili watuweke sisi (waislamu) katika maisha ya madhila na ya kitumwa,Waislamu kama tunahitajia uhuru katika maisha yetu inatulazimu kuifuata Qur-ani na kufuata yale ambayo ametuamrisha Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).
Sisi Waislamu ni lazima tuwe wamoja na tuwe kitu kimoja katika kuilinda dini ya kiislamu, ni lazima tujifaharishe kwani ni wenye kuifuata dini ya kiislamu na kukifuata kitabu kitukufu cha Mwenyeezi Mungu, Qur-ani ni kitabu ambacho kinamuokoa mwanaadamu na utumwa, na kumuongoza katika njia njema (haki) na kinamuokowa kutofuata njia iliyo batili[1]
QUR_ANI KATIKA KAULI YA AYATU LLAHI KHOMENEI .
- Mila zote duniani ni lazima zikusanyike pamoja ili kukisoma kitabu hicho kitukufu, na waislamu wote dunianai ni lazima wajuwe na kuelewa kuisoma Qur-ani.
- Chanzo na sababu za mafanikio ya Serikali ya jamhuri ya kiislamu ni kuwa pamoja na Qur-ani, waislamu wote ni lazima wafanye jitihada ili kuweza kukisoma kitabu hicho, kukitarjumu, na vile vile waweze kuyafahamu na kuyafanyia kazi yale ambayo yameamrishwa katika kitabu hicho.
-Katika nchi ambazo zinafuata kanuni za kiislamu, watu wote ni lazima wawe na uwezo wa kuisoma Qur-ani kariym kwa usahihi kabisa.
-Pindi ambapo waislamu tutakapokuwa pamoja na Qur-ani itatusaidia sisi tuwe na maarifa juu ya dini ya kiislamu, na akili zitafanya kazi vizuri zaidi.
- Matatizo na misuko suko yote inayotokea katika jamii ya waislamu yanasababishwa na kutokuwa mbali na maarifa ya Qur-ani kariym.
- Kuwa pamoja na Qur-ani yaani ni kuisoma Qur-ani, na kuisoma Qur-ani yaani ni kutafakari katika kufahamu maana yake Qur-ani.
- Ni aya za qur-ani ndizo zinazoweza kuwaongoza na kuwaonesha wanaadamu njia za haki, na kuwapa nguvu za kupambana na madhalimu. Na ni maarifa ya Qur-ani yaliyopelekea jamuhuri ya kiislamu kuweza kupambana na majahili madhalimu katika karne ya 20.
- waislamu pindi tutakapotafakari na kuzingatia maana ya aya za Qur-ani tunaweza kukabiliana na madhalimu bila ya hofu yoyote.
[1] Wasiyat Nome siyasi Ilahiy.
MWISHO