HEKIMA ZA ALLAH KATIKA NIDHAMU YA KIMAUMBILE
  • Kichwa: HEKIMA ZA ALLAH KATIKA NIDHAMU YA KIMAUMBILE
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 17:44:38 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

HEKIMA ZA ALLAH KATIKA NIDHAMU YA KIMAUMBILE
Tukiangalia na kuzingatia kwa makini siri ya uumbaji wa viumbe vyote duniani, na tukifikiria nidhamu ya vitu hivyo vinavyostaajabisha na kujalibisha hapana shaka uhakika wa wanaadamu utadhihirika.
Nidhamu hiyo tukufu tunaiona katika viumbe mbali mbali duniani, kuanzia ndege, wanyama, viumbe wanaoishi katika ardhi na baharini, n.k…vyote hivyo ni alama inayoonesha uwezo na hekima za Mwenyeenzi Mungu, na vyote hivyo vinathibitisha kutokuwepo aibu yoyote katika uumbaji wa Mwenyeenzi Mungu, na Qur-ani inaashiria uhakika huo kwa kusema:-
سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِى السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ[1]
Kinamsabihi kumtakasa Mwenyezi Mungu kila kiliomo ndani ya mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Maelezo kuhusiana na aya:-
Aya za mwanzo wa sura hii _ kama za mwisho wa suratul Hashr – zinataja nyingi katika sifa za Mwenyeezi Mungu.
Na watu wanashughulikia kuzisoma hizo za suratul Hashr kuliko hizi; na zote ni sifa za Mwenyeezi Mungu, na zote zimejiwa na hadithi za kutaja fadhila zake.
Mbali ya hayo mfumo huo wa maisha ya viumbe uko katika nidhamu maalumu, kiasi ya kwamba kila kiumbe kinatatua mahitajio yake kwa kiumbe chengine, na Mwenyeenzi Mungu ndiye anayetatua mahitajio yote ya viumbe hali ya kuwa Yeye hahitajii chochote kutoka kwa viumbe wake.
Na kila kiumbe kina wadhifa wake katika kutatua mahitajio ya viumbe wengine. Kama tunavyosoma katika Qur-ani.
اَلَمْ نَجْعَلِ الاَرْضَ مِهَاداً. وَالْجِبَالَ اَوْتَاداً . وَخَلَقْنَاكُمْ اَزْوَاجاً . وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتاً . وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاساً . وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشاً

وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعاً شِدَاداً . وَجَعَلْنَا سِرَاجاً وَهَّاجاً[2]

Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? Na milima kama vigingi? Na tukakuumbeni kwa jozi? Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? Na tukaufanya usiku ni nguo? Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto;
Maelezo kuhusiana na aya:-
Tangu aya hii mpaka aya ya 16 Mwenyeezi Mungu anawaonesha waja wake neema nyingi alizowaneemesha, ili wafahamu kwamba, Mwenye kuneemesha neema kama hizi katika ulimwengu, hawawachi waja wake katika upotevu pasi na kuwaletea mtu wa kuwaongoa njia njema ya kuwafikisha katika neema za Dunia na Akhera, na kwamba Mwenye kufanya yote haya hapana jengine liwezalo kumshinda. Na maana ya “tandiko” hapa ni mahali pa kumfaa mtu kufanya alitakalo katika maisha yake. Si mapendeleo yake kuwa Ardhi imekaa kama tandiko la kitanda.[3]                    

Kwa upande mwengine Mwenyeenzi Mungu ameweka nidhamu maalumu katika mauti na uhai, ili wanaadamu washuhudie maisha mapya,kama vile Allah (s.w) anavyosema:-
يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِى الاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَكَذٰلِكَ تُخْرَجُونَ[4]
Hukitoa kilicho hai kutokana na kilicho kufa, na hukitoa kilicho kufa kutokana na kilicho hai. Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Na kama hivyo ndivyo mtavyo fufuliwa.
Na baadae Mwenyeenzi Mungu anaelezea kwa kusema kuwa uhai ni katika alama ya rehema zake.
فَانظُرْ إِلَي آثَارِ رَحْمَتِ اللهِ كَيْفَ يُحْيِى الاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا إِنَّ ذٰلِكَ لَمُحْيِى الْمَوْتَي وَهُوَ عَلـٰي كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ[5]
Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyo ihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo ndiye bila ya shaka Mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Basi natija ya maelezo hayo ni kwamba, mwanaadamu kwa kushuhudia nidhamu ya viumbe vyote duniani atajua na kuzikubali hekima za Mwenyeenzi Mungu ya kwamba dunia hii imeumbwa kwa umbile lililozuri na lililobora kabisa. Kama anavyosema katika Qur-ani:-

الَّذِى اَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ وَبَدَاَ خَلْقَ الإِنسَانِ مِن طِينٍ [6]

Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa udongo.
Maelezo kuhusiana na Aya:-
Kila alichokiumba Mwenyeezi Mungu amekitengeneza, amekikamilishia kila lake, hakuna nuksani, hakiwezi kutilika kosa,kama alivyotuambia katika suratul-mulk Aya ya 3na ya 4.
الَّذِى خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقاً مَّا تَرَي فِى خَلْقِ الرَّحْمَنِ مِن تَفَاوُتٍ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَي مِن فُطُورٍ

ثُمَّ ارْجِعِ الْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنقَلِبْ إِلَيْكَ الْبَصَرُ خَاسِاً وَهُوَ حَسِيرٌ[7]

Aliye umba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema.
Hebu rudisha nadhari! Unaona kosa lolote? Tena rudisha nadhari mara mbili, nadhari yako itakurejea mwenyewe hali ya kuwa imehizika nayo imechoka.

[1] Surat-Alhadiyd Aya ya 1

[2] Suratun-nabaa aya ya 6-13

[3] Taz.sawi katika sura ya Alghaashiyah.

[4] Surat Ruum Aya ya 19

[5] Surat Ruum Aya ya 50

[6] Surat Sajdah aya ya 7

[7] Suratul0mulk aya ya 3-4


MWISHO