BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
Mwenyezi Mungu ni Mbora wa waumbaji.
Aya:
فَتَبَارَكَ اللهُ اَحْسَنُ الْخَالِقِينَ[1]
Tarjuma:
Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.
Hijabu
Aya:
وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلـٰي جُيُوبِهِنَّ[2]
Tarjuma:
Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao.
Kujisifu na (kujitakasa) nafsi zenu.
Aya:
فَلاَ تُزَكُّوا اَنفُسَكُمْ[3]
Tarjuma:
Basi msijisifu (msijitakase) nafsi zenu kuwa ni safi.
Kusoma Qur-ani
Aya:
فَاقْرَؤُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ[4]
Tarjuma:
Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani.
Kuwashukuru wazazi (baba na mama).
Aya:
اَنِ اشْكُرْ لِى وَلِوَالِدَيْكَ[5]
Tarjuma:
Nishukuru Mimi na wazazi wako.
Kupatanishana au (kujenga suluhu).
Aya:
فَاَصْلِحُوا بَيْنَ اَخَوَيْكُمْ[6]
Tarjuma:
Basi patanisheni baina ya ndugu zenu.
Maji
Aya:
وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاء كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ[7]
Tarjuma:
Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? .
Taquwa au ( kumcha Mwenyeenzi Mungu).
Aya:
إِنَّ اَكْرَمَكُمْ عِندَ اللهِ اَتْقَاكُم[8]
Tarjuma:
Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi.
Msiitane kwa majina mabaya.
Aya:
وَلاَ تَنَابَزُوا بِالاَلْقَابِ[9]
Tarjuma:
Wala msiitane kwa majina ya kejeli.
[1] Surat-Mu-uminun Aya ya 14
[2] Surat-Nuur Aya ya 31
[3] Surat-Najmi Aya ya 32
[4] Surat-Muzamil aya ya 20
[5] Surat-Luqmani Aya ya 14
[6] Surat- Hujurat Aya ya 10
[7] Surat Anbiyaa aya ya 30
[8] Surat Hujurati Aya ya 13
[9] Surat Hujurati Aya ya 11
MWISHO