ADABU ZA WASOMAJI QUR-AN
  • Kichwa: ADABU ZA WASOMAJI QUR-AN
  • mwandishi: USTADH MASOUD SHANI
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 5:53:13 4-9-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

ADABU ZA WASOMAJI QUR-AN

Wasomaji na wanaoishughulikia Quraan wana mtizamo maalum katika dini yao na wana haki ya kufanyiwa hivyo, kwani amana walioibeba ni kubwa ukilinganisha na kitu chengine chochote lau kama tunazingatia. Katika jumla ya matukufu wanayoyopata ni:
" Kuhusishwa moja kwa moja na Allah(S.W) wake na ndio watu aliokhusisha nao(yeye).
" Idadi ya aya za peponi ni kwa mujibu wa aya alizozihifadhi msomaji na kuwa watakao ingia katika waliohifadhi hawapindukiwi na mtu yeyote.
" Malipo ya wasomao Quraan ni kila herufi moja kwa jema moja na jema moja kwa thawabu kumi.
" Mwenye kushikamana kikweli na Quraan hapotei milele.
" Mbora na mtukufu wa watu ni yule aliyejifunza Quraan na kuifundisha.
" Wanaokusanyika na kusoma na kuidurusu Quraan hufunikwa na malaika na kupata rehma na utulivu wa nafsi na Mwenye-ezi-Mungu anajifakharisha kwa watu hao juu ya malaika wake na wanakuwa wageni wa Mwenye-enzi-Mungu muda wa kuwa wapo katika mkusanyiko huo.
" Kuwa karibu na malaika wema
" Tunzo (taji) maalum watavishwa wazazi wa mtoto aliyesoma kuhifadhi na kufuata maamrisho na kuacha makatazo ya Quraan " Uombezi wa Quraan kwa wale wanaisoma na kuioshughulikia

Ni lazima kwa msomaji wa Quraan aifanye hiyo Quraan ndio rutubisho la moyo wake na rekebisho la zile sehemu zilizoharibika katika moyo wake ajiadabishe kwa adabu zake na ajipambe kwa tabia zake Quraan ili atafautike na wale wasioisoma

" Taqwa(uchaji wa Mungu) hii ni adabu inayohitajika kwa siri na dhahiri kwa kumuogopa Mwenye-enzi-Mungu katika vyakula, vinywaji na kivazi na kipato
" Kuwa makini na wakati ulionao na maharibiko ya watu na wakati
" Achunge ulimi wake, achambue anachokisema asijiingize katika mambo yasiyo muhusu na awe mchache wa maneno na mzaha
" Aihadharishe nafsi yake kushindwa na matamanio yake
" Asitukane mtu, hachukii matatizo, Hamfanyii jeuri mtu na hana choyo wala hatii watu aibu

Quraan na Sunna ndio kigezo chake katika tabia njema atunze viungo vyake vyote kutenda yaliyokatazwa, akifanyiwa mambo ya kipumbavu na ujinga hufanya upole. Hudhulumu na akidhulumiwa husamehe, akifanyiwa jeuri hufanya subira, anazuia ghadhabu na hasira, mnyenyekevu, anaikubali haki ikitoka kwa mkubwa au mdogo na anatafuta utukufu kwa Mwenye-enzi-Mungu tu.

Haifanyi Qur-ani kuwa ndio njia kuu ya kipato chake wala haifanyi kuwa ndio sababu ya kutekelezewa haja na shida zake, hajipeleki kwa wafalme, watukufu na matajiri ili wamkirimu,anahakikisha anavaa cha halali kinacholingana naye si mwenye kujifakharisha kwa Quraan, anapokunjuliwa katika mambo ya halali hukunjuka na anapozuiwa hazidishi, ana kinai kidogo kikamtosha, anaishi na kuwatembelea ndugu na majirani, anawatendea wema wazazi wawili, hakasiriki wala hakasirishwi nao katika mambo mema, anaunga ukoo hamfanyii ukali mkosa kwa bahati mbaya.

" Kuzingatia anachokisoma kwa kuhudhurisha moyo na hisia na ufahamu kamili wa kile anachokisoma
" Akisome kwa sauti nzuri alichokihifadhi au anachotaka kukihifadhi
" Kusoma kwa kufuata sheria za usomaji (ahkam) na ujiwekee kawaida (uradi) wa kujisomea kila siku na kusoma polepole.
" Kujumuika na watu wake na majirani kwa kuomba dua mara tu anapomaliza kuisoma Quraan yote, kwani mahala hapo pana dua inayokubaliwa
" Kuanza upya kusoma Al fatiha Al Hamdu mara tu anapomaliza kusoma Qur-ani yote na dua ili usiwepo mwanya katika amali hii tukufu ya kheri.
" Tohara (usafi) wa kiwiliwili, pahala, nguo, kupiga mswaki kabla ya kusoma Quraan pamoja na kuelekea Qibla
" Kulia na kujiliza katika aya za adhabu na kujilinda kwa Mwenye-enzi-Mungu na adhabu hizo na kutoa bishara njema na kuomba dua njema wakati wakusoma aya za rehema na neema.
" Kusujudu Sijdati Ttilawah kisomo anapozipata aya hizo.
" Apende kuisikia Quraan ikisomwa kutoka kwa watu wengine
" Kusoma kwa kukamata Mashaf hata kama umehifadhi.
Ewe Mola tuwezeshe kuisoma Quraan kwa namna unayoridhia na iwe hoja kwetu na isiwe hoja dhidi yetu. - Amin
MWISHO