BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
DINI YA KIISLAMU NI DINI YA HAKI NO2
DINI NDANI YA QUR_ANI TAKATIFU
Katika Qur-ani, neno Dini limekuja na maana mbili, maana ya kijumla, na maana maalumu. Kwa mtazamo wa Qur-ani, neno dini kwa maana ya kijumla limekuja likiwa na maana ya akida na madhehebu, katika maana hiyo, neno hilo limekusanya akida na dini tofauti na sio dini ya Mwenyeezi Mungu, kwa sababu kuna aina mbili za dini. Dini za Nabii Ibrahimu (a.s) (ambazo ndio dini za Mwenyeezi Mungu) na dini zinazotokana au zilizoundwa kutokana na tamaduni za watu. (dini za Makafiri, washirikina.nk.) katika paragrafu hii natushuhudie baadhi ya Aya ambazo ndani yake neno Dini limetumika. Allah (s.w) anasema:-
وَكَذٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ اَوْلاَدِهِمْ شُرَكَآؤُهُمْ لِيُرْدُوهُمْ وَلِيَلْبِسُواْ عَلَيْهِمْ دِينَهُمْ وَلَوْ شَاء اللّهُ مَا فَعَلُوهُ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ[1]
A: Na kadhaalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwauwa watoto wao ili kuwaangamiza na kuwavurugia dini yao. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli penda wasinge fanya hayo. Basi waache na hayo wanayo yazua.
*Maelezo kuhusiana na Aya:-
Makafiri walikuwa wakuwatoa mihanga watoto wao kuwapa masanamu yao, wakiona ni kheri hivyo wanavyofanya.
لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ[2]
B: Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
*Maelezo kuhusiana na Aya:
Makafiri wa Makka walipojiona wamechoka, hawawezi kuzima nuru ya Uislamu, na wakamuona Mtume (s.a.w.w) kila siku anazidi hima katika kazi yake, na dini kila siku inaendelea mbele,walimwendea Mtume wakamtaka watangamane naye katika ibada, wao wamuabudu Mwenyeezi Mungu mwaka mmoja pamoja naye, na Yeye atangamane nao katika kuabudu miungu yao mwaka mmoja vile vile, yaani mwaka mmoja waabudu Mungu wote na mwaka mmoja waabudu masanamu pia wote! Ndipo iliposhuka sura hiyo.
Na makusudio yake ni haya: Nyinyi mna waungu wenu, na namna ya ibada zenu muabudiazo, na mimi nina Mungu Wangu na namna ya ibada nimuabudiayo. Haiwezekani kutangamanisha baina ya Mungu Wangu wa kweli na miungu yenu ya uongo, wala baina ya ibada yangu ya haki, na ibada zenu za batili, nyinyi mna dini yenu na itikadi yenu, nami nina dini yangu na itikadi yangu.
وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِيناً فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِى الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ[3]
C: Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.
فَبَدَاَ بِاَوْعِيَتِهِمْ قَبْلَ وِعَاء اَخِيهِ ثُمَّ اسْتَخْرَجَهَا مِن وِعَاء اَخِيهِ كَذٰلِكَ كِدْنَا لِيُوسُفَ مَا كَانَ لِيَاْخُذَ اَخَاهُ فِى دِينِ الْمَلِكِ إِلاَّ اَن يَشَاءَ اللّهُ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مِّن نَّشَاء وَفَوْقَ كُلِّ ذِى عِلْمٍ عَلِيمٌ[4]
D:Basi akaanza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akakitoa katika mzigo wa nduguye. Hivi ndivyo tulivyo mpangia Yusuf. Hakuweza kumzuia nduguye kwa sharia ya mfalme isipo kuwa alivyo taka Mwenyezi Mungu. Tunawatukuza kwenye vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.
[1] Surat Al-An-aam Aya ya 137
[2] Surat Kaafiruna Aya ya 6.
[3] Surat Al-Imrani Aya ya 85.
[4] Surat Yussuf Aya ya 76.
MWISHO