MAKAFIRI HAWAWEZI KUWA VIONGOZI WA WAISLAMU
  • Kichwa: MAKAFIRI HAWAWEZI KUWA VIONGOZI WA WAISLAMU
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 21:8:56 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MAKAFIRI HAWAWEZI KUWA VIONGOZI WA WAISLAMU

Mwenyeezi Mungu Mtakatifu katika Surat Al-Imrani Aya ya 28 anasema hivi:-

لاَّ يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ اَوْلِيَاء مِن دُوْنِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَن يَفْعَلْ ذٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللهِ فِى شَيْءٍ إِلاَّ اَن تَتَّقُواْ مِنْهُمْ تُقَاةً وَيُحَذِّرُكُمُ اللّهُ نَفْسَهُ وَإِلَي اللهِ الْمَصِيرُ[1]

Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu. Ila ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao.

Na Mwenyezi Mungu anakuhadharisheni naye. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.

Katika aya hiyo limekuja neon “Tuqaata” yaani taqiyya, likiwa na maana ya kuficha imani ndani ya moyo, na kutamka yaliyo kinyume na hayo.

Katika Aya hiyo Mwenyeezi Mungu (s.w) anawakataza waumini wasiwafanye makafiri kuwa viongozi wao, na akasisitiza katika Aya ya 44,4, na 47 za Suratul-Maidah. Pale Alla (s.w)aliposema:-

إِنَّا اَنزَلْنَا التَّوْرَاةَ فِيهَا هُدًى وَنُورٌ يَحْكُمُ بِهَا النَّبِيُّونَ الَّذِينَ اَسْلَمُواْ لِلَّذِينَ هَادُواْ وَالرَّبَّانِيُّونَ وَالاَحْبَارُ بِمَا اسْتُحْفِظُواْ مِن كِتَابِ اللهِ وَكَانُواْ عَلَيْهِ شُهَدَاء فَلاَ تَخْشَوُاْ النَّاسَ وَاخْشَوْنِ وَلاَ تَشْتَرُواْ بِآيَاتِى ثَمَناً قَلِيلاً وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا اَنزَلَ اللّهُ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.

وَكَتَبْنَا عَلَيْهِمْ فِيهَا اَنَّ النَّفْسَ بِالنَّفْسِ وَالْعَيْنَ بِالْعَيْنِ وَالاَنفَ بِالاَنفِ وَالاُذُنَ بِالاُذُنِ وَالسِّنَّ بِالسِّنِّ وَالْجُرُوحَ قِصَاصٌ فَمَن تَصَدَّقَ بِهِ فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَّهُ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا انزَلَ اللّهُ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ

Na humo tuliwaandikia ya kwamba roho kwa roho, na jicho kwa jicho, na pua kwa pua, na sikio kwa sikio, na jino kwa jino, na kwa majaraha kisasi. Lakini atakaye samehe basi itakuwa ni kafara kwake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu.

وَلْيَحْكُمْ اَهْلُ الإِنجِيلِ بِمَا اَنزَلَ اللّهُ فِيهِ وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا اَنزَلَ اللّهُ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ[2]

Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.

Ammar Bin Yasir ni Sahaba miongoni mwa masahaba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipoadhibiwa na makafiri akauliwa mama yake Sumaiyya, akachukuliwa na baba yake Yasir akateswa mpaka akafa, hapo ndipo alipotamka neon la kufuru, alipofika kwa Mtume (s.a.w.w) akalia alipokumbuka lile neon la kufru akasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu nitauweka wappi uso wangu ili hali mimi nimesema neon la kufru baada ya kuteswa sana nakuniulia mbele ya macho yangu wazazi wangu Baba na Mama!! Mtume (s.a.w.w) akamuuliza:” Unaonaje moyo wako?

Akajibu:umetulia katika imani ya Mwenyeezi Mungu akamteremshia Aya “Anayemkataa Mwenyeezi Mungu baada ya imani yake (ataadhibiwa) isipokuwa Yule aliyelazimishwa hali moyo wake unatulia kwa imani 16:106. Kama anavyosema allah (s.w):-

مَن كَفَرَ بِاللهِ مِن بَعْدِ إيمَانِهِ إِلاَّ مَنْ اُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالإِيمَانِ وَلَـكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْراً فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ اللهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ[3]

Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipo kuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa.

Maelezo kuhusiana na Aya:

Tumeona namna gani waislamu walivyokuwa wakiuawa kwa ajili ya dini yao, wakitambulikana na jamaa zao, Basi hapa wanapewa ruhusa waukatae Uislamu wao kwa ulimi wao tu hivi hapo wanapogunduliwa na jamaa zao ikawa hatari juu yao.

Mtume (s.a.w.w) akamsomea Ayah ii ammar kasha akamwambia: “Basi kama watarudia (kukutesa) rudia (na wewe kuwahadaa kwa maneno ya kufru)[4]

[1] Surat Al-Imrani Aya ya 28

[2] Surat Almaidah Aya ya 44,45,47.

[3] Surat An-Nahli Aya ya 106

[4] Tafsiri ya Ibni Kathiyr,juzuu ya 2, uk,609

MWISHO