KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 8
  • Kichwa: KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 8
  • mwandishi: Hassani Buss
  • Chanzo: mailto:busihassan@gmail.com
  • Tarehe ya Kutolewa: 2:31:17 14-10-1403

KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA

WAJIBU WA MWANAMUME

Sehemu ya nane

MSIMAMIZI WA FAMILIA

MWANAUME USIWE NI MWENYE KUANZISHA UGOMVI

Baadhi ya wanaume wakati wote hutafuta visingizio vya kuona kosa katika kila kitu. Hulalamika kuhusu kila jambo dogo. Kwa nini meza hii chafu? Kwa nini chakula cha mchana hakipo tayari? Kwa nini jagi la maua lipo hapa? Hivi sijasema kabla kwamba visahani vya majivu visiwekwe hapa? Na kadhalika.

Wanaume hushikilia msimamo huu hadi kufika kiasi cha kusababisha ugomvi na migongano ndani ya familia zao, na wakati mwingine familia huvunjika kwa sababu ya tabia yao.

Kama mambo yalivyo hatusemi kwamba wanaume hawana haki ya kuwaambia wake zao nini cha kufanya. Wanawake wanashauriwa kukubali haki hii. Tumesema kwamba wanawake hawatakiwi Kuonyesha kiburi kwa ushauri wa waume zao kuhusu mambo ya familia.

Hata hivyo, wanaume wanatakiwa kutumia mantiki na busara zao. Wao ni walezi wa familia zao na kwa hali hiyo, wanatakiwa kuwa na mwenendo unaostahili.

Kama mwanaume anataka kushiriki kwenye mambo ya familia basi anatakiwa kuwa na mwenendo unaostahili.

Kama mwanaume anatakiwa kushiriki kwenye mambo ya familia basi anatakiwa kufanya hivyo kwa namna iliyofanywa.

Kwa kweli, kwa kuwa mwanaume hana muda wa kutosha kushiriki katika mambo yote yahusuyo nyumba yake na kwa sababu hana utaalamu muhimu kuhusu shughuli hizo, basi ni kwa manufaa yake kumwachia mke wake kazi za nyumbani. Mwanaume anatakiwa kumwacha mke wake afanye shughuli za nyumbani kwa uhuru.

Hata hivyo, wanaume kwa kisingizio cha kutoa ushauri, wanaweza kuwakumbusha wake zao kuhusu mambo fulani bila kuwalazimisha. Mara mwanamke mwenye busara anapoona matakwa ya mume wake hufuatana nayo. Kwa hiyo, mwanaume na mwanamke ambao hujaliana wao kwa wao na familia yao.

Kwa kuzungumza pamoja kwa jinsi ilivyo wanaweza kukubaliana mambo yote. Kwa njia hii, wanawake wengi wapo tayari kukubaliana na matakwa ya waume zao ya mara kwa mara.

Lakini kama kushiriki kwake ni kutafuta dosari na kulalamika mfululizo, basi mke huzoea na kwa hiyo, msimamo huu unakuwa jambo la kawaida na hakuna lolote la maana litakalotokana na hali hiyo.

Mwanamke mwenye mume mlalamikaji, hatakuwa makini naye. Mke anaweza hata asijali mambo yake yanayofaa na muhimu. Atajishauri yeye mwenyewe: Kwa nini nipoteze nguvu zangu, kama mume wangu hatosheki hata kidogo na kazi yangu?

Si tu kwamba hatajali shutuma za mume wake, lakini anaweza hata akalipiza kisasi.

Hapa ndipo ambapo nyumba yao hugeuka kuwa uwanja wa vita. Kushutumiana mfululizo wao kwa wao kutatayarisha uwanja wa kutengana na hivyo familia huvunjika. Katika tukio hili Mwanamke hulaumiwa kwa sababu hata mke aliye na busara na mvumilivu atashindwa kuendelea kuvumilia kwa sababu ya msimamo wa mume wake wa kudhalilisha.

Mwanaume alipiga simu kwenye kituo cha police na kudai kwamba mke wake aliondoka nyumbani kwake miezi miwili iliyopita na kwamba alikuwa anaishi na wazazi wake. Baada ya uchunguzi zaidi, mke wa huyu mwanaume alisema; Mume wangu hapendi mtindo wangu wa kutunza nyumba. Wakati wote hunilaumu kuhusu mapishi yangu na uendashaji wa mambo ya nyumbani. Kwa hiyo nimemwacha ili nipate amani mahali pengine.'"

Wanaume lazima wakumbuke kwamba kazi za nyumbani ni eneo la wake zao kutekeleza wajibu wao. Ni makosa kuwanyang'anya haki yao au kuwageuza kuwa vibaraka. Ni busara zaidi kuwaacha waendeshe mambo ya nyumbani jinsi watakavyo.

Matokeo yake, mke hufanya kazi kwa shauku kubwa, utafurahi na nyumba yako itakuwa makazi ya familia yenye furaha.

Fuatana nami Sehemu ya tisa kanuni za ndoa na maadili ya familia.