KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 5
  • Kichwa: KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA 5
  • mwandishi: Hassani Bussi
  • Chanzo: mailto:busihassan@gmail.com
  • Tarehe ya Kutolewa: 2:8:36 14-10-1403

KANUNI ZA NDOA NA MAADILI YA FAMILIA

WAJIBU WA MWANAMUME

Sehemu ya tano

MLEZI WA FAMILIA

MWANAUME UWE NA TABIA NJEMA

Dunia huchukua mkondo wake kufuatana na mpangilio linganifu. Matukio hutokea na kujidhihirisha moja baada ya lingine. Kuwepo kwetu katika Ulimwengu huu mpana ni kama chembe ndogo ilioko kwenye mwendo na kuathiri chembe nyingine papo hapo.

Uendeshaji wa dunia huu haupo katika uwezo wetu na Matukio ya dunia hii hayatokei kufuatana na utashi wetu. Tangu hapo ambapo mtu hutoka nyumbani kwake asubuhi hadi hapo anaporudi jioni, inawezekana hakubaliani na mamia ya mambo yasiyofurahisha.

Mtu hukutana na matatizo mengi sana katika uwanja wa maisha. Inawezekana mtu akakutukana, na mfanya kazi mwenzake asiye rafiki, utangojea basi kwa muda mrefu mno, umeshutumiwa kwa sababu ya kitu fulani ofisini, umepoteza fedha, au umekabiliwa na tukio lolote ambalo linaweza kumtokea mtu mwingine yeyote popote.

Inawezekana ukakasirika sana na Matukio ya kawaida ya kila siku katika maisha yako hivyo kwamba unafanana na bomu lililotegwa na kulipuka wakati wowote.

Vema, inawezekana ukadhani kwamba huwezi kuwalaumu watu wengine au dunia kwa sababu ya bahati yako mbaya, hivyo kwamba unaporudi nyumbani, unajaribu kutoa nje hasira yako kwa mkeo na watoto wako.

Unaingia nyumbani kwako kama vile 'Ziraili' (Malaika wa kifo) amewasili. Watoto hutawanyika kama panya wadogo mbele yako. Mungu na aepushe mbali kwamba uone kitu fulani kilicho kosewa! Chakula, ama inawezekana kina chumvi nyingi au hakina chumvi, au kikombe chako cha chai hakijawa tayari, inawezekana nyumba chafu, au watoto wanapiga kelele na kwa hiyo unapata kisingizio cha kulipuka kwa hasira ndani ya nyumba yako.

Halafu unamkasirikia na kumpigia kelele kila mtu, unawatukana unawapiga watoto na kadhalika. Wakati huo utakuwa umeigeuza nyumba ya huba na urafiki kuwa Jahannamu iwakayo moto ambamo wewe na familia yako mtateseka.

Kama watoto wanaweza kukimbia kutoka nyumbani na kwenda mitaani, watafanya hivyo, na kama hawawezi kufanya hivyo, basi watahesabu sekunde hadi hapo utakapoondoka nyumbani.

Inaeleweka dhahiri ni mazingira ya kusikitisha na kutisha yalioje yanawatawala familia za aina hii. Kila mara upo ugomvi na mabishano. Nyumba yao kila mara imevurugika. Mke anachukia kuona uso wa mume wake.

Mwanamke anawezaje kuishi kwa furaha na mwanaume mkali na mwenye hasira?

Baya zaidi kuliko yote ni hatima ya watoto ambao watakalia kwenye mazingira hayo. Ugomvi wa wazazi wao kwa hakika utatia kovu kwenye roho na nyoyo zao zilizo nyepesi kuhisi. Watoto wanao wanaopata matatizo kama haya huendeleza tabia ya kuwa aina ya watu wenye hasira, wagomvi wenye huzuni na kuona kila jambo ni baya wakati watakapofika umri wa utu uzima. Hukatishwa tamaa kwenye familia yao na hukengeuka.

Inawezekana wakakutana na mitego ya watu waovu na kuanza kufanya uhalifu wa aina mbali mbali. Inawezekana wakawa na tabia ngumu sana kuelezeka na kuvurugikiwa akili hivyo kwamba wanaweza kuhatarisha maisha ya watu wengine kwa kuua au kujijua.

Msomaji anashauriwa kufanya utafiti wa historia ya maisha ya wahalifu. Takwimu na taarifa za kila siku za Matukio ya uhalifu yote yanaonyesha ukweli huu.

Yote haya yapo kwenye wajibu wa mlezi wa familia ambaye ameshindwa kudhibiti tabia yake na ameitendea vibaya familia yake. Mtu kama huyu kamwe hawezi kuwa na amani katika dunia hii na ataadhibiwa Akhera.

Mpendwa bwana! Hatuna nafasi na hatuwezi kudhibiti mambo ya dunia hii. Mabalaa, shida, na Matukio ya kusikitisha yote ni mambo yanayo ambatana na maisha haya. Kila mtu hupata matatizo wakati mbali mbali. Ni ukweli wa mambo kwamba, mtu hufikia kwenye umri wa baleghe kwa kukabiliana na taabu. Mtu mzima apambane nayo kwa nguvu na lazima ajaribu kutafuta ufumbuzi wake. Binadamu wanao uwezo wa kukabiliana na mamia ya matatizo madogo na makubwa na bila kukata tamaa chini ya mbinyo wa balaa.

Matukio ya dunia si ndiyo sababu ya kutibuliwa kwetu, isipokuwa hasa zaidi ni mpangilio wetu wa neva ambao huathirika na Matukio kama haya na husababisha sisi tukose furaha. Kwa hiyo, kama mtu angeweza kudhibiti hali wakati anapokabiliwa na Matukio ya maisha yasiyofurahisha, hangekasirika na kuchukia.

Fuatana nami Sehemu ya sita ya kanuni za ndoa na maadili ya familia uwe na tabia njema.