MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU
  • Kichwa: MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 17:51:57 1-10-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MSINGI WA QUR_ANI TAKATIFU

Qur-ani ni kitabu kitukufu kilichoteremshwa Na mwenyeezi Mungu ili kuwaongoza watu katika njia njema. Katika kitabu hicho kuna misingi muhimu inayomuwezesha mwanaadamu kutambua hadafu na madhumuni ya kuja katika ulimwengu huu.

MSINGI WA KUFAHAMU QUR_ANI.

Tunamshukuru Mwenyeezi Mungu aliyesema katika Qur-ani yake kuwa “Imekujieni – kutokana kwa Mwenyeezi Mungu- nuru kubwa na kitabu (kitukufu), kinachobainisha kila linalohitajiwa, na rehema zake na amani zake zimwendee Mtume wake, bwana Muhammadm, mwisho wa Mitume wote, na sala na salamu ziwaendee Ahlulbayt wake.

Kabla hatujaelezea msingi wa kufahamu Qur-ani sioni vibaya kuashiria sifa za baadhi ya sura zilizomo ndani ya Qur-ani, na kama muda utaturuhusu basi nitafafanua na kuelezea msingi wa kufahamu Qur-ani, na kama muda hautukuruhusu basi nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuelezea msingi wa kufahamu Qur-ani katika makala zitakazofuata.

 Sifa za Sura Al-Hamd (Al-Fatihah)

Miongoni mwa Sura za Qur’ani Tukufu, Sura hii inayo hadhi ya juu, ambayo hunyanyuka kutoka kwenye sifa zifuatazo:

1. Uzito wa Sura hii:

Kimsingi, sura hii inayo tofauti iliyo wazi na sura zingine za Qur’ani Tukufu kutokana na mtazamo wa uthabiti na uzito, kwa sababu sura zingine zote zinatoka kwenye usemi wa Mungu ambapo Sura hii inatoka kwenye ulimi wa waja.  Na kutoka kwenye Mtazamo mwingine katika Sura hii, Mungu amewafundisha waja wake namna ya kusema na kuwasiliana na Yeye”

Utangulizi wa Sura hii umeanza na kumsifu na kumtukuza Mola Mlezi.

Inaendelea na imani  mwanzoni na baada ya maisha ya hapa duniani (kumtambua Mungu na imani katika ufufuo), inaisha na mahitaji na masharti ya waja.

Wakati mtu mwenye hadhari, ambaye moyo wake umezinduka anasoma sura hii huhisi kwamba amewekwa kwenye mabawa na manyoya ya malaika, kwamba ananyanyuka kwenda mbinguni, na kwenye uwanja wa kiroho, hatua kwa hatua, anasogea karibu zaidi kwa Mungu (s.w.t.).

Hili ni wazo bora sana, kwamba Uislamu, katika kukinzana na mifumo mingi ya imani za uwongo (ambapo husemekana kwamba wapatanishi wameteuliwa kati ya Mungu na muumbo,) umetangaza kwa wanadamu kwamba bila ya mpatanishi wanatakiwa kuanzisha uhusiano na Muumbaji wao!. Sura hii ni mfano, ambamo uhusiano huu wa karibu kati ya Mungu na wanadamu imeegemezwa (bila ya wapatanishi), kati ya vilivyoumbwa na Muumbaji.  Mahali hapa yeye (mja) humuona Yeye tu, husema Naye tu, husikiliza ujumbe Wake kwa masikio yake na mwili wake, hivyo kwamba hapana hata Mtume au Mjumbe au mmoja wapo wa Malaika wa karibu sana anakuwa mpatanishi katika uhusiano huu.  Na inastaajabisha kwamba muunganiko huu na uhusiano wa moja kwa moja wa vilivyoumbwa kwa Muumbaji ni mwanzo wa Qur’ani Tukufu.

2. Sura Al-hamd, Msingi wa Qur’ani Tukufu.

Hadithi ya kutoka kwa Mtume Muadilifu (s.a.w.) tunasoma kwamba, “Al-Hamd ni Msingi wa Qur’ani Tukufu.” Na hii ilikuwa hapo ambapo Jaabir Bin Abdullah Ansari alikuja kumhudumia Mtume (s.a.w.), na Mtume (s.a.w.) alimwambia:-

Ungependa nikufundishe sura iliyobora sana ambayo Mwenyezi Mungu ameiteremsha kwenye Kitabu Chake?’ Jaabir alisema ‘Ndio, na iwezekane baba na mama yangu wajitolee muhanga kwako, nifundishe.’

Hivyo Mtume (s.a.w.) alimfundisha yeye Al-Hamd, ambayo ni msingi wa Kitabu.  Na akaongeza kwamba Sura hii ni ponyo la kila maradhi isipokuwa kifo.’ (Majma’ul bayan, utangulizi wa Sura Al-Fatihah)

Uthibitisho wa usemi huu unakuwa wazi kwa kutafakuri juu ya yale yaliyomo katika sura hii, kwa sababu kwa kweli, sura hii ni mkusanyiko wa yaliyomo kwenye Qur’ani Tukufu yote.  Mojawapo ya sehemu yake inahusu Upweke wa Mungu na kutambua Sifa Zake.  Sehemu nyingine inasema kuhusu yatakayotokea baada ya ufufuo na maisha ya baadaye.  Na sehemu nyingine inasema kuhusu mwongozo na kupotoka, ambao ni msitari wa tofauti, kati ya waumini na wasioamini.  Na pia, hapa inaonesha uwezo kamili wa Mola Mlezi, kituo cha Mamlaka, na ukarimu Wake usio na mwisho ambao hugawa kwenye pande mbili, upande wa ujumla na mahsusi (sehemu za Wingi wa Rehema na Usamehevu.)  Na hivyo hivyo inaonesha masuala ya ibada na utumwa, na kuwaelekeza wao kwenye Asili Yake iliyo takatifu.

Kwa kweli, Sura hii ni mbainishaji wa Upweke wa Asili  (ya Mungu), Upweke wa Sifa (wa Mungu), Upweke wa ibada (kwa Mungu).

Kutoka kwenye mtazamo mwingine, Sura hii inajumuisha viwango vitatu vya imani: kuamini kwa moyo, kushahidilia kwa ulimi na matendo kwa viungo.  Na tunatambua kwamba “Umm” inayo maana ya msingi na mzizi (kwenye fungu la maneno “Umm-ul-kitab” ikiwa na maana ya “Msingi wa Kitabu)

Labda hii ndio sababu ambayo ibn Abbas, mfasiri mashuhuri wa Uislamu, anasema, “Upo Msingi kwa ajili ya kila kitu……….na msingi wa Qur’ani Tukufu ni Al-Fatihah.”

Ni juu ya mwelekeo huu kwamba Mtume (s.a.w.) anasimulia kuhusu sifa za sura hii,

“Kila Muislamu anaye soma Sura hii, thawabu zake ni sawa na yule ambaye amesoma theluthi mbili ya Qur’ani Tukufu (na kwenye simulizi zingine ni thawabu ya mtu ambaye amesoma Qur’ani Tukufu yote), na kama akikariri kwa ajili ya muumini yeyote mwanaume au mwanamke, atakuwa amempa zawadi.” (Majma-ul Bayan, utangulizi wa Sura al-Fatihah.)

Kuhusu sura hii kuwa sawa na theluthi mbili ya Qur’ani Tukufu ni kwa sababu sehemu ya Qur’ani Tukufu inalenga kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), sehemu nyingine, inalenga kwenye Ufufuo na sehemu nyingine ni sharia na amri, na sehemu ya kwanza na ya pili zimo kwenye Sura Al-Hamdu.  Na uhusiano wake (kuwa sawa na) Qur’ani Tukufu yote ni kwasababu, kutokana na mtazamo mmoja, Qur’ani Tukufu yote inaweza kufupishwa katika imani na matendo adilifu, yote haya yamekusanywa kwenye Sura Al-Hamd.

MWISHO