UMUHIMU WA HIJABU KWA MWANAMKE
  • Kichwa: UMUHIMU WA HIJABU KWA MWANAMKE
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 17:52:22 1-10-1403

 BISMILAHIRAHMANI  RAHIYMI                                                                                                                                   KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

HIJABU NA MWANAMKE ANAPOKUA NYUMBANI KWAKE

Uliniandikia kua “ hivi ni kwa nini mwanamke akitaka kusali ni lazima avae hijabu hata kama atakua yupo peke yake ndani ya nyumba”?

Dada yangu daima usisahau ya kua Mola wako siku zote huwatakia waja wake kheri na maslahi, na hakuna hata sheria moja ya Mola wako isiyokua na hekima, ima waja waifahamu hekima hiyo au wasiifahamu, hii ni sheria ya Mwenyezi Mungu, vile vile ndani ya sheria hii mna hekima, na miongoni hekima hizo ni hizi zifuatazo:-

1. Mazowezi ya kumpandisha mtu daraja.

Sala ina fadhila nyingi, na vile vile ni moja kati ya mazowezi ya kumpandisha mtu daraja, ndani ya sala sisi tuna mambo chungu nzima tunayojizoweza nayo, kama vile kumpwekesha Mola, kumkhofu, pamoja na kusoma Qur’ani, basi sala kitu kimoja kilichokusanya mambo tofauti yenye thamani, na hijabu kwa wanawake ndio hivyo hivyo, kama vile Mola asemavyo na Qur-ani inavyosema, hijabu kwa mwanamke huwa inampa thamani maalum mwanamke, na ni moja kati ya mambo yenayomkamilisha mwanamke huyo.

2. Kutangaza rasmi kumtii na kumcha Mwenyeezi Mungu

 Mkuu wa jeshi anawaambia wafuasi wake, “mwanajeshi mzuri na mwenye kujua wadhifa ni lazima siku zote afike uwanjani hali ya kuwa amevaa fomu.

Sasa fikiria iwapo mwanajeshi mmoja atataka kuonana na mkuu wa jeshi wakati anapokwenda Idarani kwake, ikisha yeye avae fomu anapokwenda kuonana nae, kufanya kwake hivyo kutakuwa kutamaanisha kwamba yeye amekubali kufuata amri ya mkubwa wake.

Kwa hiyo basi, kuhudhuria pahali alipokuwepo mkubwa wako huku ukiwa katika utaratibu kamili alioutaka yeye, kutakuwa kunaelezea utiifu wa mtu huyo hata kama hakuzungumza kwa ulimi wake.

Mwanamke muislamu ambaye ameahidiana na Mola wake iwapo atakwenda mbele ya Mola wake na hijabu, kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mola wake basi atakuwa yeye anamtangazia Mola kuwa yeye yuko tayari kufuata amri zake na ameridhika na Mola wake.

WASIA WA MWISHO

Dada yangu we mimi nakutaka uyatie akilini na uyafikirie yale yote niliyokuandikia, na jaribu kufikiria zaidi kwamba dunia ni yenye kupita, ujana nao unakimbia kwa nguvu, kuna wangapi waliokuwa wana ndoto za uzuri na walikuwa wakishindana katika kuolewa na leo wako chini ya udongo, na nyuso zao zilizokuwa nzuri pamoja na miili yao haikubakia isipokuwa mifupa tu, kilichobakia ni amali zao tu, iwapo walitenda amali.

Kila mtu katika shule hii ya dunia ana faili lake, na akimaliza shule faili lake bado litabakia, dunia ni soko wako wenye kufaidika katika soko hilo na wako wenye kula hasara, siku zote katika soko hili hutoka watu na kuingia wafanya biashara wengine, basi kama vile unapokuwa muangalifu unapochagua kitambaa unapokuwa dukani, basi amali na matendo yako kuwa muangalifu nayo, na mwishowe niliyokuandikia katika barua hii yachunguze na uyalinganishe, na Mola wako atakuongoza katika njia iliyo sawa.

MWISHO