BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
HABARI ZA WAOVU
AYA YA 34 KATIKA QUR'AN, YA SUURATUN-NAML, INASEMA:
34. (Malkia) akasema:Hakika wafalime wanapouingia mji,wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili hivyo ndivyo wanavyofanya . Iliposema:"Hakika wafalme wanapouingia mji,wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili" Tunapozungumzia juu ya Watawala,ni muhimu kutaja ijapokuwa kwa ufupi yaliyotokea huko nyuma katika miaka ya arobaini Hijria. Historia makini kabisa,inatwambia kwamba: Muawia alipoandaa kumpeleka Mughira bin Shuuba kuwa gavana wake katika mkoa wa Kuufa,mwaka wa arobaini na moja Hijria,alimwita akamwambia:
{قد أردتُ إ?صائکَ بأشياء کثيرة فأنا تارکها اعتماداً على بصرکَ، ولستُ تارکاً إيصائکَ بخصلة!! لا تترُک شمّ ُ عليَّ وذمّه،والترحّم على عثمان والإستغفارُ له،و العيب على أصحاب عليِّ والإقصاءُ لهُ...........}
"Kwa hakika nilitaka kukuusia mambo mengi sana,lakini nitakuachia wewe na akili yako.Na sitaacha kukuusia jambo moja,usiache kumtukana Ali na kumkashifu,na kumhurumia Uthman na kumuombea msamaha.Na kuwatia aibu watu wa Ali na kuwatenga mbali" Kauli hii au wasia huu wa Muawia kwa Mughira umo ndani ya vitabu vya kihistoria vya Shia na Sunni,Lakini mimi sitakutajia rejea ya wasia huu kutoka katika vitabu vya Shia ili isije kuonekana ni kuwa ni mambo yaliyoandikwa na Mashia hivyo si yakweli,la,nitakachokifanya nitakutajia vitabu vikubwa vya wanahistoria wakubwa na wazito wa Kisunni ili urejee upate zaidi kuhusu wasia wa Muawiya kwa Mughira.
Tazama katika vitabu hivi: 1-Tarekhut-tabari: juzu 4.Ukurasa wa 188.
2-Tarekh Ibn Athir: juzu 3.Ukurasa wa 234.Hivi jamani narudia tena sio vitabu vya Mashia,bali ni vitabu mashuri vya Masunni vya kihistoria,havikuacha kitu ndugu. Kupitia agizo hili,Imam Ali (a.s) alilaniwa kwa muda wa miaka mingi sana.Wafuasi wa Ahlul bayt (a.s) kwa jumla walishambuliwa kwa kutukanwa na kwa kuuliwa kila inapopatikana fursa hiyo.
Katika mwaka wa hamsini na sita Hijriya,Muawiya alianza kumwandaa mwanawe Yazid kushika utawala mahala pake.Akawajenga watu watakao fanya kampeni hii.Katika Mkoa wa Kuufa (ulioko huko Iraq) akaweko Mughira bin Shuuba,basra akaweko Ziyad. kisha Muawiya akaandika barua kwa Mar-wan bin Alhakam kuwa:Kwa hakiki mimi umri wangu umekwisha kukua,na hali yangu imedhoofo,nachelea (isije kuzuka) mgongano katika umma baada yangu,Na nimekwishaona kuwa niwachagulie atakaye kaa mahala pangu baada yangu.Na sikupenda kuamua lolote pasina kushauliana na wewe .
Kwa hiyo,watangazie hili,na unijulishe mtu ambaye atakupinga.Mar-wan akawatangazia watu wote azimio hili,na watu wote wakaafiki ispokuwa watu wanne walipinga wazi wazi,nao ni:Husein bin Ali (a.s) mjukuu wa Mtume (s.a.w),Abdur Rahman bin Abibakar,Abdullah bin Umar na Abdullah bin Zubeir.Muawiya akaitisha mkutano,na akamwambia Dhahhak bin Qays Alfihry kuwa:Watu watakapokutana,mimi nitazungumza,nikisha zungumza,wewe simama umpendekeze Yazid kushika nafasi yangu,na uniombe kwa kusisitiza nikubali pendekezo lako.Kikao kilipokamilika ,walialikwa wote na wote wakaketi katika nafasi zao,Muawiya akatoa Hutuba fupi ya kawaida (kisha) akaketi.Ndipo Dhahhak bin Qays Alfihry akasima akasifu:
Utukufu wa Islam na heshima ya Ukhalifa na haki zake,akaonesha aya inayoamrisha kumtii Mwenyeezi Mungu (s.w) na kumtii Mtume (s.a.w) na kuwatii Watawala.(Qur'an:4:59).
Kisha akamtaja Yazid (L.a) na utukufu wake na elimu yake kwa mambo ya siasa.Akatamka kuwa Amempendekeza Yaziy kuwa Khalifa atakaye shika mahala pa baba yake Muawiya.Akasema ewe Amirul Muuminia(yaani Muawiya) ni jambo la lazima kwa watu wote kumpata mtawala atakaeshika mahala pako baada yako.Na tumechunguza kwa undani (zaidi) kumpata anayestahiki nafasi hii tumemuona ni Yazidi mtoto wa Amirul Muuminiina ni mwenye muongozo mzuri na mwenendo safi,naye ndiye mbora wetu kwa elimu na upole.
Basi mtawalishe mahala pako,na utuwekee alama tutakayoegemea na kutulia katika kivuli chake baada yako.Akasimama Amru bin Said al-Ashdaq akasema kama alivyosema Dhahhak.Kisha akasimama Yazidi bin Al-muq-nai Al-adhary akasema:"Huyu ndiye Amirul Muuminiin,akionyesha kwa Muawiya.Ikiwa atakufa, basi ni huyu,akionesha kwa Yazidi.Na atakaye kataa,basi ni huu,akaonyesha upanga wake"Muawiya akamuuliza Ahnaf bin Qays: Unasemaje?Ahnaf akasema: "Tunakuogopeni ikiwa tutasema kweli, na tunamuogopa Mwenyeezi Mungu (s.w) ikiwa tutasema uongo.Na wewe amirul Muuminiin unamjua zaidi Yazidi katika (mwenendo wake) usiku na mchana.Na katika faragha zake na uwazi wake,na ndani yake na nje yake.Basi ikiwa unamjua na ridhaa ya Mwenyeezi Mungu nay a Umma,basi usishauri chochote jambo hili.Na ikiwa kama unamjua kinyume na (sifa) hiyo,basi usimpe dunia na wewe waelekea Akhera.Sisi hatuna jingine ila kusema:Tumesikia na Tumetii. Ndugu unaesoma:Tazama maneno haya:
Tarekh Ibn Athir: Juz: 3.Ukurasa wa 251. kauli ya kwamba :"Tunakuogopeni tukisema kweli,na tunamuogopa Mwenyeezi Mungu tukisema uongo" tarehe imeshuhudia watu walioadhibiwa na wengi kuuliwa kikatili!!! Mfamo:MUHAMMDA BIN ABIBAKAR AT-TAYMY,ABDUR RAHMAN BIN HASAN AL-ANZY,HUJR BIN ADIYY AL-KINDY NA WENZAKE.Hawa ni baadhi ya waliompinga Muawiya waziwazi,matokeo yake yalikuwaje,ABDUR RAHMAN alipelekwa kwa Ziyad,na akamwamuru amuue kikatili,Ziyad akamzika akiwa hai!!! Tazama:Tarekh Tabar: Juz ya 4,ukurasa wa 206. Tarekh Ibn Athir:Juz3,Ukurasa wa 241-242. HUJR BIN ADIYY NA WENZAKE,walipigizwa chini wakafungwa na kuunguzwa chuma!!! Tazama:Tarekh Ibn Athir,Juz 3.Uk 236.
Muawiya aliagiza askari wake kumkamata MUHAMMAD BIN ABIBAKR AT-TAYMY,akatiwa katika kiriba akawashwa moto mpaka akafa!!! Tazama:Tarekh Tabar:Juz ya 4.Ukurasa wa 79. Tarekh Ibn Ibn Athir:Juz ya 3.Ukurasa wa 180. Haya ni baadhi ya matokeo ya waliompinga Muawiya na haya ndio Maf-humu ya maneno ya AHNAF BIN QAYS aliyomwambia Muawiya kuwa: (Nakhaafu In swadaqna,"yaani tunakuogopeni ikiwa tutasema ukweli". Wale waliomwambia ukweli, umeyaona yaliyowafika.Hii ndio siasa ya BANU UMAYYA ambayo leo ndio inayoongoza duniani kote.
Baada ya vita ya NAHRAWAN kumalizika,Muawiya bin Abi Sufyan aliandaa jeshi lililoongozwa na Busru bin Artaat.Na Dhahhak bin Qays Alfihry naye akakusanya jeshi jingine kubwa,akaunganisha pamoja na lile la Busru.
Muawiya akayaamuru majeshi hao kwenda katika mji ili kuwaua wafuasi wa Ahlul bayt (a.s).Jeshi likaenda Madina,huko liikaua watu wengu, na likafanya fisadi kubwa.Kisha Jeshi likaingia Makka likaua wafuasi wengi wa Ahlul Bayt (a.s). usikose makala ijayo ili ujue Muawiya alipokaribia kufa alimuusia nini mwanae,na imam Husein (a.s) aliupokeaje utawala wa Yazid mwana wa Muawiya,je naye alikubaliana na yazid au alimpinga,na kama alimpinga, Yazid alikabiliana naye vipi? Autor:Tzchali