NAMNA YA KUSWALI SWALA ZA USIKU
  • Kichwa: NAMNA YA KUSWALI SWALA ZA USIKU
  • mwandishi:
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 14:40:20 6-10-1403

NAMNA YA KUSWALI SWALA ZA USIKU

كيفية صلاة الليل

وقتها: من بعد اول الليل الى ما قبل صلاة الصبح.

Wakati wa kuswali Swala za usiku ni baada ya kuingia mwanzo wa usiku, yaani kuanzia saa tano usiku hadi muda ulio kabla ya Swala ya Asubuhi.

النية: أصلي نافلة الليل قربة الى الله تعالى.

Kunuia kwake, Utasema kwenye moyo wako au kwa kutamka: Uswali Nafilatu layli Qurbatan ilallahi ta'ala; Allahu Akbar.

الركعات: 11 ركعة، 8 ركعات تصليها بنية نافلة الليل، تصليها ركعتان تتلوها ركعتان، وتقرأ التشهد خلف كل ركعتان، وركعتان تصليها بنية الشفع وتقرأ التشهد بعدها وركعة الوتر.

Swala za usiku ni rakaa 11, rakaa 8, utaziswali kwa Kunuia Nafilatu layli, utaswali rakaa mbili zenye kufuatiwa na rakaa mbili. Na utasoma Tashahudi baada ya kila rakaa mbili, na ukimaliza rakaa mbili unatoa Asalamu Alaykum warhmatullahi wabarakatuhu.

التفصيل:

Ufafanuzi:

نافلة الليل:

Nafilatu layli:

* الركعة الأولى: بعد النية يقرأ الحمد وسورة الاخلاص.

Rakaa ya kwanza: baada ya Kunuia utasoma Alhamdu, na Kulhuwallahu Ahadu.(Al Ikhlasi)

* الركعة الثانية: يقرأ الحمد و (قل يا أيها الكافرون) ثم يقنت، ويستطيع الدعاء على من ظلمه بان يجازيه الله بما يستحقه في السجدة الأخيرة من الركعتين الأوليتين وبعد السجدتين يتشهد ويسلم، ثم ينتصب واقفاً.

Rakaa ya pili: Utasoma Alhamdu na Kulyaayyuhal kafiruna, kisha unasoma Qunuti, unaweza kusoma dua yoyote ile kama kumuomba Mwenyezi Mungu akunusuru na wenye kukudhulumu na awalipe malipo yanayowastahiki, dua kama hii ataisoma tena katika sajida ya mwisho.

Na hii Du'a ya Qunuti na unayoisoma katika sajida ya mwisho unaruhusiwa kuisoma kwa lugha yoyote.

Kisha baada ya Sajida ya mwisho utasoma Tashahudi na utatoa Salamu. Kisha utasimama.

* الركعة الثالثة الى الركعة الثامنة: يقرأ الحمد وما يشاء بعدها في كل ركعة، وبعد كل ركعتين يتشهد ويسلم ومن ثم يقف، وفي الركعة الثامنة بعد السجدتين يتشهد ويسلم ويسبح تسبيح الزهراء.

Rakaa ya tatu na ya nne hadi rakaa ya nane utasoma Alhamdu na sura yoyote uipendayo, na baada ya kila rakaa mbili utasoma Tashahudi na utatoa Salamu na ukimaliza rakaa ya nane utasoma Tashahudi na utatoa Salamu. Halafu utatulia kwa ajili ya uradi wa Tasbihi Zahara.

Tasbihi Zahara ni kusema: ALLAHU AKBAR ×34 ALHAMDU LILLAHI ×33 SUBHANALLAH ×33

 

* ركعتي الشفع: بعد النية (أصلي ركعتي الشفع قربة الى الله تعالى).

Kisha utasimama kuswali rakaa mbili za Shufa'a, baada ya Kunuia (Uswali rakatay Shufa'a Qurbatan ilallahi ta'ala Allahu Akbar).

الركعة الأولى: يقرأ الحمد وسورة الناس.

Rakaa ya kwanza: Utasoma Alhamdu na Kul Audhubi Rabi Nasi.

الركعة الثانية: يقرأ الحمد وسورة الفلق وتكون من غير قنوت، وبعد السجود يتشهد ويسلم.

Rakaa ya pili: utasoma Alhamdu na Kul Audhubi Rabil Falaqi (unaweza kusoma Qunuti au usisome) na baada ya Sajida ya mwisho utasoma Tashahudi na utatoa Salamu.

* ركعة الوتر: بعد النية (أصلي ركعة الوتر قربة الى الله تعالى) يقرأ بعد الحمد سورة الاخلاص ثلاث مراتوالمعوذتين مرة واحدة،

Utasimama kuswali Rakaa moja ya Witiri: baada ya Kunuia (Uswali raka'atal Witiri Qurbatan ilallahi ta'ala) utasoma baada ya Alhamdu Kulhuwallahu Ahadu mara tatu, Kul Audhubi Rabil Falaqi mara moja na Kul Audhubi Rabi Nasi mara moja.

، ثم يقنت، ثم يستغفر لأربعين مؤمناً بقوله (اللهم اغفر لفلان، اللهم اغفر لفلان … الخ)، ثم يستغفر الله سبعين مرة (أستغفر الله وأتوب اليه)، ثم يقول سبع مرات (هذا مقام العائذ بك من النار)، ثم يقول (العفو) ثلاثمائة مرة، ثم يكبر يركع ويسجد ثم يتشهد ويسلم.

Kisha utasoma Qunuti, kwenye Qunuti utajiombea mahitaji yako na utawaombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu Waumin 40 (mfano: Ewe Mwenyezi Mungu msamehe fulani madhambi yake) unawataja majina yao wote 40, unaweza kwawaja ndugu zako majirani zako rafiki zako hata maadui zako unaweza kuwaombea.

Kisha utaomba msamaha wewe mwenyewe hapo hapo kwenye Qunuti kwa kusema: Astaghafirullaha Waatubu ilayhi mara Sabini.

Kisha utasoma mara saba Du'a hii "HADHAA MAQAMU A'IDHU BIKA MINA NARI: yaani kisimamo hiki najilinda kwa na moto,

Kisha utasema AL AFWA, yaani naomba msamaha, mara 300, kisha utapiga Takbira ya kurukuu na utasujudu, kisha utasoma Tashahudi na utatoa Salamu.

وبعد اتمام ركعة الوتر تدعو بهذا الدعاء بعد الصلاة على محمد و آل محمد:

Baada ya kumaliza rakaa moja ya Witiri, utasoma Tasbihi Zahara, kisha utasoma: Allahumma Swali A'laa Muhammad Waali Muhammadu, mara moja au tatu. Kisha utasoma Du'a hii hapa chini ������

(أناجيك يا موجود كل في كل مكان لعلك تسمع ندائي، فقد عظم جرمي وقل حيائي، مولاي يا مولاي أي الأهوال أتذكر، وأيها أنسي، ولو لم يكن بعد الموت لكفي، كيف وما بعد الموت أعظم وأدهي، مولاي يا مولاي حتى متى والى متى أقول لك العتبي مرة بعد أخرى ثم لا تجد عندي صدقاً ولا وفاء، فيا غوثاه ثم يا غوثاه بك يا الله من هوي قد غلبني، ومن عدو قد استكلب علي، ومن دنيا قد تزينت لي ومن نفس أمارة بالسوء الا ما رحم ربي، مولاي يا مو لاي ان كنت رحمت مثلي فارحمني، وان كنت قبلت مثلي فاقبلني، يا من لم أزل أتعرف منه الحسني، يا من يغذيني بالنعم صباحاً ومساءً ارحمني، يو آتيك فرداً شاخصاً اليك بصري، مقلداً أعمي، قد تبرأ جميع الخلق مني، نعم وأبي وأمي، ومن كان له كدي وسعيي، فان لم ترحمني فمن ذا الذي يرحمني، ومن يؤنس في القبر وحشتي، ومن ينطق لساني اذا خلوت بعملي وسألتني عما أنت اعلم به مني، فان قلت نعم فأين المهرب من عدلك، وان قلت لم أفعل قلت ألم أكن الشاهد عليك، فعفوك عفوك يا مولاي قبل سرابيل القطران، عفوك عفوك يا مولاي قبل جهنم والنيران، عفوك عفوك يا مولاي قبل أن تغل الأيدي الى الأعناق، يا أرحم الراحمين وخير الغافرين.

اللهم اني أستغفرك مما تبت اليك منه ثم عدت فيه، وأستغفرك لما أردت به وجهك فخالطني فيه ما ليس لك، وأستغفرك للنعم التي مننت بها علي وتقويت بها على معصيتك، أستغفر الله الذي لا اله الا الا هو الحي القيوم، عالم الغيب والشهادة الرحمن الرحيم، لكل ذنب أذنبته، ولكل معصية ارتكبتها، اللهم ارزقني عقلا كاملا وعزماً ثابتاً، ولباً راجحاً، وقلباً زاكياً، وعزماً ثابتاً، وقلباً زاكياً، وعلماً كثيراً، وأدباً بارعاً، وأجعل ذلك كله لي، ولا تجعله علي برحمتك يا أرحم الراحمين وصلى الله على محمد و آل الطيبين الطاهرين

Naongea na wewe unayepatikana kila Sehemu, naongea kwako unayesikia maombi yangu, hakika makosa yangu yamekuwa makubwa na nimekuwa mchache wa soni , Mola wangu Ewe Mola wangu, ni vitisho gani navikumbuka na ni vingapi navisahau, lau vitisho hivyo visingekuwa ni baada ya kifo ingetosha, ni ukubwa ulioje wa vitisho hivyo vinapokuwa ni baada ya kifo.

Mola wangu Ewe Mola wangu hadi lini na kwa muda gani nasema kwako mara kwa mara (kwamba nitatii amri zako) lakini hupati ukweli wangu wala utekelezaji Ewe msaada wangu kisha Ewe msaada wangu kwako Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba kutokana na matamanio yaliyonizidi na kutokana na maadui wanaonizonga na kutokana na dunia iliyojipamba kwa ajili yangu, na kutokana na nafsi mbaya isipokuwa nafsi anayoihurumia Mola wangu.

Mola wangu Ewe Mola wangu ikiwa umeweza kuwahurumia wa mfano wangu basi nihurumie na mimi, na ikiwa umemkubalia maombi wa mfano wangu basi nikubalie na mimi, Ewe ambaye siwezi kuacha kujipendekeza kwake kwa mame yangu, Ewe mwenye kunilisha neema Asubuhi na jioni nihurumie, analetwa mtu pekee kwako aliye mbele yangu, anafuata upofu wangu ameniepusha na viumbe, na baba yangu na mama yangu na mwenye kuwa na vitimbi vyangu na mienendo yangu, ikiwa huwezi kuni hurumia ni nani sasa utamhurumia?

Na ni nani ataniliwaza katika upweke wa kaburini, ni nani atausemesha ulimi wangu baada ya kuachana na matendo yangu, na ukaniuliza kutokana na yale unayoyajua kwangu, nikisema ndiyo sasa uadilifu wako nitaukimbiaje, na nikisema sijafanya utasema hivi mimi sikuwa ni mwenye kukuona ulipokuwa ukitenda,?

Basi nisamehe nisamehe Ewe Mola wangu kabla sijavishwa mavazi ya moto, nisamehe nisamehe Ewe Mola kabla sijapelekwa kwenye mioto ya Jahannamu, nisamehe nisamehe Ewe Mola wangu kabla sijafungwa pingu za mikononi na shingoni, Ewe mwenye huruma kwa wenye kuhurumia Ewe mbora wa kusamehe.

Ewe Mwenyezi Mungu nakuomba unisamehe kwa yale niliyotubu tena nikayarudia, naomba unisamehe kwa yale niliyokusudia radhi zako na nikachanganya na yale yasiyokurudhisha, nisamehe kwa neema ulizonineemesha nikapatia nguvu za kukuasi, nisamehe Mola wangu ambaye hakuna Mungu isipokuwa yeye aliye hai mwenye nguvu, mjuzi wa yaliyojificha, na yanayoonekana mwenye huruma mwenye kuhurumia kwa kila kosa nililotenda, na kwa kila maasi niliyofanya, Ewe Mwenyezi Mungu niruzuku akili timamu na malengo ya kudumu na utambuzi mzuri, moyo Mtakatifu, malengo ya kudumu, na moyo uliotakasika, na matendo mema mengi, na adabu nzuri, na unijaaliye hayo yote yawe ya kuninufaisha, na usiyajaalie hayo yote yawe ya kuniangamiza. Kwa huruma zako Ewe mwenye huruma kwa wenye kuhurumia. Allahumma Swali A'laa Muhammad Waali Twayyibina Twahirina.

Swala ya usiku ni kwa muda wote wa maisha yako, siyo siku au mwezi maalum. Mwenyezi Mungu Mtukufu atakulinda na maadui mabalaa na atakuruzuku kwa namna huwezi jua. Na swala hizi za Usiku Katika mwezi wa Ramadan malipo yake ni mara Sabini tofauti na miezi yote.