SHIA NA SWAHABA
  • Kichwa: SHIA NA SWAHABA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 15:2:1 6-10-1403

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI.

MTIZAMO WASHIA KWA MASWAHABA

Wasomi wa Sunni wanautumia mfano huu hasa wa swahaba fasiki (fasiq) Walid kuruhusu kuswalishwa na mtenda dhambi wa dhahiri!! " 'Ali al-Qari al-Harawi al-Hanafi, Sharh Fiqh al-Akbar, chini ya Sura 'Inaruhusiwa kswalishwa na mtu mwema au muovu', Uk. 90 " Ibn Taymiyyah, Majmu' Fatawa, (Riyadh, 1381), Juz. 3, Uk. 281
Lakini kwa nini 'tusisahau yaliyopita?' Wakati tunapoyataja makosa ya maswahaba kama huyu Walid, si kwa sababu ya nia mbaya ya kutaka kusengenya tu, bali ni kwa sababu Waislamu wanahitajika wawe waangalifu sana juu ya wapi wanapopata habari zao kuhusiana na mafunzo ya kiislamu na sunnah za Mtume (s.a.w.w.). Na hii itaweza kupatikana tu kwa kuyaangalia kwa makini sana maisha ya maswahaba wote wa Mtume (s.a.w.w.), na kuziacha tabia zao zenyewe ziseme juu ya maadili na uaminifu wao. Isitoshe, Mtume (s.a.w.w.) tayari ameshatuonya kwamba: " "Nitafika kwenye hodhi (birika) kabla yenu, na atakayepita kwangu atakunywa hapo, na atakayekunywa katika hilo hatahisi kiu. Na watakuja kwangu watu niwajuao na wanijuao, lakini nitatengwa nao, kisha nitasema, 'maswahaba wangu'. Na hapo jibu litakuja, 'Wewe hujui hao walifanya nini baada yako.' Kisha nitasema, 'Basi niwe mbali nao hao waliobadilika baada yangu.'" [Sahih al-Bukhari (Tafsiri ya kiingereza), Juz 8, Kitabu 76, Namba 585]

Mtazamo wa Shia juu ya maswahaba Mashia wanawapenda maswahaba waaminifu wa Mtume (s.a.w.w.) waliosifiwa ndani ya Qur'an. Sifa hizo haziwahusu watu kama Walid bin 'Uqbah ambaye, licha ya kuwa na sifa ya uswahaba, kwa masunni, hawezi kuwa ni mfano mwema au mpokezi wa kuaminika wa sunnah. Kwa hivyo, Shia hawaamini kuwa maswahaba wote ni wazuri, bali hufanya utafiti wa historia ya kila swahaba ili kugundua uaminifu wake juu ya ujumbe wa mtume. Bila shaka walikuwa wengi kama kwa mfano kina 'Ammar, Miqdad, Abu Dharr, Salman, Jabir, na Ibn 'Abbas. Tunahitimisha kwa kipande kutoka katika Dua ya Imam wa nne wa Shia, Imam Zayn al-'Abidin (a.s.) akiwasifu maswahaba hawa watukufu (Mungu awabariki):

Eee Mola! na kwa wale maswahaba wa Muhammad hasa, ambao waliishi naye vizuri, waliopita mtihani mzuri wa kumsaidia, waliomwitika pale alipowafanya wasikie mjadala wa ujumbe wake, aliyejitenga na wenzake na watoto wake kwa ajili ya kudhihirisha neno lake, aliyepambana na kina baba na watoto ili kuimarisha utume wake, na kwa kupitia kwake ushindi ulipatikana; wale waliozingirwa na mapenzi yake, wakitarajia biashara ambayo haina hasara kwa kumpenda; wale walioachwa na koo zao wakati waliposhika udugu wake, na wakanyimwa na jamaa zao walipokuwa wametulia kwenye kivuli cha ujamaa wake; Ee Mungu, usisahau waliyoyaacha kwa ajili yako, na uwafanye waridhike na ridhaa yako kwa ajili ya viumbe waliokusanyika kwako walipokuwa na Mjumbe wako. [Imam Zayn al-'Abidin, Sahifa al-Kamilah, (Taf. ya kiingereza, London, 1988), Uk. 27]

"Enyi mlioamini, kama fasiki akikujieni na habari (msimkubalie) bali pelelezeni (kwanza), msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa ni wenye kujuta kwa yale mliyoyatenda." (Qur'an: Sura 49, Aya 6)
Je maswahaba wote walikuwa wakweli na waadilifu? Mashia ni wafuasi waaminifu wa maswahaba wote wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) walokuwa waaminifu kwa mafunzo yake alipokuwa hai na wakabaki hivyo hivyo hata baada ya kufariki. Kulingana na maoni ya Sunni, hata wale walliomuona Mtume kwa sekunde chache tu ni maswahaba na haifai kuwakosoa. Maoni haya hayaungwi mkono na Qur'an wala ushahidi wa kihistoria, na yakasababisha tofauti kubwa kati ya madhehebu haya mawili.
Ufafanuzi juu ya Swahaba Ibn Hajar al-'Asqalani, mwanachuoni mashuhuri wa Sunni, amefafanua swahaba wa Mtume ni mtu aliyekutana na Mtume (s.a.w.w.), baada ya kuukubali Uislamu, na kufariki akiwa ni mwislamu. Aliongeza pia:
" Wote wale waliokutana na Mtume (s.a.w.w.), bila ya kuangalia, aidha ni kwa muda mfupi au ni kwa muda mrefu,
" Wale waliopokea Hadith kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na wale wasiopokea,
" Wale waliopigana vita wakiwa pamoja na Mtume (s.a.w.w.) na wale wasiopigana,
" Wale waliomuona tu Mtume (s.a.w.w.) lakini hawakukaa kujumuika naye,
" Na wale ambao hawakumuona kutokana na sababu fulani, k.v. upofu n.k.
[Ibn Hajar al-'Asqalani, al-'Isabah fi Tamyiz al-Sahaba, (Beirut), Juz. 1, Uk. 10]
Je maswahaba wote walikuwa waadilifu na wakweli? Masunni wanakubaliana juu ya suala la maswahaba kuwa wote ni waadilifu na wakweli na kwamba wao ndio bora katika umma. Wanavyoni wengi wa Sunni wamesema hivyo, miongoni mwao ni: " Ibn Hajar al-'Asqalani, al-'Isabah fi Tamyiz al-Sahaba, (Cairo), Juz. 1, Uk. 17-22
" Ibn Abi Hatim al-Razi, al-Jarh wa al-Ta'dil, (Hyderabad), Juz. 1, Uk. 7-9
" Ibn al-'Athir, Usd al-Ghaba fi Ma'rifat al-Sahaba, Juz. 1, Uk. 2-3
Lakini ni vigumu kuukubali ufahamu huu kutokana na ushahidi ulio wazi unaoonyesha kinyume nao. Hebu zingatia mfano ufuatao: " "Az-Zubair ameniambia kwamba aligombana na mtu wa Ansari aliyepigana (vita vya) Badr mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu juu ya mkondo wa maji ambao ulitumiwa na wote wawili kwa kumwagilia. Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Az-Zubair, "Ewe Zubair! Mwagilia (shamba lako) kwanza, kasha uwache maji yatiririke kwa jirani yako." Yule Muansari akakasirika, akasema, "Ee mtume wa Mungu! Wafanya hivyo kwa sababu Zubair ni binamu yako?" Hapo rangi ya Mtume ikabadilika (kwa hasira) na akamwambia (Az-Zubair), "Mwagilia (shamba lako) kisha zuia maji mpaka yafikie ukutani (uzungukao mitende). "Kwa hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu alimpa Az-Zubair haki yake kamili. Kabla ya hapo Mtume alitoa hukmu kwa manufaa ya Az-Zubair na yule Muansari lakini yule Muansari alipomuudhi Mtume, akampa Az-Zubair haki yake kamili kulingana na ushahidi wa sharia. Az-Zubair akasema, "Wallahi! Nadhani Aya ifuatayo imeshuka kwa ajili ya tukio hilo: "Naapa wa Mola wako! Wao hawawi wenye kuamini mpaka wakufanye (wewe ndiye) hakimu (mwamuzi) katika yale wanayokhitalifiana." (4:65) [Sahih al-Bukhari (Tafsiri ya kiingereza), Juz 3, Kitabu 49, Na. 871]
Kulingana na madhehebu ya Sunni swahaba huyu wa Mtume (s.a.w.w.) hawezi kukosolewa kwenye sunnah na vitendo vyake kuwa ni mfano wa kufuatwa. Hii, licha ya ukweli kwamba swahaba huyu si kwamba alikataa kukubali hukmu ya Mtume (s.a.w.w.) tu, bali pia alimsononesha na hivyo kusababisha kushuka kwa Aya ya Qur'an. Kwa bahati mbaya, historia ya kiislamu imejaa mifano mingi kama hii ya watu ambao, japokuwa kwa kipimo cha Sunni wanafaa kuitwa maswahaba, lakini vitendo vyao vilikuwa si vya kiislamu. Tabia hii ilionyeshwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.), baada ya kifo chake, au hata nyakati zote! Al-Walid bin 'Uqbah Je aliye muumini atakuwa sawa na yule aliye fasiki? Hawawi sawa. (Qur'an: Surah al-Sajdah (32), Aya 18)
Wafasiri wakuu wa Sunni wanatueleza kwamba sababu ya kushuka kwa Aya hii ilikuwa na tukio ambalo neno "Muumini" lamkusudia Imam 'Ali b. Abi Talib, na "Mfasiki" (fasiq) lamkusudia swahaba wa Mtume (s.a.w.w.) akiitwa Walid bin 'Uqba bin Abi Mu'ayt. " Al-Qurtubi, Tafsir, (Cairo, 1947), Juz. 14, Uk. 105
" At-Tabari, Tafsir Jami' al-Bayan, chini ya ufafanuzi wa Aya hii
" Al-Wahidi, Asbab al-Nuzul, (Toleo la Dar al-Diyan li-Turath), Uk. 291
Tumeshaona Aya ya Qur'an inayowakataza waumini kuamini tu hivi hvi habari zozote zinazoletwa na fasiq: "Enyi mlioamini, kama fasiki akikujieni na habari (msimkubalie) bali pelelezeni (kwanza), msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa ni wenye kujuta kwa yale mliyoyatenda." (Surah al-Hujurat (49), Aya 6)
Ni vizuri kuona kwamba ufafanuzi wa Aya hii waonyesha tukio jingine ambapo Walid huyo huyo alisema uongo juu ya jambo lilisababisha kushuka kwa Aya hii iliyomtangaza yeye kuwa ni mfasiki (fasiq). " Ibn Kathir, Tafsir Qur'an al-'Adhim, (Beirut, 1987), Juz. 4, Uk. 224
" Al-Qurtubi, Tafsir, (Cairo, 1947), Juz. 16, Uk. 311
" Al-Suyuti and Al-Mahalli, Tafsir al-Jalalayn, (Cairo, 1924), Juz. 1, Uk. 185
" Abu Ameenah Bilal Philips, Tafseer Soorah al-Hujuraat, (Riyadh), Uk. 62-63
Japokuwa Abu Amina Bilal Philips asema, "lazima kila siku ichukuliwe hadhari kubwa wakati wa kushughulika na habari iliyopokewa na watu wenye tabia za kutia shaka, ambao uaminifu wao haujathibitishwa, au wale wanaojulikana kuwa ni watenda dhambi". Lakini, tunapata katika Hadith za Mtume (s.a.w.w.) zilizopokewa na Sunni, ziko zilizopokewa na Walid! Mathalan katika: " Abu Dawud, Sunan, (1973), Kitab al-Tarajjul, Bab fi'l-khuluq li'r-rijal, Juz. 4, Uk. 404, Hadith Namba 4181 " Ahmad bin Hanbal, Al-Musnad, awwal musnad al-madaniyyin ajma'in, Hadith 15784
Uovu wa Walid haukuishia wakati wa uhai wa Mtume tu. Aliteuliwa na 'Uthman, khalifa wa tatu, kuwa gavana wa mji wa al-Kufah, ambapo uovu wake uliendelea. Kuna siku aliswalisha Swala ya Alfajiri akiwa amelewa, kuswali rakaa nne badala ya mbili. Kisha yeye aliadhibiwa kwa amri ya 'Uthman. Tukio hili limetajwa katika mapokezi mengi ikiwa na yaliyotajwa hapo juu, pia katika: " Sahih al-Bukhari (Tafsiri ya kiingereza), Juz. 5, Kitabu 57, Namba 45; Juz. 5, Kitabu 58, Namba 212 " At-Tabari, Ta'rikh, (Tafsiri ya kiingereza: History of at-Tabari, The Crisis of the Early Caliphate), Juz. XV, Uk.120

MWISHO