GHADIR KHUM
  • Kichwa: GHADIR KHUM
  • mwandishi: Dr M S Kanju
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 0:2:21 2-9-1403

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI

GHADIR KHUM

Kumetokea nini katika siku ya Ghadir Khum?
Ghadir Khum ni sehemu iliyoko maili kadhaa kutoka Makka katika njia inayoelekea Madina. Wakati Mtume (s.a.w) alipopita sehemu hiyo tarehe 18 Dhul'Hijja (10 March 632) wakati anarudi kutoka Hijja yake ya mwago, aya, "Ewe Mtume fikisha uliyoteremshiwa…." Iliteremshwa, kwa hiyo alisimama ili kutangaza kwa mahujaji ambao alifuatana nao kutoka Makka na ambao walikuwa watawanyike njia panda hapo kila mtu kuelekea sehemu yake. Kwa amri ya Mtume (s.a.w) mimbari maalum ilitengenezwa kwa kutumia matandiko ya ngamia kwa ajili yake. Baada ya Salat ya mchana Mtume .(s.a.w) alipanda mimbari na akatoa Khutuba yake ya mwisho mbele ya mkusanyiko mkubwa kabla ya kifo chake miezi mitatu baadae.

Sehemu ya kuvutia ya Khutuba yake, ni pake alipomchukuwa 'Ali (a.s) kwa mkono wake, Mtume s.a.w. aliwauliza wafuasi wake iwapo yeye ana mamlaka zaidi (awla) kwa waumini kuliko wao wenyewe. Kundi kubwa lile la watu likaitikia kwa sauti kubwa "Hivyo ndivyo ilivyo , Ewe Mtume wa Allah".
Kisha akatangaza: "Yule ambaye kwamba mimi ni (mawla) mwenye kumtawalia mambo yake, huyu Ali vile vile ni (mawla) mwenye mkumtawalia mambo yake. Ewe Allah, kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki, na uwe adui kwa yule ambaye ni adui kwake." Mara tu baada ya Mtume (s.a.w) kumaliza khutuba yake, aya ifuatayo iliteremshwa: "………. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwakamilishieni yangu kwenu, na nimewaridhieni kwamba Uislamu ndiyo dini yenu." (Q:5:3) Baada ya Khutuba yake Mtume (s.a.w) alimtaka kila mtu kula kiapo cha utii kwa 'Ali (a.s) na kumpongeza. Miongoni mwa waliofanya hivyo ni Umar bin al-Khattab, ambaye alisema: "Hongera Ali Ibn Abi Talib! Leo umekuwa bwana wa waumini wote wanaume na wanawake."

Mwarabu mmoja aliposikia tukio la Ghadir Khum, alikuja kwa Mtume (s.a.w) na akasema: "Ulituamrisha tushuhudie kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah na kwamba wewe ni Mjumbe wa Allah, tumekutii. Umetuamrisha kusali sala tano kwa siku, tukakutii.Umetuamrisha kufunga (saumu) mwezi wa Ramadhani, tumekutii. Kisha umetuamrisha kwenda kuhiji Makka tukakutii. Lakini kukutosheka na yote haya yote ukamnyanyua binamu yako kwa mkono wako na ukamuweka juu yetu kama mtwala kwa kusema 'Ali ni mawla wa yule ambaye mimi ni mawla kwake: je, amri hii yatoka kwa Allah au yatoka kwako wewe?"

Mtume (s.a.w) akasema: "Kwa jina la Allah ambaye ndiye Mola Pekee! Haya yanatoka kwa Allah, Mwenye nguvu na Mtukufu" Aliposikia jibu hili aligeuka na kuelekea aliko ngamia wake jike huku akisema: "Ewe Allah! Kama asemayo Muhammad ni sawa, basi vurumisha jiwe juu yetu kutoka angani na tupatie sisi adhabu kali na mateso." Kabla hajamfikia ngamia wake Allah alimvurumishia jiwe ambalo lilipiga juu ya kichwa chake na kupenyeza ndani ya mwili wake na kumuacha akiwa amekufa. Ni katika tukio hili kwamba Allah (swt) aliteremsha aya ifuatayo: "Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea. Kwa makafiri ambayo hapana awezaye kuizuia. Kutoka kwa Allah, Mola wa mbingu za daraja." (Qur'an 70:1-3)

Je, Wanachuoni wa Ki-Sunni wanaliona tukio hili kuwa ni sahihi? Idadi ya mabingwa wa Ki-Sunni ambao wamesimulia tukio hili kwa urefu na kwa Mukhtasari, hushangaza akili! Tukio hili la kihistoria lilisimuliwa na Masahaba 110 wa Mtukufu Mtume (s.a.w) wafuasi wa Masahaba 84 na kisha likasimuliwa na mamia mengi ya wanachuoni wa ulimwengu wa Ki-Islamu, kuanzia karne ya kwanza mpaka kwenye karne ya kumi na nne AH (Karne ya 7-20 AD)

Takwimu hizi hujumuisha tu wapokezi waliomo katika simulizi zilizoandikwa na wanachuoni wa Ki-Sunni!
Sehemu ndogo ya vyanzo hivi inatolewa hapa chini. Wengi wa wanachuoni hawa hawakunukuu tu tangazo hili la Mtume (s.a.w) bali vile vile wanaliita sahihi:
" al-Hakim al-Naysaburi, al-Mustaddrak 'ala al-Sahihyn (Beirut), juzuu 3, uk. 109-110, uk. 133, uk. 148, uk. 533. Ameelezea kwa uwazi kwamba hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa vigezo vya Bukhari na Muslim. al-Dhahabi alithibitisha hukumu yake.
" al-Tirmidhi, Sunan, (Cairo), juzuu 5, uk. 633.
" Ibn Majah, Sunan, (Cairo, 1952), juzuu 1, uk. 45.
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Fath al-Bari bi Sharh Sahih al-Bukhari, (Beirut, 1988), juzuu 7, uk. 61.
" al-'Ayni, 'Umdat al-Qari Sharh Sahih al-Bukhari, juzuu 8, uk. 584.
" al-Suyuti, al-Durr al-Manthur, juzuu 2, uk. 259 na uk. 298.
" Fakhr al-Din al-Razi, Tafsir al-Kabir, (Beirut, 1981), juzuu 11, uk. 53.
" Ibn Kathir, Tafsir Qur'an al-Adhim, (Beirut) juzuu 2, uk. 14
" al-Wahidi, Asbab al-Nuzu, uk.l64.
" Ibn al-Athir, Usd al-Ghaba fi Ma'rifat al-Sahaba, (Cairo, 1932), juzuu 3, uk.92.
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Tahhdib, (Hyderabad, 1325), juzuu7, uk. 339.
" Ibn Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, (Cairo, 1932), juzuu7, uk. 340, juzuu 5, uk. 213.
" al-Tahawi, Mushkil al-Athar, (Hyderabad, 1915), juzuu 2 uk. 308-9.
" Nur al-Din al-Halabi al-Shafi'i, al-Sirah al-Halabiyya, juzuu3, uk. 337.
" al-Zrqani, Sharhe al-Mawahib al-Ladunniyya, juzuu 7, uk. 13

MWISHO