DINI YA AHMADIA
  • Kichwa: DINI YA AHMADIA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 23:53:45 1-9-1403


DINI YA AHMADIA

MIRZA GHULAM AHMAD QADIANI

Mwanzilishi wa Ahmadiya. Je,alikuwa mtumishi mwaminifu au alitenda kosa la Jinai
na kufuru dhidi ya Mtume Mtukufu Mohammad?
Kwa yakini wale wanaomuudhi Allah na mtume wake, Allah amewalaani katika
dunia na Akhera na amewaandalia adhabu ifedheheshayo
(Quran: 33:57)
Tunatangaza kuwa:Mirza Ghulam A. Qadiani. Anayejiita masihi/mahdi aliyeahidiwa ametenda kosa la jinai la kufuru dhidi ya mtume Mtukufu MUHAMMAD (SAW) No. 2Changamoto wazi la Mubahila kwa Mirza Qadiani Kiongozi wa Jumuiya ya Ahmadiyya Khalifa wa nne & mjukuu wa Mirza Ghulam Ahmad Qadiani.

Mapenzi juu ya Mohammad (SAW) ni mali adhimu ya kila muislamu yeyote. Ambaye hana chembe ya mapenzi katika moyo wake imani yake sio kamili. Muumini wa kweli ni yule ambaye humtambua Mtukufu Mtume Mohammad (SAW) kuwa ni bora kuliko maisha yake, watoto wake, wazazi wake na hata mali yake yote iliyopo duniani. Ni kwa kuwa na mapenzi makubwa kwa Mtume (SAW) ambayo hata mja asiyemcha Mungu hatavumilia shutuma yeyote kwa Mtume (SAW). Hali hiyo imefikia kwamba kila wakati Rajpal anaposema maneno mabaya dhidi ya mtume basi Ghazi Alan hufa shahiid kwa ajili ya Mtume wake. Makafiri daima wamekuwa wakiwalinda wahuni wamtukanao mtume. Salman Rushdi na mwanamama Tasleema Nasrin ni mfano wa waandishi waliolindwa na makafiri baada ya kudhihirisha chuki zao kwa Mtume (SAW). Mirza Ghulam Ahmad Qadiani Mwanzilishi wa jumuia ya Ahmadiyya ni mtu mmoja aliyeshamiri chini ya usimamizi na huruma ya Raj wa kiingereza huko India. Maisha yake yote yalitumika katika kuendeleza maslahi ya mabwana zake hali ya kufanya kufuru dhidi ya Mtume Mtukufu (SAW) na Ahlibait na maswahaba wake na mitume wote wengine. Maandishi yake yanatoa ushahidi ulio wazi ya kufuru yake hiyo.

"Aya zifuatazo za Quran takatifu zilizoshuka kumuenzi Mtume Mohammad zilizoshuka kwangu kunitukuza mimi (Roohani Khazain, Juzuu 18 uk.207, Juzuu 17 uk.426/411 Juzuu 22 uk. 110, Malfoozat, Juzuu 1, uk. 141) Katika ufunuo: Mimi nimeitwa Muhammad, mtume wa Allah (mwenyewe) wameniita Mohammad Mtume wa Allah. (Roohani Khazain, Juzuu 18 uk. 216) Mimi ni Adam, mimi ni Nuhu, mimi ni Ibrahim, mimi ni Ishaq, mimi ni Yakub, mimi ni Ismail, mimi ni Musa, mimi ni Issa mtoto wa Maryam, mimi ni Mohammad (Roohani Khazain, Juzuu 22 uk. 521)

PROPAGANDA YA AHAMADIYYA

Walii wa Mtume: Mirza Qadiani Mtumwa wa mtume: Mirza Qadiani Mfuasi wa mtume: Mirza Qadiani. Inawezekana mtumwa kuwa sawa na bwana wake? Je, mfuasi anaweza kumpaka matope kiongozi wake? Hadith yeyote ya mtume (SAW) iliyokinyume na ufunuo wangu naitupilia mbali kama karatasi chafu. (Roohani Khazain, Juzuu 19 uk. 140) Mtume Mohammad (SAW) hakuelewa sura ya Azil Zalah (Roohani Khazain, Juzuu 3 uk. 166) Kwa ajili yake (SAW) Allah alimuonyesha muujiza wa kupatwa kwa mwezi, lakini mimi alinionyesha muujiza wa kupatwa kwa jua na mwezi. Je bado mtanikataa? (Roohani Khazain, Juzuu 17 uk. 71) Ufunuo haukumfahamisha Mtume Muhammad (SAW) juu ya Issa mtoto wa Maryam, Dajjal, Punda wa Dajjal Juuj na Majuuj na Dabbatul Ardh ambapo ufunuo wangu umenifahamisha yote hayo. (Roohani Khazain, Juzuu 3 uk. 473) Ufunuo wa Mohammad (SAW) ulidhihirika kuwa ni uongo (Roohani Khazain Juzuu 3 uk. 472) Muujiza wa Mtume Mohammad (SAW) wa kugawika kwa mwezi sehemu mbili ulikuwa si chochote ila kama kupatwa kwa mwezi.

(Roohani Khazain 2 malfrozat, Juzuu 4 uk. 118) Uislamu wakati wa Mtume (SAW) ulikuwa kama mwezi mchanga na katika wakati wangu ulikuwa kama mwezi mpevu. (Roohani Khazain, Juzuu 16 uk. 184) Mitume wote walikuwa wanafanya makosa ya ufafanuzi, na kila Mtume ameshirikiana nami katika makosa hayo. Mtume Mohammad amefanya makosa. (Roohani Khazain 2 Malfrozat Juzuu 2 uk. 224) Hatuhitaji kalima mpya kwa sababu masihi aliyeahidiwa (Mirzabhula Qadiani) hayuko mbali na Mtume Mtukufu (SAW). Masihi aliyeahidiwa ni Muhammad Rasuulullah mwenyewe, aliyekuja tena ulimwenguni kuutangaza uislamu (Mirza Basheer Ahmad mtoto wa Mirza Ghulam Qadiani). (Review of Religions No-3, Vol.14 page105) Mtume mtukufu Mohammad (SAW) hakwenda mbinguni katika usiku wa Miiraj, hiyo ilikuwa ndoto tu. (Roohani Khazain2 Malfrozat Juzuu 4 uk. 118)

USHAIRI
Mohammad amekuja tena miongoni mwetu. Ni mtukufu kuliko alivyokuwa zamani. Atakayekumwona Mohammad wa kweli na amtazame Ghulam Ahmad Qadiani, (Akbar Paigham uslulh, Lahorea tarehe 14 march 1916). Mahali pa Mubahila: Makao makuu ya jumuia ya Ahmadiyya, "Alfazl Masjid" 16-18 Gressnhall Road, London sw 18. Tarehe & Wakati : Kwa nafasi yake Mirza Twahir Ahmad wakati wowote katika miezi 3 kutoka tarehe ya tangazo hili (1 May 1995) Makundi yote mawili yataapa kwa Quran takatifu mbele ya umma utakaohudhuriwa na wawakilishi wanne kutoka kila upande kwamba: "sisi sote tunakula kiapo kwamba kwa mujibu wa maandishi ya Mirza Ghulam Ahmad Qadiani ametenda kosa kubwa la jinai la kufuru dhidi ya mtume mtukufu Mohammad.

Mirza Ghulam kwa upande wake ataapa kwamba: "Mirza Ghulam Ahmad Qadiani alikuwa mfuasi mwaminifu wa mtume mtukufu Mohammad (SAW) na kwamba hajatenda kosa lolote baya la jinai la kufuru dhidi yake. Baada ya viapo hivi makundi yote yataomba laana ya Allah kwa kusoma maneno yafuatayo ya Qurani takatifu. Mpendwa Tahir Ahmad, Khalifa wa nne aliyejisimika mwenyewe katika kulinda heshima na utakatifu wa Mtume Mohammad (SAW) tumejitokeza uwanjani. Kwa kukwepa kwako kufanya mubahila nasi safari iliyopita umeonyesha na kuthibitisha kuwa ajiitaye Mtume/Mahdi/ Masihi Mirza Ghulam A.Qadiani alikuwa mnafiki halisi. Sasa tunakupa nafasi nyingine ya kurudisha heshima ya baba yako "masihi aliyeahidiwa". Kama kweli wewe ni Khalifa wake wa kweli na unamdhania kuwa ni mkweli katika madai yake mengi, basi kuwa jasiri na ujitokeze kukutana nasi katika mubahila. Nakukumbusha kuwa kukaa uso kwa uso kwa ajili ya mubahila, baada ya kupanga wakati na mahali maalumu ni Sunnah ya Mtume wangu Mtukufu Mohammad na ni njia ya huyo mtu wenu ajiitaye mtume Mirza Qadiani anasema: "Hivi sasa amka na jiandae kwa mubahila …………..na itakuwa kwamba, baada ya kuweka muda na mahali nitachukua karatasi zangu za ufunuo nilizoandika na nitaingia uwanja wa mubahala".

(Roohani Khazain, juzuu 11, uk.65) Mirza Twahir, kumbuka kuwa kukwepa kwepa mubahila kwa kisingizio chochote kile kwa mara nyingine kutathibitisha kuwa Mirza Ghulam A. Qadiani alikuwa mwongo na hadithi zake za mapenzi na mahaba juu ya Mtume Mtukufu (SAW) huelezwa kuwazuga watu wasiojua lolote. Na kwa jinsi hiyo kuwapokonya fedha kusaidia familia ya Qadiani na shirika lenu la biashara la Ahmadiyya ili kulipia harakati za mabwana zenu. Inshallah siku itakuja ambapo uovu huu utavuta pumzi yake ya

MWISHO