UDHUU KWA MTAZAMO WA QUR’ANI NA SUNNA 6
MWENDELEZO WA MAKALA ILIYOPITA
MAJINA YA SWAHABA NA TABIINA WAJULIKANAO WASEMAO KUPAKA
Bila shaka umejua riwaya zionyeshazo lazima ya kupaka katika udhu, na zimeelezwa na wajulikanao miongoni mwa Swahaba na Tabiina na wamezinakili wenye vitabu (vijulikanavyo kuwa ni Sihahi), na pia wenye masaniidi.
Ili kumjulisha msomaji majina yao na kiasi cha nafasi zao katika kunakili, twataja majina yao pamoja na kudokeza wasifu wao kwa ufupi na kuam- batanisha na namba za semi zao. Ili msomaji aelewe kuwa wasemao hivyo ni kundi la Swahaba na Tabiina na vilele vya waamininiwa:
Imam Ali bin Abi Talib (a.s,) na kuwa yeye alayhisalam alisema:
(Lau kaana diinu bir ra’ayi la kaana baatinul’qadamayni ahaqu bil’- mas’hi min dhahirhumaa, laakin ra’aytu Rasuulallahi (s.a.w.w.) masaha dhwahirahumaa. (Angalia Hadith 6).
Imamu Al-Baqir (a.s.) Muhammad bin Ali bin al Husayni al-Imamu athab- tu al-Hashimiy al-Alawiy al Madaniy ni mmoja miongoni mwa waju- likanao.
Ameeleza kutoka kwa baba yake, na alikuwa Bwana wa Baniy Hashim katika zama zake alikuwa mashuhuri kwa al’Baqir kwa ajili ya kauli yao: Baqaral ilma, yaani shaqahu, fa alima aswilahu wakhafiyahu (Tazama Hadith 21).
Bisru bin Said, ni Imamu Al-Qudwatu Al’Madaniy, ni maula wa Baniy Al’Hadhramiy, alihadithia kutoka kwa Uthmani bin Affan: Yah’ya bin Muinu na An-Nasaiy walimthibitisha, Muhammad bin Sa’ad alisema:
“Alikuwa miongoni mwa wanaibada wenye kujitenga na watawa, mwenye Hadith nyingi.
(Angalia Hadithi ya 1).53
Hamranu bin Aabaanu yeye ni maula wa Uthman bin Affan, aelezea kuto- ka kwake (Angalia Hadith 2) na alikuwa miongoni mwa wanaojulikana, Ibn Habaan ameeleza kuwa ni miongoni mwa waaminiwa.54
Uthman bin Affani, imetangulia katika Hadithi (1 na 2) kwa kweli yeye alikuwa anatawaza na anapaka juu ya miguu yake na akisema: “Huu ni wudhuu wa Mtume wa Mungu (s.w.t.).
Abu Matar, Ibn Haban alimtaja kuwa ni miongoni mwa waaminifu, Al’Hujaaj bin Artwa’atu amechukuwa riwaya kutoka kwake (Taz. Hadith 3).
Abdullah bin Zaid Al-Maazniy mwenye Hadithi ya wudhu kutoka kwa maswahaba bora hujulikana kuwa ni Ibin Ummi Ammaratu. Ibin Habani amemtaja kuwa yu miongoni mwa wanaoaminika. (Angalia Hadithi 3).
Anizalu bin Sibra Al-Hilaliy Al’Kuufiy, ameeleza kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na kwa Ali (a.s.) (Angalia Hadithi 30) Na Uthman, Abubakar, na Ibin Mas’ud. Al’Ajaliy amesema: “Ni Kuufiy Taabi’i, mwaminifu miongoni mwa Taabiina wakubwa. Na Ibin Habani amemtaja kuwa yu katika waaminiwa.55
Abdu Khayr bin Yaziid, Al’Ajaliy alisema kuwa: Ni mtu wa Kuufa Taabi’i mwaminifu. Na Ibin Haban alimtaja kuwa ni miongoni mwa waaminiwa mataabi’i Abdu Swamadu bin Sa’id Al’Himswiy amekata shauri kuwa ni mkweli muaminifu katika kitabu As-Swahaba. (Angalia Hadithi 6).
Ubaadu bin Tamim bin Ghaziyah al’Answariy al’Khazrajiy al’Mazniy: Ameeleza kutoka kwa baba yake na kwa ammi yake Abdullahi bin Zaid na kutoka kwa Uwaimiru bin Saadi, alimsema kuwa mkeli: al’Ajaliy na An- Nasaiy na wengine, na habari yake ndani ya As-Sahihayni (Al-Bukhariy na Muslim) na ibun Habani kuwa ni miongoni mwa mkweli (angalia Hadithi 10,5).
Abdullah bin Abbas bin Abdul Muttalib bin Hashim ibun Abdi Manaafi, alikuwa anaitwa Al-Baharu kwa wingi wa elimu yake, na aliitwa Hibrul’Ummah. Na Abdullah bin Utbah alisema: Ibin Abbas amewazidi watu kwa mambo kadhaa: Kwa elimu alizowapita, na fiq’hi iliyohitajika kutoka rai yake, na alisema: Sikupata kumuona yeyote aliyekuwa mjuzi zaidi ya kumshida katika Hadithi za Mtume wa Mungu kuliko yeye. Wala mwenye uelewa zaidi katika rai kutokana na yeye, wala mjuzi zaidi wa tafsiri ya Qur’an kuliko yeye56 (Angalia Hadith 13,19).
Ausi bin Abiy Ausi At-Thaqafiy: Kutoka kwake As’habu Sunanu wanne wameeleza riwaya, Hadithi sahihi katika riwaya za Shamiyina kutoka kwake. (Angalia Hadithi 11).
Asha’abiy: Aamiru bin Sharahiil bin Abdi, yeye ni Imamu Al’Hafidhu, Al’Faqih, Al’Mutaqiy, ni ustaadhu wa Abiy Hanifa na ni Sheikh wake. Ahmad bin Hambali na Al’Ajaliy walisema: Hadith mursalu ya Asha’abiy ni sahihi, kwa sababu yeye haelezei Hadith mursalu isipokuwa iliyo sahi- hi. Ibin Uyainah alisema: Wanavyuoni ni watatu: Ibin Abbas katika zama zake, na Asha’abiy katika zama zake, na Athauriy katika zama zake.57 (Angalia Hadithi 22, 23, 24, 28).
Ikrimah: Abu Abdillah Al-Madaniy Maula wa Ibin Abbas, Ibin Haban amemtaja katika thiqaatu. Na alisema: Alikuwa miongoni mwa wanazuoni wa zama zake kwa fiq’hi na Qur’an, na Jaabir bin Zaid alikuwa akisema: Ikrima ni miongoni mwa wanazuoni, wameeleza kutoka kwake As’habu Sunanu wa nne Hadithi zilizo sahihi.58 (angalia20, 25).
Rifaatu bin Raafiu bin Maliki bin Al’Ajalani Abu Mu’adhi Azzarqiy, ali- hudhuria Badri. Na alikuwa na riwaya kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). Alikufa mwanzoni mwa ukhalifa wa Muawiyah. Ibin Haban alimtaja miongoni mwa waaminifu.59 (Angalia Hadithi ya 7,12).
Urwatu bin Azzubair bin Al’Awamu Al’Qarashiy nduguye Abdullahi bin Az-Zubair, Faqiihun, Aalimun.
Na alikuwa miongoni mwa wana wa Madina waliobora na miongoni mwa wanazuoni wake. Ibin Haban amem- taja miongoni mwa waaminifu.60 (Angalia Hadith 14).
Qutaadatu bin Azizi, Al-Haafidh, Al’Alammah Abul’Khataabi Asadusiy Al-Baswariy Adhwariru Al’Akmah Al’Mufasiru. Amesema Ahmad bin Hambal: Qutada ni mwanachuoni wa tafsiri na wa tofauti za wanazuoni. Na alimsifu kuwa ni mwenye kuhifadhi. Na alienda mbali zaidi kumueleza. Na alikuwa mwenye hifadhi mno miongoni mwa watu wa Basra. Alifariki huko Wasiti katika (Kitongoji cha Twauni) mwaka118 A.H.61 na Ibin Habaan amemtaja kuwa ni miongoni mwa waaminifu. (Angalia Hadith 26).
Anas bin Maliki Ibn Anadhwar mhudumu wa Mtume (s.a.w.w.) alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) akiwa kijana wa miaka kumi, na alifariki (s.a.w.w.) naye akiwa na miaka ishirini. Alihamia Basra na alikufa huko mwaka 91 A.H. (Angalia Hadith18).
Musa bin Anas bin Maliki, Qaadhi wa Basra, anaeleza riwaya kutoka kwa baba yake. Kutoka kwake Mak’hulu na Hamiidu Atwawilu walichukua riwaya,62 (Angalia Hadithi 27).
Husain bin Jundab al’Kuufiy al’Janbiy (Abu Dhwabyani al’Kuufiy) Anaelezea riwaya kutoka kwa Ali bin Abi Talib na Salmani. Kutoka kwake wamechukuwa riwaya: Ibrahim na al’Aa’mashi. Amekufa mwaka 56 A.H. Ibn Habani amemtaja miongoni waaminifu. (angalia Hadithi 31).
Jubayr Ibn Nufayri bin Malik bin Aamir al’Hadhramiy. Anachukua riwaya kutoka: Kwa Abu Dharr na Abu Dar da’u. Kutoka kwake wamechukua riwaya watu wa Shaam. Kuniya yake ni Abu Abdir Rah’mani, alifariki mwaka 80 A.H. huko Shaam. Ibin Haban amemtaja katika waaminifu. (Angalia Hadithi 15).
Ismail bin Abiy Khalid al’Bujaliy al’Ah’masiy Abu Abdillahi Al’Kuufiy. Al-Ajaliy amesema: Alikuwa mtu mwema mwaminifu, thabiti, na alikuwa mkosoaji. Marwan bin Muawiyah alisema: Ismail alikuwa akiitwa Al- Mizan. Alikufa mwaka 146 A.H.63 (Angalia Hadithi 29).
Tamimu bin Zaid Al’Maazniy, Abu Ubadu Al’Answariy katika Bani An- Najaar, amekuwa Swahaba, Hadithi zake ziko na mwanawe.64(Angalia Hadith 5,10).
At-Twau al’Qudahiy, anachukua riwaya kutoka kwa Abdillah bin Umar, na Urwa bin Qays amechukua kutoka kwake, baba yake Ya’aliy bin Atwa’u, Ibnu Haban amemtaja kuwa ni miongoni mwa waaminifu. (Angalia Hadithi 11).
Abu Maliki al’Ash’ariy: al’Harithu bin Al-Haarithi al’Ash’ariy Ash- Shaamiy Aswahabiy, ameelezea Hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na kutoka kwake Abu Salamu al’Aswadu. Kuniya yake ni Abu Maliki, na alikufa katika khilafa ya Umar. (Angalia Hadithi 9).
Kama utastaajabishwa basi ya kustaajabisha ni kauli ya Ash-Shaukaniy, aliposema: “Haikuthibiti kutoka kwa mmoja yeyote miongoni mwa swa- haba kinyume na hivyo (yaani kuosha) isipokuwa Ali na Ibun Abbasi na Anas.65
Isipokuwa itikadi yake kuhusu kuosha imemzuia kutafiti na kufuatilia katika vitabu vya Sunanu na Masaaniidu.
WUDHU WA MTUME (S.A.W.W.) KUTOKA USEMI WA MAIMAMU WA NYUMBA YA MTUME (S.A.W.W.)
Kwa kweli Maimamu katika Ahlu-bayt ni rejeo la pili ya Waislamu baada ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuhusu walilohitilafiana (Waislamu), kwa kuwa wao ni wahifadhi wa Sunna ya Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) na ni kasha la elimu yake, kwa hakika Mtume (s.a.w.w.) ameagiza hivyo katika Hadithi ya Thaqalayni ambayo Waislamu wameafikiana kuinakili na usahihi wake na amesema (s.a.w.w.):
“Kwa hakika nimeacha kati yenu vitu viwili vya thamani: Kitabu cha Mungu na Kizazi changu.” Ikiwa hii ndio nafasi ya Ahlu-bayt naturejee kwao kuhusu jinsi ya wudhu wa Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) kwa kuwa wao wamefyonza kutoka maji baridi yanayokimbia na walihifadhi Sunna ya Mtume kwa kunakili mkubwa kwa mkubwa, na hapa yanakuijia waliy- oyaeleza yakujia:
1- Kutoka kwa idadi kadhaa ya swahibu zetu, kutoka kwa Ahmad bin Muhammad na Abi Daudi wote kutoka kwa Husein bin Sa’id kutoka kwa Fadhwalatu kutoka kwa Daud bin Farqad, alisema: “Nilimsikia Abu Abdillah akisema: Kwa kweli baba yangu alikuwa anasema: Kwa hakika wudhu una mpaka, mwenye kuuvuka hatopata malipo. Mtu mmoja aka- muuliza: “Mpaka wake ni upi?” Akasema: “Utaosha uso wako na mikono yako miwili, na utapaka kichwa chako na miguu yako miwili.”66
2 - Ali amenakili kutoka kwa baba yake, na kwa Muhammad bin Ismail, kutoka kwa al’Fadhlu bin Shadhani, wote kutoka kwa Hamadiy bin Isa, kutoka kwa Harizu, kutoka kwa Zurara alisema: “Abu Ja’far (a.s.): (Ala ahkiy lakum udhua Rasuulillahi (s.a.w.w.)? Qulna: Balaa.) (Je, nisikuonyesheni wudhu wa Mtume wa Mungu (s.a.w.w.)?” Tukasema: “Ndio tuonyeshe,” akaagiza chombo chenye maji kidogo, akakiweka mbele yake, halafu alipania dhiraa zake na aliingiza kiganja chake cha kulia, kisha akasema: “Ni kama hivi ikiwa kiganja kiko tohara,” kisha aliteka na kukijaza maji na aliyamwagia kwenye paji la uso wake na akasema: (Bismillah) na aliyaeneza kwenye ncha za ndevu zake, kisha ali- upitisha mkono wake usoni kwake na juu ya paji la uso wake mara moja, halafu alitumbukiza kiganja chake cha kushoto akateka na kukijaza, kisha alikiweka kwenye kiwiko chake cha kulia na alipitisha kiganja chake kwenye dhiraa yake mpaka maji yalitiririka kwenye ncha za vidole vyake, na alipaka mbele ya kichwa chake na juu ya nyayo zake kwa umajimaji wa kiganja chake cha kulia na baki ya umajimaji wa kushoto.
Alisema: Na Abu Ja’far alisema (a.s.): (Kwa hakika Mungu ni Witri anapenda witiri, yaweza kukutosheleza maji miteko mitatu: Mmoja kwa ajili ya uso na miwili kwa ajili ya dhiraa mbili, na kwa umajimaji wa mkono wako wa kulia utapaka kichwa na umaimaji uliobakia utapaka juu ya unyayo wako wa mguu wa kulia, na utapaka kwa umajimaji wa kushoto wako juu ya unyayo wako wa kushoto).
Zurara alisema: “Abu Ja’far (a.s.) alisema: (Mtu mmoja alimuuliza Amiirul’Muuminiina wudhu wa Mtume wa Mungu (s.a.w.w.). Alimuonyesha kama hivi).67
3 – Ali bin Ibrahim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn Abiy Umair, kutoka kwa Umar bin Udhayna, kutoka kwa Zurara na Bakiir kuwa waw- ili hawa walimuuliza Abu Ja’far (a.s.) kuhusu udhu wa Mtume wa Mungu (s.a.w.w.) aliagiza chombo ndani yake muna maji, aliutosa mkono wake wa kulia aliteka mjazo alimwagia usoni kwake aliosha kwa mkono huo uso wake, kisha alitosa kiganja cha mkono wake wa kushoto, kwacho aliteka mteko akamwagia kwenye dhiraa yake ya kulia akaosha kwao dhiraa yake kutoka kwenye kiwiko hadi kwenye kitanga cha mkono, haurudishi kwenye kiwiko. Hatimaye alikitosa kiganja chake cha kulia akamwagia dhiraa yake ya kushoto kutokea kwenye kiwiko, na alifanya kama alivyofanya mkono wa kulia. Halafu alipaka kichwa chake na nyayo zake kwa unyevunyevu wa kiganja chake, hakuvifanyia maji mapya, hatimaye alisema: wala asiingize vidole vyake chini ya kanda. Kisha akasema:
Kwa hakika Allah Mtukufu anasema:
(yaa ayyuha lladhiyna Aamanu idha Qumtum ilaswalati fagh’silu wujuhakum wa aydiyakum): Qur:5-6
“Enyi mlioamini mkusudiapo kuswali osheni nyuso zenu na dhiraa zenu…”
Asiache kitu mikononi mwake hadi viwiko viwili ila awe amekiosha kwa sababu Mungu anasema:
Hamae akasema:
Hivyo akipaka kitu kichwani mwake au nyayoni mwake kati ya ka’abu mbili mpaka ncha za vidole itamtosha, alisema. “Tukauliza: Ka’abu mbili zi wapi? Akasema: “Hapa, yaani kwenye mgawanyiko (kati ya unyayo na muundi).” Tukauliza: “Hiki ni nini?” Akasema: “Huu ni katika mfupa wa muundi, na ka’ab ni chini zaidi ya hiyo.”
Tukasema: “Mungu akurekibishe, choto moja latosha kwa ajili ya uso na choto kwa ajili ya dhiraa?” akasema: “Ndio likifika humo, na mawili yanakuja kwa vyote hovyo.
4 – Kutoka kwa idadi kadhaa ya watu wetu: Ahmad bin Muhammad, Ali bin Al’Hakam, Daudi bin An-Nu’uman, Abu Ayyubu, Bakiir bin Ayan, kutoka kwa Abu Ja’far (a.s.)
Alisema: “Je nisiwaonyesheni wudhu wa Mtume wa Mungu (s.a.w.w.),” akachota kwa mkono wake wa kulia gao la maji, kwayo aliosha uso wake halafu aliteka kwa mkono wake wa kushoto gao la maji kwayo aliosha mkono wake wa kulia, halafu aliteka kwa mkono wake wa kulia gao la maji kwayo akaosha mkono wake wa kushoto, hatimaye alipaka kwa mabaki ya mikononi mwake kichwa chake na miguu yake.
HATIMA YA MZUNGUKO HUU
Ukweli umebainika na kudhihiri kwa uwazi wake wote hivyo ni kwa mambo yafuatayo:
Kitabu kimesema kwa sauti ya wazi kupaka miguu na kwamba Qur’an Tukufu haiafikikuosha.
Kwa hakika kundi katika swahaba wajulikanao na vilele katika wao – ambao ni bweta la kuhifadhia Sunna na ni wahifadhi wa athari - walikuwa wakipaka na wanakataa kabisa kuosha, na nimezijua riwaya zao nyingi zinazofikia kusaidiana.
Kwa hakika Maimamu wa Ahlul-bayt, wakiwemo miongoni mwao: Maimamu wawili al-Baqir na As-Sadiq (a.s.) wamebainisha udhu wa Mtume wa Mungu, kuwa yeye alikuwa anapaka miguu badala ya kuiosha, na maneno yao yamekwishapita.
Na (dalili) zilizojulisha kuosha miguu kuna ambazo ni sahihi na dhaifu, bali dhaifu ni zaidi kuliko sahihi.
Hivyo basi ni wajibu wa mwanachuoni agange kupingana kwa riwaya zinazoonyesha kuosha, kwa kuzilinganisha na Kitabu kwanza, pili kuziambatanisha na Sunna zinazoonyesha kupaka.
Kwa hakika Mtume (s.a.w.w.) ndiye aliyewaamuru Waislamu wote kuchukua kauli ya kizazi chake, aliposema: (Inniy taariku fiikum Ath thaqalayni Kitaba llahi wa Itratiy) (Hakika nimeacha kati yenu vizito viwili – vyenye thamani - Kitabu cha Mungu na kizazi changu).
Kwa hiyo kujiambatanisha na kauli zao na Hadith zao ni kutekeleza kauli ya Mtume (s.a.w.w.) naye haitoi ila kwa haki, kwa hiyo mwenye kuvichukua vyenye thamani viwili atakuwa ameshikamana na kitakachomuokoa mbali na upotovu, na mwenye kukichukua kimoja kati ya viwili atakuwa amemkhalifu Mtume.
Ukiongeza kuwa Ali (a.s.), ni mlango wa elimu ya Mtume. Yeye ni maarufu kwa kauli ya kupaka. Na Ar-Raziy anasema katika kuongoka na Ali: (wa man iqtadaa fii dinihi bi Aliyin bin Abiy Talib faqadih’tada,) na dalili juu ya hilo ni kauli yake (s.a.w.w.) (Allahuma adril’haqa ma’a Ali haythu dara.)68 (Ewe Allah izungushe haki pamoja na Ali azungukapo).
Ikiwa ijitihadu maana yake ni kuitumia juhudi katika kuichomoa hukumu kutoka dalili zake za kisharia basi ni kwa nini neema hii kubwa imekua mah’susi kwa maimamu wanne tu, na si wengine? Na vipi imekuwa waliotangulia ndio wastahiki zaidi kuliko waliokuja nyuma?
Haya na yaliyo mfano wake yalazimu kufungua mlango wa ijitihadi katika zama zetu hizi, na kuzingatia kitolewacho na Qur’an na Sunna katika hukumu za maswala haya na mfano wa haya ni miongoni mwa ambayo yatakayokupitia katika mlolongo huu, yakiwa mbali na kauli za maimamu wanne na walio mfano wao.
Kwa kweli ijtihadi ni alama ya kudumu kwa dini na kufaa kwake kulin- gana na hali ya mambo na mazingira na wala si bid’aa ya kuzushwa, bali ilikuwa wazi toka zama za Mtume na baada ya kifo chake (s.a.w.w.) na (mlango wake) ulifungwa kwa sababu za kisiasa mnamo mwaka 665 A.H.
Al’Miqriziy alisema yalipoanza kuzingirwa madh’habu kwa wanne tu: Yaliendelea mamlaka ya maimamu hao wanne tokea mwaka 665 A.H. kiasi kwamba haikubaki katika jumla ya nchi za kiislamu madhehebu ijulikanayo miongoni mwa madh’habu za kiislamu isiokuwa hizi nne, na alifanyiwa uadui afuataye madh’habu isiyokuwa hizi nne, na alikanushwa na wala kadhi yeyote hakupenda wala kukubaliwa shahada ya yeyote kama angekuwa si mfuasi wa mojawapo ya madhehebu hizi.
Na wanavyuoni wao walitoa fatwa katika nchi hizi kipindi chote cha muda huu wajibu wa kuzifuata madhehebu hizi na kuziharamisha zisizokuwa hizi, na kuzitendea kazi hizi mpaka hii leo.69
NA MWISHO WA DUA YETU NI AL’HAMDULILLAHI RABBI L’ALAMIIN.
• 1. Sahih Muslim kwa sherehe ya An-Nawawiy: 3115, Na. 229.
• 2. Sahih Muslim kwa sherehe ya An-Nawawiy: 3115, Na. 230.
• 3. Mafaatiihul'ghaybi au Atafsiyrul'Kabiiru: 3252, chapa ya mwaka1308, Misri.
• 4. Ad-Durul'Manthur: 3403 .
• 5. 1 na 2. Nuru Thaqalayni: 1483.
• 6. 1 na 2. Ad-durul'manthur: 31,4.
• 7. 1na2.2
• 8. At’fur: Ni kiunganishi mfano wa ‘na’ katika Kiswahili. K.m yaani mkirimu Zaid na Amri kwa hiyo na ndio at’fu kama vili katika kiarabu.
• 9. 1 na 2. Mughniy Alabibu, mlango wa nane,Al'qaidah Athania,359.
• 10 Ah'kaamul'Qur'an:2346.
• 11. Al'intiswar:24.
• 12. Ata'awilu:6/112
• 13. Kwa minajili hiyo twaona watembeao miguu wazi miongoni mwa Shia katiyao wafanya kazi- kama wakulima na walio mfano wao nawengine wasiotilia manani usafi wa miguu yao wakati usio wa ibada iliyo na sharti ya tohara- wakusudiapo wudhu huosha miguu yao kisha wana tawadhwa na wapaka juu ya miguu ikiwa safi na mikavu.
• 14. Gazeti'Alfaiswalu N0235 uk,48, maqala ya Abu Abdur rah'mani Adhahiry
• 15. Musnad Ah'mad:1/109, Hadith489.
• 16. Kanzul'ummali:9/439, Al'hadiithu26863.
• 17. Kanzul'ummali:9/439, Al'hadiithu26863.
• 18. Kanzul'umal:9 /448 kwa namba 26908.
• 19. Kanzul'umal:9/429 kwa NO26822
• 20. Musnad Ah'mad :1 N0 937 na 919
• 21. Sunanu Ibn Maajah:1,hadiith 460;Sunanu Annasaaiy:2226.
• 22. Swahihul'Bukhariy:1 23, Babu man rafa'a swautahu bil'ilmi min kitabil'ilmi, Al'hadiith 1.
• 23. Musnad Ahmad: 5 342.
• 24. Sunanu Ibin Maajah:1, Al Hadith 460.
• 25. Tafsiyru Tabariy: 686; Al-Mu'ujamu Akabir: 1221 N0 603.
• 26. Mustadrakul-Hakim: 1241
• 27. Mustadrakul-Hakim: 1241
• 28. Al Khaswaisul Kubraa: 1 94
• 29. Usudul'Ghabah: 5 156
• 30. Musnad Ahmad, Al'hadiith 1018.
• 31. Kanzul Ummal: 5 106.
• 43. Hadithi 18-26, zote zimenakiliwa kutoka Tafsiri ya Tabariy: 6 82.
• 44. Atabariy: Jaamiul'bayani: 6 182. Alqaasimiy: Mahasinu ta'awili: 6 111;
• 45. Ibn Kathiiri Adamashqiy, Tafsiyrul qur'an Aladhiim:2 27.
• 46. Tafsiyrul Qur'an Al'adhwimu: 227.
• 47. Tafsiyrul Qur'an Al'adhweem: 2 25
• 48. Kanzul'ummal:9 435 kwa N026856
• 49. Kanzul Ummal: 5 126.
• 50. Tafsirul'Qur'an Al'Adhwimu: 2518.
• 51. Tafsiru Ruhul'Bayani:351.
• 52. Hivyo hivyo katika toleo, na sahihi ni aliosha.
• 53. Tadhkiratul'hufadh: 1 124. Tah'dhiibu tahdhiibi:9 350, Hilyatul'auliyai:3 180. Shadharatu dhahabi: 1 149. Atabaqaatul kubra ya Ibin Saad: 1 149.
• 54. Ibn Hayyani: Athiqaatu: 4 179.
• 55. Tah'dhiibu Tahdhiibu:10 423; Al'Bukhariy: At-Tariykhu Al'Kabiiru:8117
• 56. Usudul'Ghaabah: 3 192-195.
• 57. Tadhkiratul'Hufaadhu: 1 79,Tah'dhiibu tah'dhiibu: 565, Hilyatul'Auliya'I lil'Asbahaniy:4310, Shadharatu dhahabi: 1126, Twabaqaatul'hufadhu:43.
• 58. Tah'dhiibu tah'dhiibu:7293, Tadh'kiratul'hufaadhu:195, Tah'dhiibul'asmaau:1340.
• 59. Athiqaatu:4240
• 60. Athiqaatu:5194-195. Tadh'kiratul'hufaadhu:192.Tah'dhiibutah'dhiibu:7180.
• 61. Athiqaatu:5321, Albidaya wa nnihayah li ibin Kathiir:9313. Tah'dhiibul'asma'u:257, Tah'dhiibu tah'dhiibu:8337.
• 62. Athiqaatu:5401.
• 63. Tadhkiratul' hufaadhi:1153,, Tahdhiibu tahdhiibu:1291. Al'abar:1203.
• 64. Athiqaatu:341.
• 65. Ashaukaniy: Neilul'autari:1163.
• 66. Alkulayniy: Al'kaafiy: v,3 kitabu twahara, babu twahara babu miqdarul'mai alladhi yujzyi lilwudhui wal'ghusli waman ta'ada fil'wudhui, Al-hadiith.3
• 67. Alkaylaniy: Alkafiy:v 3, kitabu twahara, babu sifatul'wudhui, Al'hadiith 4.
• 68. Ar- raziy: Mafaatiihul'ghaybi:1111.
• 69. Rejea Al'khutatu al'miqriziah: 2 333-344.
MWISHO