UTAMBUZI JUU YA SUALA LA UIMAMU NDANI YA RIWAYA
  • Kichwa: UTAMBUZI JUU YA SUALA LA UIMAMU NDANI YA RIWAYA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 21:55:47 1-10-1403

UTAMBUZI JUU YA SUALA LA UIMAMU NDANI YA RIWAYA

MEZANI HALISI YA KULIELEWA SUALA LA UIMAMU

Hakuna shaka kua kuna hadithi nyingi zilizoelezea sifa za Maimamu (a.s) sifa ambazo zimesababisha kuwatia wasiwasi baadhi ya watu, kwani sifa hizo zimegusia baadhi ya sifa ambazo ni sifa za Mweny enzi Mungu na kuzinasibisha sifa hizo kwa Maimamu (a.s).

Kiasi ya kwamba kumetokea baadhi ya watu waliowapandisha cheo Maimamu (a.s) na kuwapa cheo cha Uungu, limetokea hili baada ya pale watu hawa walipoziona zile Hadithi zinazozungumzia sifa kubwa kubwa za Maimamu (a.s), na watu hawa hawahesabiwi kua ni Waislamu ndani ya dini yetu ya Kiislamu na wastahiki kulaaniwa kwani hao ni washirikina waliomshirikisha Mola wao, na kuna wengine walidai kua Mwenye enzi Mungu amewapa Maumamu kazi za Uungu!, nao hao pia wako katika upotofu vilevile na Maimamu (a.s) wako mbali na watu kama hawa, na kuna wele wengine waliobirukia upande wa pili nao ni wale wenye kudai kkua Maimamu (a.s) ni sawa na watu wengine hawana tofauti yeyote na wayu wengine,nao hawa si waumini wa kweli, ama kuna lile kurupu la watu walio katika njia ilionyooka nao ni wale wenye kuamini kua Maimamu (a.s) ni watu maalumu alioteuliwa na Mola wao ili kuuongoza umma huu nao wenye sifa kamili za kuuongoza umma huu na uadilifu wa Mwenye enzi Mungu hudhihirika kwa kupitia kwao na sifa tofauti za Mwenye enzi Mungu hudhihirika kwa kupitia kwa Maimamu (a.s). na pia Maimamu (a.s) ni watu kama watu wenge isipokua wao ni wateuliwa wa Mwenye enzi Mungu nao si Miungu.

MWISHO