KILICHOTOKEA GHADIIR KHUM
Assalam Alaikum
Jee, kulitokea nini Siku ya Ghadir Khum?
Ghadir Khum ni sehemu iliyoko maili kadhaa kutoka Makka katika njia inayoelekea Madina. Wakati Mtume (s.a.w) alipopita sehemu hiyo tarehe 18 Dhul'Hijja (10 March 632) wakati anarudi kutoka Hijja yake ya mwago, aya, "Ewe Mtume fikisha uliyoteremshiwa…." Iliteremshwa, kwa hiyo alisimama ili kutangaza kwa mahujaji ambao alifuatana nao kutoka Makka na ambao walikuwa watawanyike njia panda hapo kila mtu kuelekea sehemu yake. Kwa amri ya Mtume (s.a.w) mimbari maalum ilitengenezwa kwa kutumia matandiko ya ngamia kwa ajili yake. Baada ya Salat ya mchana Mtume .(s.a.w) alipanda mimbari na akatoa Khutuba yake ya mwisho mbele ya mkusanyiko mkubwa kabla ya kifo chake miezi mitatu baadae.
Sehemu ya kuvutia ya Khutuba yake, ni pake alipomchukuwa 'Ali (a.s) kwa mkono wake, Mtume s.a.w. aliwauliza wafuasi wake iwapo yeye ana mamlaka zaidi (awla) kwa waumini kuliko wao wenyewe. Kundi kubwa lile la watu likaitikia kwa sauti kubwa "Hivyo ndivyo ilivyo , Ewe Mtume wa Allah". Kisha akatangaza: "Yule ambaye kwamba mimi ni (mawla) mwenye kumtawalia mambo yake, huyu Ali vile vile ni (mawla) mwenye mkumtawalia mambo yake. Ewe Allah, kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki, na uwe adui kwa yule ambaye ni adui kwake."
Mara tu baada ya Mtume (s.a.w) kumaliza khutuba yake, aya ifuatayo iliteremshwa:
"………. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwakamilishieni yangu kwenu, na nimewaridhieni kwamba Uislamu ndiyo dini yenu." (Q:5:3) Baada ya Khutuba yake Mtume (s.a.w) alimtaka kila mtu kula kiapo cha utii kwa 'Ali (a.s) na kumpongeza. Miongoni mwa waliofanya hivyo ni Umar bin al-Khattab, ambaye alisema: "Hongera Ali Ibn Abi Talib! Leo umekuwa bwana wa waumini wote wanaume na wanawake."
Mwarabu mmoja aliposikia tukio la Ghadir Khum, alikuja kwa Mtume (s.a.w) na akasema: "Ulituamrisha tushuhudie kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah na kwamba wewe ni Mjumbe wa Allah, tumekutii. Umetuamrisha kusali sala tano kwa siku, tukakutii.Umetuamrisha kufunga (saumu) mwezi wa Ramadhani, tumekutii. Kisha umetuamrisha kwenda kuhiji Makka tukakutii. Lakini kukutosheka na yote haya yote ukamnyanyua binamu yako kwa mkono wako na ukamuweka juu yetu kama mtwala kwa kusema 'Ali ni mawla wa yule ambaye mimi ni mawla kwake: je, amri hii yatoka kwa Allah au yatoka kwako wewe?" Mtume (s.a.w) akasema: "Kwa jina la Allah ambaye ndiye Mola Pekee! Haya yanatoka kwa Allah, Mwenye nguvu na Mtukufu" Aliposikia jibu hili aligeuka na kuelekea aliko ngamia wake jike huku akisema: "Ewe Allah! Kama asemayo Muhammad ni sawa, basi vurumisha jiwe juu yetu kutoka angani na tupatie sisi adhabu kali na mateso." Kabla hajamfikia ngamia wake Allah alimvurumishia jiwe ambalo lilipiga juu ya kichwa chake na kupenyeza ndani ya mwili wake na kumuacha akiwa amekufa. Ni katika tukio hili kwamba Allah (swt) aliteremsha aya ifuatayo:
"Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea. Kwa makafiri ambayo hapana awezaye kuizuia. Kutoka kwa Allah, Mola wa mbingu za daraja." (Qur'an 70:1-3) :
Kama unakumbuka, niliwahi kusema kuwa nimeeleza maelezo ya ziada ili mpate kuyafahamu hayo nitakayoyaandika baadaye, hapa nitapenda kuwaeleza kuwa nimeleta ushahidi wa maneno ya Hazrat Ali mwenyewe ya kwua alikuwa akiamini kuwa Ukhalifa ni wake ingawa alikubaliana na wenzake baada ya fujo na kutoelewana juu ya suala hilo kutokea: Je, Wanachuoni wa Ki-Sunni wanaliona tukio hili kuwa ni sahihi?
Idadi ya mabingwa wa Ki-Sunni ambao wamesimulia tukio hili kwa urefu na kwa Mukhtasari, hushangaza akili! Tukio hili la kihistoria lilisimuliwa na Masahaba 110 wa Mtukufu Mtume (s.a.w) wafuasi wa Masahaba 84 na kisha likasimuliwa na mamia mengi ya wanachuoni wa ulimwengu wa Ki-Islamu, kuanzia karne ya kwanza mpaka kwenye karne ya kumi na nne AH (Karne ya 7-20 AD)
Takwimu hizi hujumuisha tu wapokezi waliomo katika simulizi zilizoandikwa na wanachuoni wa Ki-Sunni! Sehemu ndogo ya vyanzo hivi inatolewa hapa chini. Wengi wa wanachuoni hawa hawakunukuu tu tangazo hili la Mtume (s.a.w) bali vile vile wanaliita sahihi: " al-Hakim al-Naysaburi, al-Mustaddrak 'ala al-Sahihyn (Beirut), juzuu 3, uk. 109-110, uk. 133, uk. 148, uk. 533. Ameelezea kwa uwazi kwamba hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa vigezo vya Bukhari na Muslim. al-Dhahabi alithibitisha hukumu yake.
" al-Tirmidhi, Sunan, (Cairo), juzuu 5, uk. 633.
" Ibn Majah, Sunan, (Cairo, 1952), juzuu 1, uk. 45.
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Fath al-Bari bi Sharh Sahih al-Bukhari, (Beirut, 1988), juzuu 7, uk. 61.
" al-'Ayni, 'Umdat al-Qari Sharh Sahih al-Bukhari, juzuu 8, uk. 584.
" al-Suyuti, al-Durr al-Manthur, juzuu 2, uk. 259 na uk. 298.
" Fakhr al-Din al-Razi, Tafsir al-Kabir, (Beirut, 1981), juzuu 11, uk. 53.
" Ibn Kathir, Tafsir Qur'an al-Adhim, (Beirut) juzuu 2, uk. 14
" al-Wahidi, Asbab al-Nuzu, uk.l64.
" Ibn al-Athir, Usd al-Ghaba fi Ma'rifat al-Sahaba, (Cairo, 1932), juzuu 3, uk.92.
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Tahhdib, (Hyderabad, 1325), juzuu7, uk. 339.
" Ibn Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, (Cairo, 1932), juzuu7, uk. 340, juzuu 5, uk. 213.
" al-Tahawi, Mushkil al-Athar, (Hyderabad, 1915), juzuu 2 uk. 308-9.
" Nur al-Din al-Halabi al-Shafi'i, al-Sirah al-Halabiyya, juzuu3, uk. 337.
" al-Zrqani, Sharhe al-Mawahib al-Ladunniyya, juzuu 7, uk. 13
Hapa ni lazima kutaja kuwa Sheikh Juma Mazrui ataliona tukio hili kuwa halikusihi, hizi ndio mbinu zake kubwa za kutaka watu waendelee kudanganwa na kuona kuwa Shia wametowa habari hizi kutoka kwenye mifuko yao. Mbinu hizi hazitafanikiwa, watu siku hizi wanarejea Vitabu vinavyothibitisha habari hizo, Maulamaa wote hao wamethibitisha ukweli wa habari hizo isipokuwa huyo anayesema kuwa anajuwa kila hukmu ya Hadithi inayotajwa humu, basi tazameni Maulamaa hao nini wamesema na mtazame nini Sheikh Juma Mazrui amawaambieni, kisha mpime maneno yake na maneno ya Maulamaa hawa, na akili kichwani mwenu inshaallah.
Angalieni basi msidanganywe na waliopumbazwa na tungo za kimadhehebu na Khawarij wa Akheri zamaan kama Mtume alivyotuagiza kwa kutubashiria kutokea kwa watu kama hawa wenye kuukana ukweli hata kama wanajuwa kuwa wanayoyasema si sahihi. Nakuomba Sheikh Juma usiwe katika kundi hilo inshaallah na urudi katika haki na usisimame na uongo inshaallah. Hilo jina la mwenye kujibu makala hii Sheikh wewe ni mtu mzima na mwenye hekima kama unavyotaka watu wakujuwe, hivyo usitoke kwenye maudhuwi ya mjadala huu, haikuhusu wewe kujuwa kuwa mimi ni Wahida au si Wahida, jambo muhimu ni kuwa unajibiwa hayo unayoyaandika na waisilamu wanapata faida inshaallah. Na huyo Hassan Alliy, Sheikh Juam tafadhali muusie asiingilie makala hii wala asiwe mwenye kupenda kutaja majina ya watu, asiingilie mambo ya watu binafsi, tafadhali husika na makala inayoandikwa tu, huu ndio ustaarabu wa Japani, tabia hii si tabia ya mtu anayesema amesoma Japan, basi tafadhali atulie asome makala hizi kwa tabia za Kiislamu, hakuna haja ya kutowa ya ukumbi huu kupeleka ukumbi mwengine, ya ukumbi huu ni ya ukumbi huu hakuna haja ya kuandika mambo kama hayo.
Sheikh Juma Mazrui aya ya 55-56 ya Sura ya 5 (Al-maidah) imeshuka kwa shani ya Imam Ali (a.s), jambo hili najuwa unaweza kulikataa lakini huwezi kulifuta katika Vitabu vilivyoandikwa kabla ya wewe hujazaliwa. Jambo hili limetajwa katika Vitabu vya Shia na Sunni, miongoni mwa Vitabu vya Shia vilivyotaja jambo hili ni: Bihar al-Anwar, cha Allama Majlisi, Tafseer al-Mizan, cha Allama Tabatabai, Tafseer al-Kashaf, cha Allama Muhammad Jawad Mughniyah, al-Ghadir, cha Allama Abdul Husain Ahmad al-Amini na Ithbat al-Hudate, cha Allama Muhammad Ibn Hasan Amuli.
Amma Vitabu vya Sunni vilivyosema kuwa tukio la aya hiyo lilikuja kwa shani ya Imam Ali (a.s) ni vingi sana, miongoni mwa Vitabu hivyo ni:
(1) Tafsir al-Kabir, ya Imam Ahmad Ibn Muhammad al-Tha'labi, chini ya maelezo ya aya ya Sura ya 5 aya ya 55-56.
(2) Tafsir al-Kabir, ya Imam Ibn Jarir al-Tabari, jalada la 6, kurasa za 186, 288-289
(3) Tafsir Jamiu al ahkam al-Quran, ya Imam Muhammad Ibn Ahmad Qurtubi, jalada la 6, uk. wa 219
(4) Tafsir al-Khazin, jalada la 2, uk. wa 68
(5) Tafsir al-Durr al-Manthoor, ya Imam al-Suyuti, jalada la 2, uk. wa 293-294
(6) Tafsir al-Kashshaf, ya Imam al-Zamakhshari, Chapa ya Misri mwaka 1373, jalada la 1 uk. wa 505 na 649
(7) Asbab al-Nuzool, cha Imam Jalaluddin al-Suyuti, Chapa ya Misri ya mwaka 1382, jalada la 1 uk. wa 73, hadithi ya Ibnu Abbass (r).
(8) Asbab al-Nuzool, by al-Wahidi, on the authority of Ibn Abbas
(9)Al- Musnad ya Imam Ahmad Ibn Hanbal, jalada la 5, uk. wa 38
Mwisho:
Naona hapa nimkumbushe Sheikh Juma Mazrui kuwa mimi sisemi maneno matupu juu ya suala hili, nimeweza na ninaweza na nitaweza kukutolea Dalili nyingi sana zenye kuthibitishwa na ushahidi wa kutosha ambao ni sahihi juu ya suala hili la Ukhalfa na Ubora wa Ali (a.s) juu ya Cheo hicho: hapa tunayo Tafsiir ya Iamm Thaalabi ambaye jina leke hasa ni Abi Is'haq Ahmad Ibn Muhammad ibn Ibrahim Nisaboori al-Tha'labi. Imamu huyu amekufa mwaka 337 AH, mwanachuoni Mkubwa wa Historia ya Kiislamu Ibn Khallikan amesema juu yake kuwa "Imam Thaalabi alikuwa wa pekee katika kuifasiri Kur'ani na tafsiri yake ndio bora zaidi kuliko tafsiri nyengine" (Wafiyaat al a'ayaan).
Ima Thaalabi alipofika kwenye Sura 5:455-56 amenakili maelezo ya hadithi yenye simlizi za Sahaba Abu Dhar al Ghifari ( r ) kuwa amesema: "Masikio yangu yote mawili yawe hayasikii tena na macho yangu mawili yapofuwe kama ninasema uongo, nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani ziwe kwake akisema, "Ali ni Kiongozi wa wachamungu na ni Muwaji wa makafiri, atakayemsaidia atakuwa mshindi pamoja naye na atakayemwacha naye ataachwa". Siku moja niliswali na Mtume Muhammad (s), masikini akaja kwa ajili ya sadaka, lakini hapakuwa na ye yote aliyempa sadaka hiyo, wakati huo huo Ali alikuwa katika hali ya kurukuu na akamuashiria masikini huyo kuchukuwa pete yake kwenye kidole chake, hapo Mtukufu Mtume akamtukuza Allah na kusema "Allahu Akkbar"! Kaka yangu Mussa (a.s) alikuomba akisema ewe mola wangu, ukunjuwe moyo wangu kwa kuifanya kazi yangu nyepesi na niondolee utata uliopo kwenye ulimi wangu ili waweze kunifahamu, na mchaguwe kutoka miongoni mwa ahli zangu Harun ambaye ni ndugu yangu awe waziri wangu na nitie nguvu kwa ajili yake na mfanye ashiriki kwenye kazi yangu ili tuweze kukutukuza na kukukumbuka wewe kila mara.
Kwa hakika unatuona.' Na ewe Mola wangu ukamwambia Mussa kuwa, ewe Mussa, nimekutakabalia maombi yako, ewe Allah! Mimi ni mja wako na Mtume wako. Ungarishe moyo wangu pia na nifanyie kazi yangu iwe nyepesi na mfanye Ali ambaye ni miongoni mwa ahli zangu kuwa waziri wangu na mfanye yeye awe ni nguvu kwangu". Kisha Abu Dhar akaendelea kusema; Wallahi! Mtume hakumaliza dua yake isipokuwa Siddiq Jibriil alishuka na aya hii "INNA-MA WALIYYUKUM ALLAH .... (Sura ya 5 aya ya 55-56): "Hakika Allah ndiye Msimamizi wa mambo yenu, na Mtume wake pia na wale walioamini ambao wanasimamisha Swala na kutowa Sadaka hali wao wanarukuu. Na ye yote atakayemfanya Allah na Mtume wake na wale walioamini kuwa ndio wasimamizi wa mambo yake, hakika kundi la Allah ndilo litakalofaulu" Tafsir al-Kabir, ya Imam al-Tha'labi chini ya maelezo ya Sura 5:55-56. Sheikh Juma Mazrui, jee Imam Thaalabi hakujuwa ipi hadithi Sahihi na ipi hadithi Dhaifu, na kwamba wewe unajuwa zaidi zipi Hadithi sahihi na zile zisizokuwa Sahihi?
MWISHO