BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
KUTOA MSAADA
Kutowa kwa ajili ya M/Mungu nakutowa kwa ajili ya wengine wanaohitaji ni thawabu kubwa kwani watoao kwanjia hizo ndio watakao radhi za Mola wao na waliojuwa maana ya kuneemeshwa. Kuneemeshwa nako kuna sura nyingi kuna neema ya akili, kuna neema ya kiwiliwili, kuna neema ya mali, kuna neema ya watoto, kuna neema ya elimu na kadhalika. Sisi tulopewa utukufu tafauti na wanyama na viumbe wengine ndoo tupaswao kuzitumia neema hizo katika njia za kheri tupu. Tupo tulio na kasoro na ukosefu wa shukrani kwa kufanya ubaghili kwa neema hizo, au kudhalilisha kwa neema hizo.
Ndio sisi tutesao wanyama kama punda au ng’ombe, kuwatwisha kazi nzito kutwa nzima bila kuwapa malisho mazuri. Punda leo hii hutwishwa chasesi nzima ya lori anapumua hadi anaanguka! Punda leo hii anapakiwa mifuko ya saruji kama ana mwili wa chuma, punda leo hii anapakiwa nondo au boriti mchungaji na rafiki zake nao wakakaa juu ya gari hiyohiyo iliyo mabegani mwa mnyama, na kigongo anachopigiwa si cha kawaida tena hapachaguliwi pakupigwa, sikuhizi hupigwa hadi masikioni utashangaa ndoo anafanywa asikie amri au vipi! Lakini tunarudi wapi, kwani sisi wanaadamu tuna mtindo wakulaumiana sisi wenyewe tunapotendeana maovu pahala pakushukuriwa husema hee shukrani za punda mateke, lakini leo mabadiliko shukrani za Mwanaadamu vigongo na mzigo mzito, Punda wangekuwa na kauli nao wangesema, hiyo ni dhambi jamani.
Yule ni mnyama kanyimwa akili tuu bali nikiumbe kumtuma kwako ni kama kumuajiri lazima apumzishwe baada ya kukusaidia, Punda humtii mafuta wala kumnunulii kwatu mpya za miguu, kakupa zawadi Mola mhurumie mfanyishe kazi kiasi. Muoshe, mtibu anapoumwa, mpe malisho mazuri. Sasa punda hutumiwa mchana kutwa na mchungaji kishakusanya pesa saa moja usiku humfungulia aende kwenye majaa ya taka akajitegemee kujitafutia chakula asubuhi anatafutwa akabebeshwe mzigo tena hamjui kashiba au laa. Tazama mwanaadamu anavyofikia ukatili kiasi hicho na kuzikufuru neema alizopewa zimsaidie, yule usimuone ni mnyama kumtesa unako mtesa kunaandikwa kusanya pesa lakini jaza na kapu la dhambi pia.
Wapo walopewa neema ya mali, bali ubaghili umewatopea haifai kukusanya tuu fedha ukazifukia ndani hazikufai wala haziwafai wengine hata kusaidia nyumba za Ibada au madrasa au Mayatima! Ni dhambi neema unaitia uovu kwa upande wako, si tupo humu? Hatuvai vizuri, hatuli vizuri wala hatuwahadumii watoto wetu wenyewe, pesa kama imetiwa maji mfukoni, anachuma maelfu kwa siku ukimkabili tuu kama pana uchochoro wakukimbia atapitia huko au kama ana ofisi jawabu la mwambie hayupo ni maarufu. Ingawa hali yaleo ya watu matapeli inachangia kuwakimbiza watu hata wasio na nia hizo za ubaghili.
Tumia au tutumie ndugu yangu bali usifanyie Israfu kile ulichooneemeshwa, kwanini lakini leo hii hata wale watoao au wanaogawa sadaka ambao siyo mabaghili baadhi hupenda Watu wengine wajuwe kama wametowa! Anahitaji nini furaha yakusifiwa au radhi za Mola? Na kwanini wengine wasimbulie kwa walichokitowa kama wamelazimishwa? Hii yote ni mielekeo tunayoiyona ni vyema tujizinduwe katika kutozitia dosari neema tulizo neemeshwa.
Kwanini neema ya kizazi nayo tunaifuja? Maana tumo humu wenye kujisifia watoto wengi, hiyo ni neema. Lakini jee! unawaadilisha vipi? Unawatunza vipi? Unahakikisha wote wanajishughulisha na ibada walio wakubwa? Unawapeleka kupata elimu wote? Isiwe tunapanga hesabu za kuzaa kwa ushindani tuu, tena baadhi tunaposhambuliana na wenzetu hata lugha ya Utu huondoka si hasha alompandisha hasira akasemwa “Mimi na mbwa kama wewe ishirini” akimaanisha wanawe, haya hilo tusi gani tena! Tunalojirudishia sisi wenyewe hata kwa watoto wako mbwa, Sasa wewe baba yao uitweje? Maana ndiye uliye wazaa.
Kuna wanaona miili yao ina nguvu na kifuwa au misuli ya mikono yao huwa siyo neema ya kuwa na Afya njema, aaa hutumia vibaya umbile hilo mwendo ukabadilika, ncha za vidole vya miguu ndoo zionazoshika ardhi visigino juu, mikono nayo ikatanuliwa kiasi mtu mzima akapita baina ya mikono na kwapa asikuguse, tukasahau hata usia wa Bwana Luqman. Huwajui mitanuo ile wako mashindanoni au wanapita njia barabarani.
Dunia isituhadae tutumie neema vizuri na tuwe na viwango. Tutumie neema vizuri, kwani M/Mungu ametwambia
“ Mkinishukuru nitawazidishieni lakini mkinikufuru basi adhabu yangu nikali ”
Shukrani hata kwa neema hii ya SWAUM ALHAMDU LILLAH. M/Mungu Atughufirilie makosa na madhambi yetu Amiin.
Tunajaribu Kukumbushana Kwa kile tulichopokea kutoka kwa walotuzidi Elimu. Ndugu yangu katika Imani na wewe Shiriki kusambaza ukumbusho huu ili tufaidike sote.
Kijana Wako All Hajj Udii Katika Kufikishiana ukumbushana.
MWISHO