BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
UZAYUNI MELE YA WAYAHUDI
Watu wengi ulimwenguni huenda wakadhani kwamba maneno “Uzayuni” na “Uyahudi” au “Uyuda” yana maana moja lakini ukweli wa mambo ni kuwa si hivyo hata kidogo. Wasomi na wataalamu wa Kizayuhudi ambao wanaelewa vyema mafundisho ya kitabu kitakatifu cha Mayahudi yaani Taurati au Torati wanasema kuwa, dhana na fikra kwamba maneno hayo yana maana moja haionekani kuwa ni sawa. Pamoja na kuwa Wazayuni hujihesabu kuwa ni miongoni mwa Mayahudi, lakini Mayahudi wengi hujiweka mbali na fikra za Uzayuni.
Katika makala hii, tatajaribu kudurusu na kuchunguza maaoni na mitazamo ya wasomi wa Kiyahudi kutoka pembe tofauti za dunia kuhusiana na suala hili. Wakati huohuo, tutajaribu kuona ni jinsi gani utawala ghasibu wa Israel hutoa radiamali yake kuhusiana na maoni hayo na pia ni jinsi gani mitazamo hiyo iliyo dhidi ya Uzayuni huakisiwa katika vyombo vya habari vya kimataifa. Hata kama baadhi ya wasomi wa Kiyahudi wanaamini kwamba kuna uwezekano wa kiasisiwa dola la Kiyahudi, lakini wanasisitiza kwamba dola hilo lililoahidiwa si hili la hivi sasa la utawala ghasibu wa Israel lililoasisiwa kinyume cha sheria katika ardhi za Wapalestina. Shughuli za taasisi nyingi za Mayahudi zinaendeshwa kwa imani kwamba, taifa la Mayahudi halina haki yoyote ya kubuni dola hadi atakapokuja mwokozi wa dunia.
Fikra hizi zinatolewa katika hali ambayo Mayahudi wengi hivi sasa wanaishi kinyume cha sheria katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel. Hata hivyo, baadhi yao wamekataa kujiunga na jeshi la taifa kama alama ya kubainisha malalamiko yao kuhusiana na operesheni za kijeshi zinazotekelezwa mara kwa mara na Wazayuni dhidi ya Wapalestina. Afisa mmoja wa jeshi anasema kwamba, idadi ya Mayahudi wanaopinga vita vya kichokozi na kiukandamizaji vinavyotekelezwa na jeshi la utawala huo dhidi ya Wapalestina wasio na hatia imekuwa ikiongezeka kila siku kiasi kwamba, tokea kuanza kwa mapambano ya Intifadha hadi sasa, maafisa wapatao 1100 wamekiuka amri ya kujiunga na jeshi katika utekelezaji wa operesheni zake za kijeshi dhidi ya Wapalestina.
Dan Tamir, afisa mwingine wa jeshi la Israel alisema mapema mwezi huu kwamba, idadi ya askari jeshi wa Israel wanaokwepa kushiriki katika operesheni hizo kwa visingizio tofauti kama vile ugonjwa na matatizo ya kifamilia, imekuwa ikiongezeka kwa kasi kubwa. Afisa huyo ambaye kipindi fulani alifungwa jela kutoka na hatua yake ya kutoshiriki katika operesheni hizo alisema kwamba, hata kama yuko tayari kushirikiana na jeshi la utawala huo lakini hayuko tayari kuwakandamiza na kuwaua ovyo Wapalestina na raia wengine wasio na hatia. Tamir ameongeza kwamba, hatua ya Waisraeli ya kutoshiriki katikka operesheni za kijeshi za kuwakandamiza Wapalestina katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni limegeuka na kuwa tatizo kubwa katika siasa za ndani za utawala huo kiasi kwamba, watu wengi hufadhilisha kutozungumzia wazi mashinikizo hayo ya kijamii, kisiasa na kinafsi kutokana na woga wao wa kukandamizwa na watawala wa Kizayuni. Amesema viongozi wa utawala huo hujaribu sana kuficha upinzani huo unaoonyeshwa na maafisa wa kijeshi kuhusiana na jambo hilo.
Kituo kimoja cha televisheni cha Marekani pia hivi karibuni kilitangaza kuhusiana na suala hilo la kuongezeka idadi ya vijana wa Kiyahudi wanaopinga operesheni za kijeshi za Israel dhidi ya Wapalestina kwa hoja kuwa zinaenda kinyume na misimamo yao. Ripoti hiyo ya televisheni ya ABC iliyotangazwa chini ya anwani ‘maudhui moja ya kimsingi,’ iliashiria maneno ya kijana mmoja wa Kiyahudi aliyesema kuwa anafadhilisha kupelekwa mahakamani au hata kufungwa jela kuliko kuhudumia jeshi la Israel.
Kijana mwingine wa Israel kwa jina la Hagi Mater mwenye umri wa mika 18 anatazamiwa kufikishwa kortini mwezi ujao wa Agosti kwa sababu ya kukwepa kwake huduma ya lazima jeshini. Katika msimu wa kiangazi uliopita yeye na marafiki zake walimwandikia barua Waziri Mkuu Ariel Sharon wakimwambia kwamba hawakuwa tayari kujiunga na jeshi. Barua hiyo ambayo ilitiwa saini na wanafunzi wa sekondari 62 ilitumwa katika ofisi ya Sharon mwezi Agosti uliopita. Barua hiyo hivi sasa ina saini za watu 140 na inavyoonekana ni kuwa Mater ameazimia kuongeza saini katika barua hiyo kabla ya kuituma tena katika ofisi ya waziri mkuu. Katika moja ya mahojiano yake ya simu na televisheni hiyo ya ABC kutoka Israel, Mater alisema kuwa, alikuwa anafahamu vyema athari ya hatua yake hiyo ya kukataa amri ya kuhudunia jeshi. Huku akiashiria idadi inayozidi kuongezeka ya vijana wa Kiyahudi wanaokataa kutekeleza amri ya Sharon kuhusiana na suala hilo, Mater aliongeza kuwa hayuko peke yake katika njia hiyo hatari. Katika safari yake aliyofanya hivi karibuni nchini Marekani, Mater alifanya mahojiano mengi na vyombo vya habari na pia kushiriki katika vikao na makongamano tofauti ambapo alitetea kwa hoja madhubuti msimamo wake na marafiki wake wa kutohudumia jeshi linalowakandamiza kinyama Wapalestina. Mara nyingi amekuwa akituhumiwa na Mayahudi wenzake kuwa hana imani halisi ya Kiayahudi. Mara kadhaa amelazimika kuzungumza Kihibrania ikiwa ni katika juhudi zake za kuwakadhibisha wapinzani wake wanaomtuhumu kuwa si Myahudi halisi na kutilia shaka imani yake kuhusiana na dini hiyo.
Televisheni ya ABC inaongeza kuwa, katika umri wa miaka 54 wa utawala haramu wa Israel, makundi ya askari wa dhiba yamekuwa yakipinga amri zake za kushiriki katika operesheni za kijeshi hasa katika kipindi cha kukalia kimabavu jeshi la utawala huo ghasibu ardhi ya kusini mwa Lebanon na pia Intifadha ya kwanza. Mwezi huu wa Mei, Redio Tel Aviv ilitangaza kuwa makundi matatu ya Israel kwa majina ya Mertz, Peace Now and There is the Boundary yalimpelekea barua jaji mkuu wa Israel yakimtaka ailazimishe serikali ya Ariel Sharon iwaondoe askari wa Israel katika vitongoji haramu vya Mayahudi katika Ukanda wa Gaza na Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan. Yakiashiria kuwa tokea mwaka 1997 hadi sasa vitongoji 93 vimekwishajengwa katika maeneo hayo mawili ya Wapalestina kwa lengo la kupelekwa huko Mayahudi zaidi , makundi hayo yaliongeza kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa katika votongoji hivyo, thuluthi mbili ya Wahamiaji hao wa Kiyahudi wako tayari kuondoka katika vitongoji hivyo kwa fidia au wapewe nyumba katika maeneo mengine yanayodhibitiwa moja kwa moja na utawala wa Kizayuni. Kwa mujhibu wa matokeo ya uchunguzi huo wa maoni, ni asilimia sita tu ya wakazi wa vitongoji hivyo ndio waliokataa kuhama vitongoji hivyo kwa sababu yoyote, ile na kwamba hata walikuwa tayari kutumia silaha kwa lengo la kuzuia jambo hilo kutekelezwa.
Katika hatua kama hiyo, maprofesa na wahadhiri wa Kiyahudi wapatao 101 wanaofundisha na kufanya utafiti katika vyuo vikuuu mbalimbali ulimwenguni walielelzea kuchukizwa kwao na siasa za kupenda vita na uchokozi za serikali ya Marekani na za kinyama pamoja na kibaguzi za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Palestina. Katika barua yao hiyo iliyochapishwa na gazeti la The Guardiana la nchini Uingereza, wasomi hao waliitaka jamii ya kimataifa kuzingatia zaidi matukio yanayoendelea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Waliitaka kukemea kwa kila njia jinai zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni bila huruma dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Palestina ili kuzuia kukaririwa kwa jinai hizo. Miongoni mwa watu waliotia saini barua hiyo ni wasomi mashuhuri kama vile Profesa Abraham Ovaz na Profesa Linda bin Zavy wa Chuo Kikuu cha Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Katika nchi nyinginezo pia, Mayahudi wamekuwa wakilalamikia kwa njia mbalimbali kuendelea kuwepo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na kukosoa vikali vitendo vyake vya jinai na kwamba utawala huo unapasa kufikishwa mbele ya mahakamu ya kimataifa ili kujibu mashtaka yanayoukabili kuhusiana na jinai hizo.
Kuhusiana na suala hilo, Myahudi mmoja anayeishi nchini Ufaransa aliutaja utawala huo kuwa ni wa kimabavu, kijinai na kifashisti na kwamba unapaswa kufikishwa mbele ya mahakama ya kimatafa ya uadilifu mjini The Hague Uholanzi. Katika toleo lake la mtandao wa intaneti, gazeti la al-Quds al-Arabi liliandika kuwa Sefi Hindler, mwandishi wa Kizayuni wa gazeti la Ma’ariv mjini Paris aliandika kuhusiana na kadhia hiyo kama ifuatavyo; ‘ Siku chache zilizopita mtu mmoja aliyekuwa na lahaja iliyoonyesha wazi kuwa alikuwa ni Muisraeli alizungumza dhidi ya Israel katika mahojiano na redio moja ya Kiyahudi ni kana kwamba alikuwa ni msemaji wa Hizbullah.’Aliendelea kusema, ‘ukosoaji mkubwa hutoka kwa Mayahudi au Waisraili ambao wamejitenga na Uyahudi au Israel.
Pia Wapalestina wanaoishi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi wa utawala wa Kizayuni na pia nusu karne ya uchokozi na ukiukaji wa wazi wa haki zao.’ Gazeti la La Nacion linalochapishwa huko Buenos Aires nchini Argentina liliandika, ‘katika hali ambayo mapambano yasiyokoma ya Wapalestina yameweza kuukumba utawala haramu wa Israel kutoka pande zote, kundi moja la Mayahudi limefanya maandamano nje ya nyumba ya Ehud Barak likitaka kukomeshwa kwa jinai za utawala huo dhidi ya Wapalestina.’ Liliandika kuwa maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea huko Israel kwa kipindi cha wiki mbili mfululifo yamefichua uso mbovu wa ubaguzi wa rangi wa utawala huo wa Kizayuni.
Gabriela Lasky, mkurugenzi wa taasisi ya Kiyahudi ya Amani ambayo ndiyo taasisi kubwa zaidi isiyo ya kiserikali yaani NGO huko Israel, amesema kuwa tokea mwaka 1967 hadi leo utawala wa Kizayuni haujaheshimu hata haki za kimsingi kabisa za watu wa Wapalestina. Ameongeza kuwa katika kipindi hiki, ardhi za Wapalestina zimekuwa zikiporwa bila sababu yoyote na utawala huo na kisha kujengwa humo vitongoji vya Mayahudi. Isreal imewanyima Wapalestina hao haki yao ya kimsingi zaidi ya kukanyaga na kupita katika ardhi hizo na hata wakati mwingi kuwanyima haki ya kibinadamu kabisa kama vile ya kunywa maji. Katika sehemu nyingine ya mahojiano yake Lasky alikiri kwamba, kinyume na madai yanayotolewa na utawala wa kibaguzi wa Israel uhuru na demokrasia haviwezi kutekelezwa Israel katika hali ambayo Wapalestina milioni moja wanaishi katika ardhi hizo zinazoklaiwa kwa mabavu wakiwa chini ya utawala wa kijeshi na kunyimwa haki za kimsingi kabisa.
Katika sehemu nyingine za dunia, Mayahudi huteta kuhusiana na kuanzishwa kwa nchi haramu ya Kizayuni katika ardhi za Wapalestina na kutaka utawala huo uvunjwe mara moja. Kuhani Graham, mmoja wa wanachama wa kundi la Kiyahudi la Neturei Karta amesema kwamba si sahihi kubuniwa kwa dola la Kizayuni. Amesema kuwa kuhamahama na kuhangaika ni bila ya kuwa na makao maalumu ni sehemu moja ya imani ya Mayahudi. Kuhani Graham amessisitiza kwamba, kujengwa kwa vitongoji vya Mayahudi katika ardhi za Wapalestina kunaenda kinyume na imani ya dini ya Kiyahudi. Kundi hilo lililoshiriki katika kongamano moja lililoandaliwa mjini London Uingereza mwezi Novemba lilisema kwamba, lilitaka kuvunjwa kwa dola la Kizayuni katika ardhi za Wapalestina likisisitiza kwamba, ndilo chanzo cha ukosefu wa amani na uthabiti katika eneo zima la Mashariki ya Kati. Huku akilaani kitendo chochote kinachopelekea kupotea kwa maisha bila ya sababu ya kisheria, Kuhani Graham alisema kuwa kuanzishwa kwa utawala wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina ndicho chanzo halisi cha kuweko mgawanyiko na kutoelewana kati ya Mayahudi na Waislamu.
Pia aliwalaumu Wazayuni akisema kuwa ndio sababu kuu ya kuongezeka ufisadi miongoni mwa baadhi ya Mayahudi. Kuhani Graham aliongeza: ‘niliondoka Orshalem (Jerusalem) miaka arubaini iliyopita na kuomba hifadhi hapa mjini London na tokea wakati huo sijawahi kurudi tena huko. Ninawaomba Mayahudi wengine wote wasiwe na fikra ya kurudi huko tena.’ Alisema katika kubainisha nukta hiyo, ‘kabla ya kuasisiwa serikali ya Kizayuni, watu wa Palestina wakiwemo Wakristo, Waislamu na Mayahudi waliishi pamoja kwa amani na utulivu bila ya tatizo lolote lile. Lakini baada ya kuasisiwa utawala huo, chuki na ukandamizaji ulichukua sehemu ya upendo na huruma.’
Mwanachama mwingine wa kundi la Neturei Karta kwa jina la Kuhani Dovid Weiss anasema, ‘kwa bahati mbaya picha ambaya ambayo imedhihirishwa na serikali ya Israel na wafuasi wake kuhusiana na Mayahudi imepelekea watu wengi ulimwenguni kuwa na mtazamo mmbaya kuhusiana na dini ya Kiyahudi.’ Huku wakibainisha kuchukizwa kwao na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Israel dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa Palestina katika ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu, baadhi ya wasomi wa Kiyahudi wanasisitiza kwamba jinai hizo kamwe hazihusiani kwa njia yoyote ile na imani ya Kiayhudi.
Kwa mfano, Yasirwail Dawoudwais, mkurugenzi wa taasisi ya Kiyahudi ya Muungano wa Mayahudi dhidi ya Uzayuni yenye makao yake mjini New York na amabaye alishiriki kama kuhani katika kongamano la kupinga ubaguzi wa rangi lililoandaliwa mwaka uliopita na Umoja wa Mataifa huko mjini Durban Afrika Kusini aliwaambia washiriki wa kongamano hilo kwamba, alishiriki katika kongamano hilo kwa ajili ya kufichua jinai zinazotendwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina. Akifanya mahojiano pambizoni kwa kongamano hilo huku akiwa amesimama pembeni mwa Wapalestina kadhaa wanaopinga utawala wa Kizayuni, kuhani huyo aliwambia waandishi kwamba jinai zonazotekelezwa na Israel katika ardhi unazozikalia kwa mabavu huko Palestina hazina uhusiano wowote na dini ya Kiyahudi. Kwa kulaani jinai zinazotekelezwa na Ariel Sharon, Mayahudi waliowengi duniani hujitenga na serikali ya Kizayuni kutokana na jinai zake za kinyama dhidi ya wananchi wasio na hatia wala ulinzi wa Palestina.
Katika toleo lake la mwezi Machi mapema mwaka huu, gazeti la Daily Telegraph la nchini Uingereza liliandika kuwa wawakilishi wa Kiyahudi katika bunge la Uingereza walimkosoa vikali Waziri mkuu wa Israel kutokana na jinai za serikali yake dhidi ya watu wa Palestina. Hata kama maudhui ya kikao icho ilikuwa ni kuzungumzia mgogoro wa Mashariki ya Kati, ambayo bila shaka haikuzaa matunda, lakini wawakilishi wenye asili ya Kiayahudi walitumia fursa hiyo kumkemea vikali Ariel Sharon. Mwakilishi mmoja ambaye ana uhusiano na familia moja ya Kiyahudi yenye misimamo mikali ya kiorthodox alimtaja Sharon kuwa mhalifu wa kivita na mjinga. Alisisitiza kwamba Nyota ya Daudi ni ya Mayahudi wote lakini kwamba kwa bahati mbaya vitendo vya Sharon vimetumbukiza na kuichafua nyota hiyo katika damu. Wasomi kadhaa wa Magharibi pia wanatambua tofauti uliyopo kati ya Uzayuni na Uyahudi na kuamini kwamba, wachinjaji wa Wapalestina ni Wazayuni na wala sio Mayahudi. Mikhail Adams mwandishi wa Kimagharibi anaamini kwamba, tatizo na mgogoro wa Palestina haujawahi na kamwe hautatokana na ugomvi wa Waarabu, wawe ni Wakristo au Waislamu kwa upande mmoja na Mayahudi kwa upande wa pili. Hii inatokana na ukweli kwamba, Waarabu na Mayahudi wameishi kwa pamoja kwa amani na kwa muda wa karne nyingi bila ya tatizo lolote. Anaongeza kwamba, mgogoro wa hivi sasa wa Palestina unatokana na Wazayuni ambao wameazimia kuwachinja kinyama Wapalestina ambao ndio wamiliki halisi wa ardhi ya Palestina.
Wapalestina wamelazimishwa kuhama na kuishi uhamishoni katika nchi nyingine huku ardhi zao zikiporwa na Wazayuni kwa jili ya kuanzisha humo serikali yao haramu. Makuhani wa Marekani na Canada pia wamekuwa wakidhihirisha mara kwa mara hasira na kuchukizwa kwao na jinai zinazotekelezwa kila siku na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wasio na hatia wa Palestina. Mwaka uliopita maelfu ya wananfunzi na makuhani walifanya maandamano makubwa mbele ya ofisi za uwakilishi wa utawala haramu wa Israel huko katika katika makao makuu ya umoja wa Mataifa ili kuonyesha kuchukizwa kwao na siasa za kiukandamizaji na kijinai za utawala huo haramu.
Katika maandamani hayo yaliyoandaliwa na Kongamano Kuu la Makuhani wa Marekani na Canada, waandamani walibeba mabango na maberamu yaliyokuwa yameandikwa nara kama vile “sisi tu Mayahudi na sio Wazayuni’, ‘serikali ya Israel ni tofauti na Uyahudi’ na ‘taifa la Kiyahudi halina haki ya kuwa na nchi.’ Kongamano hilo lilitangaza kwamba sababu kuu ya kuandaliwa maandamano hayo ilikuwa ni kulaani siasa za hivi karibuni za Israel kukiwemo kuzidishwa kwa hatua zake za kuwakandamiza Mayahudi wenye mielekeo ya kidini, kufutiliwa mbali kibadi kilichokuwepo kwa kuwaruhusu wanafunzi wa dini ya Kiyahudi kutoshiriki katika huduma za lazima katika jeshi na hatua za kibaguzi za utawala huo wa Kizayuni zinazokiuka wazi sheria za kimataifa.
Kongamano hilo la makuhani liliasisiwa miaka khamsini iliyopita na Kuhani Mkuu Joel Teitelbaum ambapo shughuli zake hasa zinatekelezwa kwa imani kwamba Mayahudi hawaruhusiwi na dini yao kuunda serikali ya aina yoyote ile hadi atakapokuja mwokozi wa dunia ambaye ni Masih. Mwaka uliopita, mhadhiri mmoja mashuhuri kwa jila la Daniel Benton ambaye alikuwa akilalamikia kubomolewa kwa makaburi ya eneo la Haifa na wataalamu wa mambo ya kale, jambo ambalo bila shaka linakwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiayahudi, alipigwa vibaya na askari wa Kizayuni ambao hatimaye walimvunja mbavu kufuatia kitendo hicho cha aibu.
Mwezi Disemba uliopita pia, kundi moja la Mayahudi wa Marekani 600 waliojiita ‘Kilio cha Mayahudi dhidi ya Ukaliwaji Mabavu wa Ardhi za Wapalestina na Israel’, walitoa tangazo katika gazeti la New York Times wakitaka kukomeshwa kwa ukaliwaji mabavu wa Palestina, kupelekwa kwa askari wa kimatifa katika ardhi za Wapalestina kwa ajili ya kuwalinda wananchi hao wanaokandamizwa na kukatwa kwa misaada yote ya kifedha na kijeshi inayotolewa na serikali ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel. Wasomi 15 mashuhuri wa Kiayahudi pia wamekosoa msaada mkubwa na usiozingatia haki za kibinadamu wala maadili unaotolewa na serikali ya Marekani kwa utawala haramu wa Israel na kutaka kudhaminiwa kwa usalama wa watu wa Palestina kwa misingi ya sheria za kimataifa.
Vilevile idadi kadhaa ya Mayahudi imeelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na kutozingatiwa usalama wa Wapalestina na kutaka maisha yao yalindwe. Kwa mfano Noam Chomsky ni mwanafikra na mkosoaji wa Kimarekani ambaye anaamini kwamba, jamii ya nchi yake imechafuka na kwamba inahitajia mapinduzi ya kiutamadini.
Yeye akiwa na profesa Simona Sharoni, msomi wa Kiyahudi katika Chuo Kikuu cha Evergreen Olympia Marekani na wanafikra wengine 13 wa Kiyahudi waliandika barua ya pamoja mwezi Oktoba mwaka 2000 wakiitaka serikali ya Marekani itumie ushawishi wake juu ya utawala Israel ili kuulazimisha upunguze jinai zake dhidi ya Wapalestina. Katika barua hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha maneno yasemayo ‘idhibiti Isral’ na kuchapishwa na gazeti la Guardian, Mayahudi hao wa Marekani walielezea wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na usalama wa Wapalestina wanaoishi chini ya ugaidi wa jeshi la Israel linazozikalia ardhi zao kwa mabavu. Walisema waliandika barua hiyo kutokana na wasiwasi wao wa dharura kuhusiana na tabia ya Marekani ya kukwepa majukumu yake ya kutumia ushawishi wake katika kuilazimisha Israel iheshimu sheria na kulinda maisha ya Wapalestina.
Moshe Ari Freedman, Myahudi wa kiorthodox na anayesimamia kituo cha Mayahudi huko mjini Vienna Austria amesema, Wazayuni hutumia vinaya tukio la holocaust lililotokea katika kipindi cha utawala wa Adolph Hitler katika Vita vya Pili vya Dunia ili kujidhihirisha kuwa walidhulumiwa katika vita hivyo na kwa hivyo wanapasa kuhurumiwa.’ Kwa mujibu wa imani yake, Mayahudi walikuwa wakiishi kwa amani na Waislamu pamoja na Wakristo huko Palestina bila ya tatizo lolote na ulimwengu wa Kiarabu. Ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu pia ulikuwa na uhusiano mzuri na Mayahudi.
Huku akiashiria nukta hii muhimu kwamba kama walivyo Waislamu, Mayahudi waorthodox pia ni wahanga wa Wazayuni. Kuhani huyo alisisitiza kwamba, Mwenyezi Mungu aliwaamuru Mayahudi katika kitabu chao kitakatifu kwenda kimaaniwi huko Palestina na sio kudhihiri huko kimwili na kisha kupora mali za Wapalestina na kuwaua kwa umati. Huku akisisitiza kwamba kupora ardhi za watu wengine kunaenda kinyume kabisa na mafundisho ya dini ya Kiayahudi, aliongeza kuwa Wazayuni wanajaribu kuwashawishi Mayahudi kuwa hawana mustakbali mzuri katika bara Ulaya na kwa hivyo wanapasa kulihama bara hilo na kuhamia Israel.
Freedman alitilia mkazo nukta hii kwamba Maayahudi wa kiorthodox wanapinga vikali kuundwa kwa serikali ya Israel katika ardhi za Wapalestina akiongeza kuwa, mwezi Januari 2001 zaidi ya Mayahudi laki moja waliandamana huko mjini New York dhidi ya Israel. Mbali na hayo, kundi jingine la Mayahudi wa Marekani ambao wanahofia kwamba siasa hatari na za kijinai za Israel huenda zikahatarisha maslahi na maisha yao katika pembe mbalimbali za dunia, mwezi Mei walliamua kuanzisha taasisi ya wananchi ya kutetea maslahi yao. Katika toleo lake la mtandao wa intaneti, gazeti la Kiarabu la as-Sharq al-Ausat liliandika kwamba, ili kundi hilo kujaribu kuonyesha kwamba haliafikiani na vitendo vya utawala wa mabavu wa Israel dhidi ya Wapalestina, liliipa taasisi yake hiyo jina la ‘Si kwa Jina Letu.’
Muisraeli anayeishi Ufaransa: Israel ukiwa ni utawala vamizi, kijinai na wa kifashisti unapasa kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uadilifu mjini The hague. Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiayahudi ya Amani huko Israel: Tokea mwaka 1967 hadi leo, Israel haijawahi kuheshimu hata haki za kimsingi zaidi za watu wa Palestina. Kuhani Graham: Kujengwa kwa vitongoji vya Mayahudi katika ardhi za Wapalestina kunakwenda kinyume na thamani namafundisho ya dini ya Kiyahudi. Kuhani wa Kiingereza: Serikali inayojulikana hii leo kama Israel ni utawala usio na haki ya kisheria ya kuishi na kwa hivyo tunasubiri tu kutokomezwa kwa utawala huo wa Kizayuni.
MWISHO