YVONE NA HIJABU
  • Kichwa: YVONE NA HIJABU
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 20:50:36 13-9-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

Yvonne Ridley - Nilivyokuja Kuipenda Hijaab
Nilikuwa nikiwaona wanawake wanaojisitiri ni kama, viumbe waliodhulumiwa - mpaka nilivyokamatwa na Taliban. Katika mwezi wa tisa mwaka wa 2001, masiku 15 baada ya mashambulizi ya kigaidi katika nchi ya Marekani, Nilikamatwa ndani ya Afghanistan, nikafunikwa kutoka kichwa hadi vidole vya miguu kwa burqa ya rangi ya samawati, nikiwa nimedhamiria kuandika gazeti kuhusu maisha chini ya uonevu wa mfumo wa utawala. Badala yake, niligunduliwa, na kukamatwa na kufungwa siku kumi. Niliwatemea mate na kuwatukana walionikamata; waliniita mwanamke "mbaya" lakini waliniachilia baada ya kutoa ahadi kuwa kuisoma Quran na kujifunza Uislamu. [kwa kweli, sina uhakika nani aliyekuwa mwenye furaha zaidi wakati nilipoachiliwa huru; wao ama mimi.]

Niliporejea nyumbani London, niliweka nadhiri yangu ya kujifunza Uislam na nilistaajabu kwa yale niliyoyavumbua. Nilikuwa natarajia kuona kutoka katika surah za Quran kuwa vipi kumpiga mke wako na kuwadhulumu watoto wako; badala yake, nilikuta dondoo za uimarishaji wa ukombozi wa wanawake.

Miaka miwili na nusu baada ya kukamatwa, niliingia Uislamu, kulisababisha mshangao, uvunjaji moyo na pia tashtiti miongoni mwa jamaa na marafiki.

Sasa hivi, ni chuki na hofu ninayoiona hapa Uingereza kama katibu wa zamani wa mambo ya nje Jack Straw akieleza Niqaab kuwa mtandio unaofinika uso wote isipokuwa macho kuwa ni kizuizi kisichokubaliwa katika matangamano, hayo ni mawazo yake na yale ya waziri mkuu wake.

Nilivyopata ufahamu wa pande zote mbili kuhusu Hijaab, ninaweza kusema kuwa aghlabu wanaume wa magharibi, wanasiasa na waandishi wa habari ambao wanapigia kelele ukandamizaji wa wanawake katika ulimwengu wa Kiislamu, kwamba hawana fikra ya yale wanayozungumzia. Wanazidi kuzungumzia kuhusu mitandio, mabiharusi watoto, tohara kwa wanawake, hukumu za kifo, na ndoa za lazima, kwa hayo, wanaushutumu vibaya Uislam. Kutokana na kiburi chao walishinda kwa ujinga tu.

Tamaduni na desturi hizi hazimo katika Uislam. Usomaji wa makini wa Quran unaonesha kuwa karibu kila kitu walichokipigania mashabiki wa kimagharibi katika Miaka ya Sabini (1970), kilipatikana kwa Waislamu Wanawake tangu karne kumi na nne (1,400) zilizopita. Wanawake katika Uislam wanachukuliwa sawa na wanaume katika imani ya kidini, kielimu, na kithamani. Pia wanawake wamepewa hidaayaya kuzaa na kulea mtoto, na haya ni mazingatio yaliyo wazi.

Uislamu umewatunukia mambo mengi wanawake, kwanini wanaume wa kimagharibi wanashikilia vazi la wanawake wa Kiislam tu? Hata mawaziri wa serikali ya Uingereza, Gordon Brown na John Reid walitoa maoni tofauti kuhusu Niqaab - wakati huo huo wanawafurahikia wanaume wa Scottland wanapokuja kutoka kwao wakiwa na vazi la sketi.

Niliposilimu na kuanza kuvaa mtandio, mambo makubwa mno yalinitokea. Nilichokifanya ni kujifunika kichwa na nywele zangu. - lakini papo hapo nilijikuta nimegeuka kuwa ni raia wa daraja la pili. Nilijua nitajisikia ugeni katika upande wa Kiislamu, lakini sikutarajia kupata uadui wa dhahiri kutoka kwa watu nisiowajua. Wakati wa usiku nilipokuwa nasimamisha teksi zilikuwa zikinipita, hali ya kuwa alama za taa juu ya teksi hizo zinawaka kuashiria kuwa zinachukua abiria. Dereva wa teksi moja baada ya kumshusha abiria mweupe mbele yangu akanitazama nikiwa na hima ya kuifata teksi yake, aliondoka na kuniacha. Dereva mwengine alisema, "usiwache bomu hapo nyuma" na kisha akauliza, "Bin Laden amejificha wapi?"

Huu ni katika wajibu wa dini ya Kiislamu wanawake kuvaa kiheshima, lakini wanawake wengi wa Kiislamu ninaowajua wanapenda kuvaa Hijaab, ambayo inawacha uso wazi, japokuwa wachache wanapenda zaidi Niqaab. Ni katika kauli yangu binafsi: Nguo yangu inakuambia kwamba mimi ni Muislamu na hivyo nataraji kutendewa heshima zaidi, kama mtunza fedha za kijiji (mtaa) ambaye anaheshimiwa kwa dhati. Na hasa miongoni mwa walioingia Uislamu kama mimi, Utumishi wa wanaume ambao wanaokabili wanawake isivofaa, tabia ya kutupia jicho halitastahmilika.

Nilikuwa mwanamke wa kimagharibi kwa miaka mingi, lakini niligundua kuwa wanawake wa Kiislaamu ni wenye hadhi zaidi kuliko ulimwengu unavyofahamu. Tunachukizwa na maonyesho ya wanawake warembo, na hatukufurahia katika mwaka wa 2003 ambapo majaji wa mashindano ya Mrembo wa Dunia (Miss Earth) walipopongeza kuvalishwa bikini hadharani kwa mrembo wa Afghanistan, Vida Samadzai, wakidai kuwa ni mkombozi hodari wa uhuru wa wanawake. Na hata walimpa Samadzai zawadi mahsusi kwa "kutoa mfano wa ushindi wa uadilifu wa wanawake."

Baadhi ya wasichana wa Kiislamu wanadhani kuwa Hijaab na Niaqaab ni alama ya kisiasa, na pia wanadhani ni njia ya kujizuia na maasi ya kimagharibi, kama kulewa, uasharati na utumiaji wa dawa za kulevya. Ni upi uhuru zaidi: kujadiliwa kwa urefu wa sketi na uengezwaji wa matiti yako au kujadiliwa kwa sifa na ujuzi wako? Katika Uislaam, cheo cha juu hupatikana kwa kumcha Mwenyezi Mungu - sio uzuri, mali, mamlaka, cheo au jinsia.

Sikujua nipige kelele au nicheke wakati Wataliano walipojiunga kuchochea mjadala wiki iliyopita kwa kuarifu kuwa ni "kitu cha kawaida" kusivaliwe Niqaab, kwani kuvaa Niqaab kunasababisha mahusiano ya jamii kuwa "magumu sana." Ni upuuzi! Ikiwa hii ndio hali, kwa nini simu za mkono, simu za ndani, barua pepe, ujumbe wa maandishi, na faksi ni katika matumizi ya kila siku? Na hakuna yeyote anayezima redio eti kwa sababu ya kutomuona mtangazaji!.

Katika Uislam ninaheshimiwa. Uislamu unaniambia kwamba nina haki ya kujielimisha na hivyo ni jukumu langu kutafuta elimu, bila kujali kuwa nimeolewa au la.

Katika mfumo wa Kiislam hakuna pahali popote tulipoelezewa kuwa ni lazima wanawake tuoshe, tusafishe au tuwapikie wanaume. Kama vile wanaume wa Kiislam wasivyokubaliwa kupiga wake zao. Wapinzani wa Uislam japokuwa watadondoa hapa na pale aya za Quran au hadithi, lakini kawaida maelezo yao huwa ni nje ya makusudio. Ikiwa mwanamme atanyosha kidole dhidi ya mke wake, hakubaliwi kuacha alama kwenye mwili wake, kama Quran ilivyosema , "Musipige wake zenu."

Si Waislamu wanaume pekee wanaolazimika kutathmini pahali na utendaji wa wanawake (na wanawake pia wana haki). Kulingana na matokeo ya karibuni yaliyofanywa na mataifa kuchunguza vurugu za ndani ya nchi, imegunduliwa kwamba milioni 4 ya wanawake wa Kimarekani wanapitia hali mbaya ya kushambuliwa na wenza wao, ndani ya kipindi cha mwaka tu. Zaidi ya wanawake watatu wanauliwa na waume zao au marafiki wa kiume kila siku. Hivyo wanakaribia takriban 5,500 kuanzia 9/11.

Wanaume wenye shari hawatoki kwenye dini mahsusi au aina fulani ya utamaduni; kulingana na utafiti wa pande zote za dunia, kila penye wanawake watatu mmoja miongoni mwao hupigwa, hulazimishwa kujamiiana au hutendewa vibaya katika maisha yake. Hili ni tatizo la ulimwengu mzima ambapo limekiuka taratibu za dini, utajiri, cheo, kabila na utamaduni.

Ni kweli kwamba katika nchi za Magharibi, wanaume bado wanaitikadi ya kwamba wao ni bora kuliko wanawake, ijapokuwa wanawake wanalalamika. Ingawa wanapata malipo bora kwa usawa wa kazi - ikiwa ndani ya chumba cha posta au chumba cha baraza la halmashauri - wanawake bado wanatendewa kama ni chombo cha starehe, ambapo nguvu zao na utendaji wao unaoporomoka wazi wazi kutokana na kuonekana kwao.

Na wale ambao bado wanajaribu kudai kwamba Uislam unawakandamiza wanawake; rejea kauli ya 1992 kutoka kwa mheshimiwa Pat Robertson, pale alipotoa maoni yake juu ya kuwapa mamlaka wanawake: "Mwanawake ni kujitegemea." Yaani kutokuwa na familia ni kuendelea kisiasa, hii inawachochea wanawake kuacha waume zao, kuua watoto wao, kutenda uchawi, kuangamiza ubepari na wanawake kuwa wasagaji.

Sasa niambie nani ni mstaarabu na nani siye?
Yvonne Ridley ni mhariri wa siasa katika Televisheni ya Islam Channel iliyopo London na ni mtunzi mwandamizi wa kitabu "In the Hands of the Taliban: Her Extraordinary Story" (Robson Books)
Enyi mlio amini! Takeni msaada kwa subira na Sala. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri. (Quran 2:153).

MWISHO