KUANZIA NDOA HADI KUWA WAZAZI (SEHEMU YA NNE) B
MLANGO WA 3: KANUNI MUHIMU ZA KIFIQHI -1 KWA WAWILI WALIOOANA NO: 2
UTARATIBU WA KUFANYA TAYAMMAM
Tofauti na utambuzi wa kawaida, kufanya tayammam kwa kweli ni jambo rahisi na jepesi sana; ni rahisi zaidi kuliko kutawadha. Kunapaswa kutekelezwa kama ifuatavyo:
HATUA YA KWANZA:
Tia nia ya kufanya tayammam (sawa na wudhuu ama Ghusl).
HATUA YA PILI:
Kwa mikono yote kufunguliwa wazi na kunyooka kuelekea kile kitu ambacho tayammam inaruhusiwa juu yake (udongo, vumbi, mchanga na au jiwe); piga (au weak) mikono yote kwa pamoja, mmoja pembeni ya mwingine juu ya kitu hicho ambacho tayammam inafanyika juu yake.
HATUA YA TATU:
Nyanyua mikono yako na uiweke pamoja kama mtu anayeomba du’a, halafu weak vitanga vya viganja vyako juu ya paji la uso kuanzia maoteo ya nywele. Telezesha mikono yako chini juu ya nyusi na ncha ya pua, halafu vishushe viganja vyako kuelekea upande wa kulia wa paji la uso na halafu upande wa kushoto. Kisha rudisha mikono yako katikati ya paji la uso na uiteremshe yote kwa pamoja kuelekea puani, ukihakikisha na vidole pia vinaparaza juu ya nyusi na ncha ya pua. Paji lote la uso linapaswa kufunikwa hadi kwenye nyusi (inapendekezwa kushusha kupita zaidi ya nyusi).
HATUA YA NNE:
Nyoosha mkono wa kulia ukihakikisha kwamba kiganja chako kimeelekea chini, vidole na dole gumba vikiwa vimefungana pamoja na dole gumba halikuchimbiwa chini ya vidole. Halafu weka upande wa ndani wa mkono wa kushoto katika hali ya wima juu kidogo ya kifundo (yaani, kile kidole kidogo tu ndio kinapaswa kukandamizwa juu ya kifundo cha mkono wa kulia, kiganja cha mkono wako wa kushoto kikuangalie wewe).
Teremsha mkono wa kushoto (ukishusha kiganja chini), ukihakikisha maeneo yote ya ndani ya mkono wa kulia ziefunikwa. Rudia utaratibu huohuo juu ya mkono wa kushoto (bila ya kurudia kupiga mikono juu ya udongo tena).
MAMBO MUHIMU KUHUSIANA NA TAYAMMAM
a.) Kama utaacha hata sehemu ndogo tu ya paji lako la uso au sehemu ya nyuma ya mikono yako katika tayammam, kwa makusudi au kwa kusahau, au hata kwa kutokujua, tayammam yako itakuwa batili. Unapaswa kuwa mwangalifu lakini usizidi kuwa mahususia, kama itaweza kuchukuliwa vya kutosha kwamba paji la uso na nyuma ya mikono vimepakwa itakuwa imetosheleza.1
b.) Kama namna ya tahadhari, upakaji wa kichwa na mikono unapaswa kufanywa kuanzia juu kushuka hadi chini.2
c.) Ni Ihtiyat mustahab (tahadhari inayopendekezwa) kwamba hilo paji la uso, viganja vya mikono na sehemu za nyuma za viganja na mikono vinakuwa tohara.3
d.) Wakati wa kufanya tayammam, pete ni lazima zivuliwe na kizuizi chochote kwenye paji la uso au kwenye viganja au nyuma ya mikono navyo ni lazima viondolewe.4
KUVITOHARISHA VILE VITU AMBAVYO VIMECHAFULIWA NA MANII
NGUO AU SHUKA ZA KITANDA
Kama mashuka ama chochote cha kuvaa kama nguo au taulo vikinajisika kwa manii vinaweza kutoharishwa katika njia zifuatazo:
A. KUTUMIA MAJI YANAYOTIRIRIKA
1. Kama kitu hicho bado kina ubichi kutokana na manii, mtu anapaswa kuwa mwangalifu kwamba kisigusane na nguo nyinginezo au vitu vinginevyo kwa sababu hapo navyo vitakuwa vimenajisika.
2. Mtu anapaswa kuosha kile kilichonajisika mara moja chini ya maji ya bomba (kurr) katika namna ambayo kwamba:
a.) Maji yanafika kwenye kila sehemu ya lile eneo lililonajisika.
b.) Kuwe hakuna dalili za yale manii hasa yaliyoachwa kwenye nguo (yaani, sugua na kukamua nguo wakati wa kufua kwa namna ambayo hakuna mabaki ya manii yanayoachwa kwenye nguo wala rangi yake).
3. Kama kitu chenyewe ni kipande cha nguo, hakuna haja ya kukipopotoa au kukikamua baada ya kuwa kimetoharishwa (kwa mtindo huo hapo juu), ingawa hili huwa linafanyika kutokana tu na mazoea.
4. Wakati kitu hicho kikiwa kimeoshwa mara moja na kuwa safi kitohara (kwa mtindo huo hapo juu) hii inatosha; hailazimiki kukiosha mara mbili au tatu.
5. Kama kitu kilichonajisika kinatoswa kwenye maji ya bomba yanayotiririka (kurr) au maji yanayotembea, kwa namna ambayo maji yanaz- ifika sehemu zake zote zilizonajisika, kinakuwa kimetoharika. Na katika suala la zulia au vazi sio muhimu kulikamua, kulipopotoa au kuliminya.5
B.) KUTUMIA MASHINE ZA KUFULIA
Hukmu inayotumika kwenye mashine za kufulia ni ile ya maji ya kurr.6 Hivyo kitu ambacho kimekuwa najis kwa manii kinaweza kuwekwa moja kwa moja kwenye mashine ya kufulia, na madhali hakuna dalili ya manii iliyobakia baada ya mzunguko kukamilika, halafu kitu hicho kinachukuliwa kuwa kimetoharika, na hakihitaji kuoshwa tena, au kupopotolewa na kukamuliwa.
Hata hivyo, kama hatua ya tahadhari, linaweza kuwa ni wazo jema kukifanya kile kitu kilichonajisika kuwa kisafi kitohara kwanza (kwa njia ile ya pale juu) na kisha tukiweke kwenye mashine ya kufulia, kwa sababu kama mtu ataweka kitu hicho moja kwa moja ndani ya mashine ya kufulia, na kwa sababu yoyote iwayo manii hayo yakabakia kwenye nguo baada ya kufuliwa, haitakuwa safi kitohara, na endapo nguo hiyo itakutana na nguo nyinginezo zenye ubichi, nguo hizo pia zitakuwa zimenajisika
GODORO:
A. KUTUMIA MAJI YANAYOTIRIRIKA
Endapo godoro litanajisika kwa manii kwa sababu yoyote ile iwayo, inawezekana kulifanya tohara kwa maji safi yanayotiririka kutoka kwenye bomba au mpira wa maji:
Kama mtu anataka kutakasa godoro kwa kutumia maji safi yaliyounganishwa kwenye chanzo cha bomba – kurr – (kwa mfano kwa kutumia mpira wa maji au bomba) hakuna haja ya kuyafuta maji hayo kwa kutumia nguo hiyo au mashine ya kuvuta vumbi na kadhalika.
Mara tu yale maji ya kurr yanapolienea eneo lenye najis, litakuwa tohara (madhali ile najasat ayn – manii, itakuwa imeondolewa) [na maji hayo pia yatachukuliwa kuwa tohara].7
Ni muhimu kukumbuka yafuatayo wakati godoro linapokuwa limenajisika kwa manii: Manii hayo yanahamia tu kutoka kwenye godoro kwenda kwenye kitu kingine kupitia unyevunyevu unaobubujika (yaani, unapokuwepo ubichi mwingi katika kile kilichonajisika ambao unapenya kwenye kitu kingine na kukifanya kuwa najisi).
Hiyo najisi haihamishiki inapokuwa kavu, hivyo iwapo utaweka mwili au mkono wako juu ya godoro lenye najisi kavu, huo mkono au mwili wako hautakuwa umenajisika.
Kwa hiyo, inawezekana kulala juu ya godoro ambalo limenajisika bila ya nguo zako kunajisika, alimradi tu kwamba kile kipande ambacho kimenajisika kinabakia kuwa kikavu ili kwamba ile najisi haihamishiwi kwenye nguo hizo kutoka kwenye godoro hilo.
B. KUTUMIA MAJI MACHACHE KULIKO KURR (QALIIL)
Maji machache kuliko kurr yanatumika katika hali ambazo imma maji ya kurr hayapatikani au kwamba huwezi kuweka kitu kama godoro chini ya maji ya kurr (chini ya bomba). Utaratibu wa kukifanya kitu kiwe kisafi kitohara kwa maji machache ni kama ifuatavyo:
HATUA YA 1: KUIONDOA NAJISI
Manii hayo ni lazima yaondolewe kutoka kwenye godoro hilo. Mbinu inayowezekana ya kufanya hili ni kwanza kumwaga maji kutoka kwenye gilasi kuenea kwenye eneo lote lililoingia doa. Halafu chukua taulo na liweke juu ya ile sehemu iliyolowa na tumia nguvu kuminya juu yake kwa namna ambayo maji hayo yananyonywa na kwamba hakuna manii yanayobakia. Taulo litakalotumika litakuwa limenajisika na litahitaji kuoshwa kitohara.
HATUA YA 2: KUMWAGA MAJI KULIKO KIWANGO CHA KURR
Baada ya kuyaondoa yale manii, sehemu hiyo inatakiwa ifanywe kuwa tohara. Hili linafanywa
kwa kuchukua gilasi nyingine ya maji na kumwagia tena maji juu ya eneo lote tena (lile lililokuwa limenajisika).
Maji hayo ni lazima yakamuliwe na kuminywa yatoke kwenye godoro kabla halijawa tohara. Hili linaweza kufanyika kwa kuchukua taulo na kuliweka juu ya eneo lililoloweshwa kwa namna ambayo wakati nguvu inapoongezwa juu ya taulo hilo maji yote yananyonywa yatoke.
Godoro hilo sasa limekuwa tohara. Kama rai iliyothibitishwa na sio tahadhari ya wajibu, taulo hilo na maji yaliyotolewa yatahesabiwa kuwa ni najisi.
Kama kitu chochote kinakuwa najisi kwa uchafu mwingineo mbali na mkojo, kitakuwa tohara kwa kwanza kuondoa ule uchafu na kisha kumwa- gia maji machache chini ya kiwango cha kurr, mara moja, na kuyaruhusu yamwagike. Bali kama ni nguo na kadhalika, inapaswa kukamuliwa na kuminywa ili kiasi chochote cha maji kilichobakia kiweze kumwagika.8
ANGALIZO: Ni muhimu kabisa kutambua kwamba hata kama sehemu ya juu ya godoro inafanywa kuwa safi kitohara kwa maji machache (qaliil) kwa kufuatilia mfano huo hapo juu, sehemu ya ndani ya godoro itakuwa najisi kutokana na kununi ya maji machache. Hata kama godoro hilo litawekwa kwa pembe, bila shaka yatanywea kwenye godoro hilo.9
PENDEKEZO: Ili kuepukana na kazi hii ngumu ya ziada na ugomvi wote wa kulisafisha godoro, kuna manufaa makubwa sana kwamba mtu awe anaweka tandiko la plastiki kati ya shuka na godoro, ili kwamba kama kiasi chochote cha manii kitavuja kwenye shuka hakitavuja kupita kwenye plastiki hadi kwenye godoro.
MWILI WENYEWE
Kama sehemu ya mwili inanajisika kwa sababu ya manii, inaweza kufanywa safi kitohara kwa kumwagiwa maji kiwango chini ya kurr juu yake mara moja kwa namna ambayo kwamba hakuna mabaki ya manii yanayoachwa kwenye mwili. Hili linaweza kufanyika kwa kusimama chini ya bomba la manyunyu.
Hata hivyo, kanuni hii ni tofauti kama najisi yenyewe ni mkojo, ambao kuuosha mara moja hakutoshi, mwili lazima uoshwe mara mbili. Sio lazima kuingia na kutoka kwenye maji ili kupata majosho mawili. Endapo sehemu iliyopata najisi inapanguswa kwa mkono kuruhusu maji kufika hapo tena, hiyo itatosha.10
• 1. Islamic Laws, Kanuni ya 710
• 2. Wasa'ilush-Shi'a; Juz. 20, Uk. 109, namba 25163
• 3. Islamic Laws, Kanuni ya 714
• 4. Islamic Laws, Kanuni ya 715
• 5. Islamic Laws, Kanuni ya 160
• 6. Imethibitishwa na ofisi ya Ayatullah Sistani, Qum.
• 7. Kanuni ya Desturi kwa Waislam huko Magharibi, Ayatullah Sistani.
• 8. Islamic Laws, Kanuni ya 163
• 9. Islamic Laws, Kanuni ya 163
• 10. Islamic Laws, Kanuni ya 172
ITAENDELEA MAKALA IJAYO