KUWEKA MKONO WA KULIA JUU YA MKONO WA KUSHOTO NI BID'A ALIYOIANZISHA OMAR BIN KHATABI KWA KUWAIGA MAJUSI (WAABUDU MOTO)
۱. إنّ وضع إحدى اليدين على الأخرى حالة صلاة سنّة عند أكثر الجمهور إلّا مالك ؛ فقد قال في المغني لابن قدامة / ٥۱٤ : « ظاهر مذهبه الذي عليه أصحابه : إرسال اليدين وروي ذلك عن ابن الزبير والحسن ».
Hakika kuweka mmoja ya mikono juu ya mwingine wakati wa Swala imekuwa ni kama Sunnah kwa Ahlisuna isipokuwa Ma Maalik.
Ibn Quddamah ameyasema hayo katika kitabu kiitwacho Al Mughniy UK 514, na madheheb ya wafuasi wake yanaitwa Adhwahiri, Dhwahiri wenyewe hunyoosha mikono kufuata mapaja wakati wa ku Swali na wamepokea hayo kutoka kwa Ibn Zubayr na Hassani.
۲. قد جاءت روايات أهل البيت عليهم السلام لترد على التكتيف ، وأنّه من فعل المجوس ، ففي حديث الإمام الباقر عليه السلام : « ولا تكفر فإنّما يفعل ذلك المجوس » ، والتكفير هو التكتيف في الصلاة. [ راجع وسائل الشيعة باب ۱٥ من قواطع الصلاة حديث ۱۲ وكذلك ح ۱ وح ۳ و ح ٤ وح ٥ وح ۷ ]
Imekuja riwaya kutoka kwa Ahlubaiti Rasul as ya kukataa na kukataza kufunga mikono kifuani wakati wa Swala, kwa sababu hicho ni kitendo cha Majusi.
Na katika hadithi ya Imamu Muhammad Baqir as anasema,: Msifunge mikono kifuani hakika wanayafanya hayo Majusi.
۳. : « ويحكى أنّه لما جيء باُسارى الفرس إلى الخليفة الثاني ، كفّروا أمامه فسأل عن ذلك ، فأجابوه بأنّا نستعمله خضوعاً وتواضعاً لملوكنا ، فاستحسن فعل ذلك مع الله سبحانه في الصلاة وغفل عن قبح التشبيه بالمجوس في الشرع ». [ جواهر الكلام : ۱۱ / ۱۹ ]
Na inasimuliwa kuwa walipoletwa mateka wa kivita kutoka Furusi (Iran) mpaka kwa Umar bin Khatabi, walifunga mikono vifuani mwao mbele ya Umar bin Khatabi, Umar akawauliza mnafanya nini hivyo? Wakamjibu kuwa tunafanya hivyo kuwaonyesha heshima na unyenyekevu wafalme wetu. Basi Umar akasema hiki ni kitendo kizuri kufanyiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Swala, huku akisahau kuwa katika Sheriah ya Kiislamu ni vibaya kujifananisha na Majusi.
٤. ولو كان التكتّف ثابتاً عن النبي صلّى الله عليه وآله لشاع واشتهر ؛ اذ الصلاة تؤدّى في كلّ يوم خمس مرّات ـ كفرض ـ ، ومعارضة مالك وأصحابه وأهل البيت عليهم السلام يوجب الإطمئنان ببطلان التكتّف ـ التكفير في الصلاة ـ. وعلى هذا فمن أين تولّدت هذه الظاهرة ؟
Lau kama kufunga mikono kifuani ingethubutu kutoka kwa Mtukufu Mtume saww suala hili lingeenea na kujulikana kwa wote; kwani swala kwa siku ni tano za Wajibu na vilevile kuna Swala za matukio, Mtume saww alikiswalisha lakini hilo halijawahi kuonekana mbele ya Ahlubaiti wake na Maswahaba.
Maalik na wafuasi wake na Ahlubaiti Rasul as wanasema kwamba kufunga mikono kifuani katika Swala, swala inakuwa ni batili.
Sasa hawa Dhahiri wamepata wapi hili?
أقول : اصطنعت لهذه الظاهرة ـ التي أمر بها الخليفة الثاني غفلة منه عن قبح التشبيه بالمجوس ـ بعض الأحاديث من قبيل إنّ النبي كان يؤمّ الناس ويأخذ شماله بيمينه على ما رواه الترمذي ، ولكن هذا مرفوض لما قدمناه :
Tunasema: Hawa Dhahira walifanya hili kuwa ni Sunnah kwa ile amri ya Umar kuwaamrisha watu kufunga mikono vifuani, kwa kusahau ubaya wa kujifananisha na Majusi. Na walitengeneza baadhi ya hadithi (wakasingizia) kutoka kwa Mtukufu Mtume saww kuwa Mtume saww alikuwa akiwaswalisha watu akiwa ameshika kwa mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto,
Hadithi hii ipo katika Sunanu Tirmidhiy. Lakini hadithi hiyo imekataliwa kutokana na tuliyoyasema hapo juu:
أ ـ من مخالفة أهل البيت عليهم السلام.
1.Yaani ni riwaya inayoenda kinyume na Ahlubaiti Rasul as.
ب ـ مخالفة مالك وأصحابه.
2. Riwaya Inaenda kinyume na Maalik na wafuasi wake
ج ـ لما حكي في التاريخ من أسارى الفرس.
3. Na kutokana na simulizi ya kihistoria inayosema kuhusu mateka wa kifursi (ki Iran) inayoonyesha ndiyo chanzo chake.
REJEA:
- Wasa'ilu Shi'ah mlango wa 15 katika vyenye kuharibu (kubatilisha) swala, hadithi namba 12, hadithi namba 1,3,4,5na 7.
- Jawahirul Kalami Jz 11 UK 19.