NENO SHIA
  • Kichwa: NENO SHIA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 3:31:6 7-10-1403

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI.
NENO SHIA

Lakini vipi Mtume (s.a.w.w.) atumie neno la kuleta mgawanyiko?
Je Nabii Ibrahim alikuwa ni wa ki-madhehebu? Vipi kuhusu Nabii Nuh na Nabii Musa? Ikiwa neno Shi'ah ni la kuleta mgawanyiko au la ki-madhehebu, basi Mwenyezi Mungu asingelilitumia kwa Mitume wake wenye daraja ya juu, na wala Mtume Muhammad (s.a.w.w.) asingeliwatukuza.

Ni lazima isisitizwe kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) hakutaka kuwagawaya Waislamu kwa makundi. Bali aliwaamuru watu wote wamfuate Imam Ali (a.s.) akiwa ni mwakilishi wake wakati alipokuwa hai, na akiwa ni mrithi na khalifa wake baada yake. Lakini kwa bahati mbaya waliokubali kufuata matakwa yake walikuwa ni wachache, na walijulikana kama "Shi'ah wa Ali". Walipatwa na kila aina ya ubaguzi na mateso, na waliteseka kuanzia ile siku aliyofariki rehma ya umma, Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Lau Waislamu wote wangelitii na kufuata vile Mtume (s.a.w.w.) alivyotaka, kusingelikuwa na makundi au madhehebu ndani ya Uislamu.

Mtume (s.a.w.w.) amesema:
"Mara tu nitakapofariki, mizozo na chuki itajitokeza miongoni mwenu; wakati hali hiyo itakapodhihiri, basi mtafuteni Ali, kwa sababu yeye anaweza kupambanua kati ya ukweli na uongo."

" Ali Muttaqi al-Hindi, Kanz al-'Ummal, (Multan) Juz. 2 Uk. 612, Na. 32964
Kuhusu ile Aya tuliyoitaja hapo awali, baadhi ya Wanavyuoni wa Sunni wameipokea kutoka kwa Ja'far al-Sadiq (a.s.), Imam wa sita wa Shi'ah, Imam anayetokana na kizazi cha Mtume (Ahl al-Bayt), kwamba:
"Sisi ni kamba ya Mwenyezi Mungu ile aliyoitaja akasema: Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote, wala msiachane."

" al-Tha'labi, Tafsir al-Kabir, chini ya maelezo ya Aya 3:103
" Ibn Hajar al-Haythami, al-Sawa'iq al-Muhriqah, (Cairo) Sura. 11, She. 1, Uk. 233
Kwa hivyo, ikiwa Allah anakataa migawanyiko ya ki-madhehebu, basi vilevile anakataa wale wanaojitenga na kamba Yake, na si wale wanaoshikamana nayo barabara!

Mwisho:
Tumekwishaonyesha kwamba neno Shi'ah limekuwa likitumika katika Qur'an kwa wafuasi wa watumishi wakuu wa Allah, na katika Hadith za Mtume, kwa wafuasi wa Imam Ali (a.s.). Yeyote atakayefuata mwongozo huu wa Mwenyezi Mungu atakuwa amesalimika na mizozo katika dini, na atakuwa ameshikamana na kamba madhubuti ya Mwenyezi Mungu, na atapata bishara njema za Peponi.
Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote, wala msiachane
(Qur'an 3:103)

Kwa nini Shi'ah?
Neno "Shi'ah" ni sifa ya jina litumikalo kwa Waislamu wanaowafuata Maimam wanaotokana na kizazi cha Mtume (Ahl al-Bayt). Hawakulitumia jina hilo kwa sababu za ki-madhehebu au kusababisha migawanyiko miongoni mwa Waislamu. Walilitumia kwa sababu Qur'an inalitumia, Mtume Muhammad alilitumia, na Waislamu wa mwanzo walilitumia - hata kabla ya maneno kama Sunni au Salafi kuwapo duniani.

Shi'ah ndani ya Qur'an
Neno "Shi'ah" linamaanisha "wafuasi; wanachama wa chama". Allah ametaja katika Qur'an kwamba baadhi ya watumishi Wake wema walikuwa ni wafuasi (Shi'ah) wa wafuasi Wake wengine wema. Na hakika Ibrahim alikuwa katika Shi'ah wake,(akaenda mwendo wake) (Qur'an 37:83)

(Nabi Musa) akaingia mjini (siku moja) wakati wenyeji wake walikua katika ghafla (yaani katikati ya mchana), na akakuta humo watu wawili wakipigana: Mmoja ni katika Shi'ah wake na mwengine katika adui zake. Basi yule aliyekuwa Shi'ah wake alimwomba msaada juu ya yule adui yake. (Qur'an 28:15) Hivyo basi Shi'ah ni neno rasmi lililotumika na Allah katika Qur'an yake kwa ajili ya Mitume wake wenye daraja ya juu, na kwa wafuasi wao.

Ikiwa mtu ni Shi'ah (mfuasi) wa watumishi wema sana, basi hapana makosa kuwa Shi'ah. Au kwa maneno mengine, ikiwa mtu atakuwa ni Shi'ah wa dhalimu au wa mkosefu, bila shaka atayapata yatakayompata kiongozi wake. Qur'an yaashiria kuwa siku ya Kiyama watu watakuja kwa makundi, na kila kundi litakuwa na kiongozi wake (Imam) mbele yake. Allah amesema: (Wakumbushe) siku tutakapowaita kila watu pamoja na waongozi wao. (Qur'an 17:71) Mnamo siku ya Kiyama, majaaliwa ya "wafuasi" wa kila kundi yatategemea na majaaliwa ya Imam wao (kwa sharti kwamba wao, kweli, walimfuata Imam huyo). Allah ametaja ndani ya Qur'an kwamba kuna aina mbili za Maimam: Na tuliwafanya maimam (waongozi) waitao katika moto, na siku ya Kiyama hawatanusuriwa. Na tukawafuatishia laana katika dunia hii, na siku ya Kiyama watakuwa miongoni mwa wenye hali mbaya (kabisa). (Qur'an 28:41-42)

Qur'an pia yakumbusha kwamba kuna Maimam walioteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwa ni viongozi wa wanaadamu: Na tukawafanya miongoni mwao Maimamu wanaoongoa kwa amri yetu, waliposubiri, na walikuwa wakiziyakinisha Aya zetu. (Qur'an 32:24) Kwa yakini, wafuasi halisi (Shi'ah) wa Maimam hawa, watakuwa ndio watu waliofaulu hasa, katika siku ya Kiyama.

Shi'ah katika Hadith
Katika historia ya Kiislamu, neno "Shi'ah" limekuwa likitumika hasa kwa wafuasi wa Imam 'Ali (a.s.). Msemo huu si kitu kilichobuniwa baada ya Mtume! Mtu wa kwanza aliyetumia istilahi hii ni yeye mwenyewe Mjumbe wa Allah. Wakati Aya ya Qur'an ifuatayo iliposhuka: Hakika wale walioamini na kutenda mema, basi hao ndio wema wa viumbe. (Qur'an 98:7) Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ali: "Hii ni kwa ajili yako na wafuasi (Shi'ah) wako." Kisha akasema: "Naapa kwa yule anayeyatawala maisha yangu kwamba mtu huyu (Ali) na wafuasi wake wataokolewa na adhabu mnamo siku ya ufufuo."
" Jalal al-Din al-Suyuti, Tafsir al-Durr al-Manthur, (Cairo) Juz. 6, Uk. 379
" Ibn Jarir al-Tabari, Tafsir Jami' al-Bayan, (Cairo) Juz. 33, Uk. 146
" Ibn Asakir, Tarikh Dimashq, Juz. 42, Uk. 333, Uk. 371
" Ibn Hajar al-Haythami, al-Sawa'iq al-Muhriqah, (Cairo) Sura. 11, Sehemu 1, Uk. 246-247
Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Ewe Ali! (Mnamo siku ya Kiyama) wewe na wafuasi wako mtakwenda kwa Mwenyezi Mungu mkiwa mmeridhiwa na mmeridhika, na maadui zenu watakwenda kwake wakiwa na ghadhabu na huku shingo zimewasimama!

" Ibn al-'Athir, al-Nihaya fi Gharib al-Hadith, (Beirut, 1399), Juz. 4 Uk. 106
" Al-Tabarani, Mu'jam al-Kabir, Juz. 1 Uk. 319
" Al-Haythami, Majma' al-Zawa'id, Juz. 9, Na. 14168

Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Furaha kuu! O Ali! Hakika wewe na wafuasi wako mtakuwa Peponi."

" Ahmad Ibn Hanbal, Fadha'il al-Sahaba, (Beirut) Juz. 2, Uk. 655
" Abu Nu'aym al-Isbahani, Hilyatul Awliya, Juz. 4, Uk. 329
" Al-Khatib al-Baghdadi, Tarikh Baghdad, (Beirut) Juz. 12, Uk. 289
" Al-Tabarani, Mu'jam al-Kabir, Juz. 1, Uk. 319
" Al-Haythami, Majma' al-Zawa'id, Juz. 10, Uk. 21-22
" Ibn 'Asakir, Tarikh Dimashq, Juz. 42, Uk. 331-332
" Ibn Hajar al-Haythami, al-Sawa'iq al-Muhriqah, (Cairo) Sura. 11, Sehemu 1, Uk. 247

MWISHO