MAJIBU KWA BWANA JUMA MAZRUI
Allah amesema: "Ewe Mtume, fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi hujafikisha ujumbe wake, na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu". (Qur'an: 5, 67) Shia wanaamini kwamba agizo lililotajwa na Aya hiyo ya Qur'an lilitekelezwa na Mtume (s.a.w.w.) alipomteua Imam 'Ali bin Abi Talib (a.s.) kuwa wasii wake kwenye siku ya Ghadir Khumm.
Aliposikia majibu haya, yule mtu aligeuka na kumuelekea ngamia wake huku akisema: "Ee Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ayasemayo Muhammad ni sahihi, basi tuteremshie jiwe kutoka mbinguni na utuadhibu vikali." Basi mtu huyo kabla hajamfikia ngamia wake, Mwenyezi Mungu alimteremshia jiwe lililomwingia mwilini mwake kupitia kichwani kwake na kumwacha akiwa amekufa. Ilikuwa katika tukio hili ndipo Mwenyezi Mungu Mtukufu alipoteremsha Aya ifuatayo: Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayotokea. Juu ya Makafiri - ambayo hapana awezaye kuzuia. Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye utukufu mkubwa. (Qur'an 70:1-3) Je Wanavyuoni wa Sunni hulichukulia tukio hili kuwa ni la kweli?
Idadi kubwa ya Wanavyuoni wa Sunni waliosimulia tukio hili, kwa urefu na kwa muhtasari, ni ya kushangaza! Tukio hili la kihistoria limesimuliwa na Maswahaba wa Mtume 110, pia Tabiina (waliokuwako baada ya Maswahaba) wapatao 84, na Wanavyuoni wengi wa ulimwengu wa Kiislamu, kutoka karne ya 1 AH hadi karne ya 14 AH (Karne ya saba hadi ya ishirini CE). Takwimu hizi ni zile tu za wapokezi waliotajwa katika Hadith zilizopokewa na Wanavyuoni wa Sunni!
Idadi chache sana mkusanyiko wa misingi ya marejeo imetajwa hapo chini. Wengi wa Wanavyuoni hawa hawakunukuu hotuba ya Mtume tu bali pia wameiita kuwa ni sahihi, nayo ni: " alHakim alNaysaburi, alMustadrak `ala al-Sahihayn (Beirut), Juz. 3, Uk. 109-110, Uk. 133, Uk. 148, Uk. 533. yeye amesisitiza kuwa Hadith hii ni sahih kulingana na vipimo vya alBukhari na Muslim; alDhahabi pia amethibitisha hili.
" alTirmidhi, Sunan (Cairo), Juz.. 5, Uk. 633
" Ibn Majah, Sunan, (Cairo, 1952), Juz. 1, Uk. 45
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Fath al-Bari bi Sharh Sahih al-Bukhari, (Beirut, 1988), Juz. 7, Uk. 61
" Al-'Ayni, 'Umdat al-Qari Sharh Sahih al-Bukhari, Juz. 8, Uk. 584
" Ibn al'Athir, Jami` al'Usul, i, 277, Na. 65;
" Al-Suyuti, al-Durr al-Manthur, Juz. 2, Uk. 259 na Uk. 298
" Fakhr al-Din al-Razi, Tafsir al-Kabir, (Beirut, 1981), Juz. 11, Uk. 53
" Ibn Kathir, Tafsir Qur'an al-'Adhim, (Beirut), Juz. 2, Uk. 14
" Al-Wahidi, Asbab an-Nuzul, Uk. 164
" Ibn al-'Athir, Usd al-Ghaba fi Ma'rifat al-Sahaba, (Cairo), Juz.3, Uk. 92
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Tahdhib al-Tahdhib, (Hyderabad, 1325), Juz. 7, Uk. 339
" Ibn Kathir, al-Bidayah wan Nihayah, (Cairo, 1932), Juz. 7, Uk. 340, Juz. 5, Uk. 213
" Al-Tahawi, Mushkil al-Athar, (Hyderabad, 1915), Juz. 2, Uk. 308-9
" Nur al-Din al-Halabi al-Shafi'i, al-Sirah al-Halabiyya, Juz. 3, Uk. 337
Al-Zurqani, Sharh al-Mawahib al-Ladunniyya, Juz. 7, Uk. 13
Neno mawla kwenye hadithi hii Sheikh Juma halina maana ya rafiki! Japokuwa idadi kubwa ya Wanavyuoni wa Sunni wa zama zote na maoni yote wamethibitisha tukio hilo na maneno ya kihistoria ya Mtume (s.a.w.w.), lakini imekuwa ni vigumu kwao kukubaliana na yaliyotokea baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.). Lakini nakala hii fupi haiwezi kutaja kwa ufafanuzi matukio hayo. La muhimu ni kwamba Wanavyuoni wengi wa Sunni wamedai kwamba Mtume (s.a.w.w.) alimtangaza 'Ali (a.s.) kuwa ni rafiki na msaidizi wa Waislamu! Kuna mitazamo mingi ya tukio hili inaoonyesha jinsi lilivyokuwa na umuhimu. Miongoni mwayo ni kufunuliwa kwa Aya nyingi za Qur'an, mkusanyiko mkubwa wa watu, hatua za mwisho za maisha ya Mtume (s.a.w.w.), watu kuthibitisha kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na mamlaka makuu, kupongezwa baada ya tukio hilo na 'Umar, na sababu sababu nyingine nyingi ambazo haitoshi kuzitaja katika nakala hii fupi; yote yanaonnyesha juu ya kutawazwa kwa wasii wa Mtume (s.a.w.w.). Ni dhahiri kwamba neno mawla lilitumika kwa maana ya mamlaka kamili baada ya Mtume na si kwa mamlaka ya muda tu.
Neno la Mwisho Ikiwa bado kuna shaka juu ya umuhimu wa kihistoria wa hotuba hii, na bidii ya baadhi ya watu ya kuificha, hebu basi neno la mwisho liwe ni hili: Wakati Imam 'Ali (a.s.), alipokuwa khalifa, na hapo ni miongo kadhaa baada ya tukio la Ghadir, siku moja alimwambia Anas bin Malik, swahaba wa Mtume (s.a.w.w.): "Kwa nini hutoi ushahidi kwa uliyoyasikia kwa Mtume siku ya Ghadir?" Akajibu, "Ee Amir ul-Muminin! Nimezeeka na siwezi kukumbuka." Hapo 'Ali (a.s.) akasema: "Mungu atakupa doa jeupe (la ukoma) lisilofichika na kilemba chako! Ikiwa kwa makusudi waficha ukweli!" Na kabla Anas hajainuka pale alipokuwa amekaa, alipatwa na doa kubwa jeupe usoni kwake.
" Ibn Qutaybah al-Dinawari, Kitab al-Ma'arif, (Cairo, 1353 AH), Uk. 251
" Ahmad bin Hanbal, al-Musnad, Juz. 1, Uk. 119
" Abu Nu`aym al-'Isfahani, Hilyat al-Awliya', (Beirut, 1988), Juz. 5, Uk. 27
" Nur al-Din al-Halabi al-Shafi'i, al-Sirah al-Halabiyya, Juz. 3, Uk. 336
" Al-Muttaqi al-Hindi, Kanz ul-'Ummal, (Halab, 1969-84), Juz. 13, Uk. 131
Sheikh Juma nawe tahadhari usije ukapata alama kwa kuukanusha Ukhalifa wa Ali Bin Abu Talib na kwa kumkanushia Hadithi nyingi zenye kutaja Ubora na Fadhila zake, hata umethubutu kusema kuwa Ali hakuwa na elimu hata kuliko Ibnu Abbas !!!!!!! Maa Shaallah! Haya Maa salaam, Wahida Marjana.
MWISHO