ATHARI YA KUJIULIZA
  • Kichwa: ATHARI YA KUJIULIZA
  • mwandishi: Taqee Zacharia
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 18:28:10 6-10-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

SOMO LA TATU.

ATHARI YA KUJIULIZA KATIKA MAISHA YA MWANADAMU.

Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakatuh.
Iwapo mwanadamu atayajibu vizuri maswali yanayohusiana na Muumba wa Ulimwengu na Mwanzilishi wa mfumo wake, maswali yanayomjia kutokana na maumbile yake ya kutaka kujua uhakika wa vitu,basi bila shaka atathibitisha Muumba wa Ulimwengu huu na Mfumo wake wa ajabu asiyekuwa na mwanzo wala mwisho.Jambo hili pia litamfanya akiunganishe kila kitu na azma yake thabiti inayotegemea uwezo na elimu yake isiyokuwa na mwisho. Hatimaye mwanadamu atajipata kuwa na joto la kadiri na matumaini.Hukabiliana inavyopaswa na matatizo yanayomkumba maishani mwake na kamwe hakati tamaa kuhusiana na yale matatizo asitoweza kuyatatua.Hii ni kwasabu hutambua kuwa kila kitu humu duniani kiwe na uwezo mkubwa kitakavyokuwa nao,kiko chini ya uwezo na uthibiti wa Mwenyeezi Mungu (s.w).

Mtu kama huyo huwa si rahisi kwake kusalimu amri kirahisi mbele ya mambo mbali mbali yanayomkumba maishani mwake.Hata akiona kuwa kila kitu kiko katika manufaa na faida yake huwa hajivuni wala kuwa na wivu ili asije akasahau nafasi yake na ile ya Ulimwengu.Hii ni kwa sababu hutambua kila chanzo na sababu iliyomo humu duniani haifanyi kazi wala kusababisha kutokea kwa jambo jingine yenyewe bali husababisha kutokea kwa jambo hilo kwa mujibu wa utaratibu aliouweka mwenyeezi mungu (s.w).Mwisho mtu kama huyo huamua kuwa hakuna mtu apaswaye kutiiwa ispokuwa Mwenyeezi Mungu (s.w) na kuwa hapaswi kutii moja kwa moja amri za mtu yeyote yule ispokuwa amri za Mwenyeezi Mungu (s.w) Muumbwa wa kila kitu.

Hata hivyo kwa yule ambaye huyajibu vibaya maswali haya hujinyima matarajio,ukweli,moyo mkuu na ushujaa wa kimaumbile.Kwa mfano mzuri ni kwamba sisi wenyewe (yaani mimi na wewe) huona idadi ya watu wanaojinyonga wenyewe ikizidi kuongozeka kila siku katika mataifa yanayozingatia zaidi maada.

Wale ambao nyoyo zao zimefungamanishwa kwenye vitu visivyokuwa thabiti hukata tamaa mara moja wanapokumbana au wanapokabiliwa na tatizo dogo kuwapelekea kujinyonga wenyewe. Katika upande mwingine wa pili mtu anamwamini Mwenyeezi Mungu (s.w) huwa hakati tama hata anapokaribia kifo.Huwa daima wana matarijio makubwa kuhusiana na uwezo na pia baraka za Mwenyeezi Mungu (s.w).

Mfano mzuri ni huu hapa kutoka kwa Sayyid Ash-shuhadaa Imam Husein (a.s): Katika masaa ya mwisho ya maisha yake wakati ambapo panga za maadui zilikuwa zimemwelekea kutoka kila upande,Imam Husein (a.s) alisema sentensi hii: "Jambo la pekee litakaloweza kuyaondoa machungu na balaa hili kubwa ni mtazamo (kuona) wa Mwenyeezi Mungu usiokoma wa vitendo vyangu." Qur'an Tukufu inalizungumzia jambo hili katika aya kadhaa. Mwenyeezi Mungu (s.w) anasema:

*إنَّ الذين قالوا ربُّنا الله ثم استقاموا فلا خوف عليهم ولا هم يحزنون*

"Hakika wale waliosema Mola wetu ni Mwenyeezi Mungu, kisha wakadumu imara,hawataogopa wala hawatahuzunika"

*الذين آمنوا وتطمَئِنَّ قلوبَهُم بذکرِ اللهِ ألا بذکر اللهِ تطمئِنُّ القلُوبِ*

"Wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyeezi Mungu,sikilizeni!kwa kumkumbuka Mwenyeezi Mungu,nyoyo hutulia"

NJIA YA KUMJUA MWENYEEZI MUNGU KATIKA MTAZAMO WA QUR'AN.

Mtoto mdogo anayeshika maziwa au matiti ya mama yake kwa mikono yake,hunyonya matiti hayo kwa lengo la kupata maziwa hayo.Bila shaka huwa nataka maziwa,na anapokichukua kitu chochote kwa lengo la kutaka kukila basi bila shaka atakielekeza katika mdomo wake.Lengo lake halisi ni kula.Iwapo atapata kuwa kitu alichokichukua ili akile hakiliki basi hukitupilia mbali.Kwa njia hiyo hiyo mwanadamu hutafuta uweli na hakika katika kila kitendo anachokitenda au anachokifanya.Anapopata kujua kuwa amekosema hujuuta na kuumia kwanini amejisumbuya bure na kukose katika kitendo hicho.Daima mwanadamu hujiepusha na makosa na hujaribu kuufikia ukweli na hakika,kadiri ya uwezo wake.

Jambi hili linaashiria nukta hii kwamba kimaumbile na kihisia mwanadamu ni mkweli.Yaani atake au asitake daima hutafuta ukweli na kufuata haki.Mwanadamu hakufunzwa jambo hili na mtu yeyote yule wala kutoka sehemu yoyote ile.Iwapo mara nyingine mwanadamu hukana na kukataa haki,huwa ni kwa sababu amechanganyikiwa kutokana na makosa na kutotofautisha kati ya haki na batili na iwapo haki itambainikia basi bila shaka huifuata haki hiyo na hawezi kuifuata batili hata siku moja.Mara nyingine pia mwanadamu huparta maradhi ya nafsi kutokana na tamaa, majivuno na kuipenda nafsi yake kupindukia.Hali hii huibadilisha ladha nzuri ya ukweli kuwa chungu.

Haki ikisha kuwa chungu kwake utaona mwanadamu huyo anaipinga haki na kutoifuata hata kama anaifahamu vyema haki na utaona najitahidi kila awezavyo kuificha haki na kudhihirisha batili hali ya kuwa anajua uweli uko wapi.Hata kama mtu wa aina hii hukubali uzuri wa haki na kukiri umuhimu wa kuifuata lakini yeye huwa hawezi kusalimu amri mbele ya haki.Jmabo hili ni mfano wa mambo yanayotokea kutokana na mazoea ya utumizi wa vitu vyenye madhara,mwanadamu huikandamiza hisia yake ya kimaumbile(ambayo ni ya kuondoa kuondoa hatari na kuepuka madhara) na kufanya kitendo cha kumsababishia madhara (kama wale waliozoea kuvuta sigara,kunywa pombe na kuvuta madawa ya kulevya).

Watu hawa hujishughulisha na utumiaji wa vitu hivyo kutokana na kuipinga hisia yao ya kimaumbile maana hisia hiyo huwajulisha wazi kuwa kufanya hivyo(yaani kuvuta sigara na kadhalika) kuna madhara katika afya ya mwili wako,lakini watu hao huipinga na kuikandamiza hisia hiyo iliyokuwa na lengo la kuzuia madhara yasitokee na hatimaye wanapovuta sigara hizo au kunywa pombe hizo madhara mbalimbali hupatikana na watu hao hudhurika kirahisi.

Qur'an tukufu humsihi mwanadamu kuzingatia ukweli na kuifuata haki.Qur'an tukufu inasisitiza juu ya jambo hili kwa njia mbali mbali na kuwataka wanadamu wailinde na kuihifadhi hisia yao ya (kimaumbile) ukweli na inayotatua haki. Mwenyeezi Mungu (s.w) anasema:
*فماذا بعد الحق إلا الضلال...*

"Tena ni nini baada ya haki ispokuwa upotofu?

ITAEDELEE.

Suuratul Ahqaaf:Aya ya 13.
Suuratur-raa'd:Aya ya 28.
Suurat Yuunus:Aya ya 32.