HATARI ZA BID_A
  • Kichwa: HATARI ZA BID_A
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:9:18 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

HATARI ZA BID_A

Katika makala iliyopita (makala namba 2), tulielezea maudhua yanayohusiana na sifa tukufu za Mitume, na tukabainisha sifa mbili ambazo wanatakiwa Mitume kuwa nazo, sifa hizo zilikuwa ni elimu, na kuwa Maasumu, katika makala namba mbili tulifikia sehemu inayosema kuwa, "kama angelizua juu yetu baadhi ya maneno" ambayo ni tarajama ya Aya ya 44 ya Surat Haaqqah, basi tukapata maelezo na maudhui yanayohusiana na Aya hiyo, maudhui hayo yalikuwa ni Bid-a, katika makala hii tutaelezea kwa kina kuhusiana na maudhui hayo.

UFAFANUZI WA NENO BID_A.

Neno "Bid-a kilugha ni: lina maana ya Lenye kuzuka" ikiwa ni zuri au baya.

Ama "Bid-a kitaalamu (kiistilaha) ni hivi asemavyo Mtume Muhammad (s.a.w.w) "kila lenye kuzuka ni upotovu, na upotovu wote utatupwa motoni"

"Yatakapotokeza yenye kuzuka katika umati wangu basi mwanachuoni aonyeshe elimu yake (kwa kukanya hayo) na yeyote asiyefanya (hilo) basi laana ya Mwenyeezi Mungu iko juu yake."

(Rejea wasailu Shia.j.16.uk.269-272).

Imam Husseyn Bin Ali (a.s) anasema:-

" Enyi watu! hakika Mtume wa Mwenyeezi Mungu amesema":-

" Atakayemuona mtawala muovu anahalalisha haramu ya Mwenyeezi Mungu, anavunja ahadi ya Mwenyeezi Mungu, anaacha sunna za Mtume wa Mwenyeezi Mungu, anawatendea maovu na uadui waja wa Mwenyeezi Mungu, na asikanye kwa kitendo au kwa kusema, ni haki kwa Mwenyeezi Mungu kumtia popote." (rejea Tarekhut tabari, j.4,uk.304).

Mayahudi na waliokuwa kabla yao walivuka mipaka katika kuwatukuza Manabii na watu wema mpaka wakawafanya baadhi yao kuwa ni watoto wa Mungu. wakiristo nao waliendelea kuwa kama Mayahudi wa kumtukuza Nabii Issa na mama yake bibi Maryam (a.s) wakamfanya Issa kuwa ni mtoto wa Mungu. kama anavyosema allah (s.w) katika kitabu chake kitukufu:-

Katika Qur-ani takatifu kuna Aya nyingi zinazoelezea kwa uwazi kabisa kuhusiana na akida au uzushi wa Mayahudi na Manasara, na Mwenyeezi Mungu amezichukia na kubainisha kuwa akida hizo sio sahihi, pale aliposema:-

وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَنُ وَلَداً . لَقَدْ جِئْتُمْ شَيْئاً إِدّاً . تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الاَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدّاً. اَن دَعَوْا لِلرَّحْمَنِ وَلَداً[1]

Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana! Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno! Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana.

Na katika Aya nyengine anasema:-

وَقَالُواْ لَن يَدْخُلَ الْجَنَّةَ إِلاَّ مَن كَانَ هُوداً اَوْ نَصَارَي تِلْكَ اَمَانِيُّهُمْ قُلْ هَاتُواْ بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ[2]

Na walisema: Hataingia Peponi ila aliyekuwa Yahudi au Mkristo. Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli.

Na katika Aya nyengine anasema hivi:-

وَلَن تَرْضَي عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَي حَتَّي تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَي اللهِ هُوَ الْهُدَي وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ اَهْوَاءهُم بَعْدَ الَّذِى جَاءكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللهِ مِن وَلِيٍّ وَلاَ نَصِيرٍ[3]

Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.

Na katika Surat Almaidah anasema hivi:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَي اَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ اَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللّهَ لاَ يَهْدِى الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ[4]

Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.

Maelezo kuhusiana na Aya:

Aya nyingi sana zimetukataza kuwafanya wasiri wetu, na baadhi yake tumekwisha kuzitaja. Tumehimizwa kuwafanyia:-

a) Uadilifu katika haki zao.

b)Kuwafanyia mema kwa chetu na yetu, ama hapana ruhusa kuwafanya wasiri wetu, kwa kila namna hawana usafi wa roho na sisi, wana misiba ya nyoyo juu yetu na uadui wa milele.

Basi natija tunayoipata kutokana na aya hizo ni kuwa :-

Mayahudi na Manasara wamezua mengi ambayo hayakuamrishwa na Mwenyeezi Mungu wala Mitume (a.s).

[1] Surat Maryam Aya ya 88-91

[2] Surat Albaqarah Aya ya 111.

[3] Surat Albaqarah Aya ya 120

[4] Surat Almaidah Aya ya 51

MWISHO