HISTORIA YA QUR_ANI
  • Kichwa: HISTORIA YA QUR_ANI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 3:58:49 2-9-1403

 

                                                BISMILLAHI RAHMANI RAHIM

HISTORIA KUHUSIANA NA MAUDHUI YA MIUJIZA

DOCTOR SAYYID RIDHA MUADAB

Ijapokuwa haieleweki ya kwamba maudhui kuhusu miujiza yalianza kipindi gani, lakini muujiza wa qur-ani ndio maudhui ya mwanzo yaliyokuja yanayohusiana na Qur-ani. Na Qur-ani tukufu kwa kuthibitisha madai yake hayo – yaani kuwepo kwa muujiza kuhusiana na kitabu hicho – imetumia neno muujiza, katika kipindi chote hicho kilichopita Qur-ani inapoelezea kuhusu miujiza ya Mitume hutumia neno (ايه na  بينه) kwa kuthibitisha kuwepo kwa miujiza, na kwa sababu hiyo basi neno (istilaha) muujiza (معجزه)  kutokana na riwaya au hadithi zilizokuja ndio neno la mwanzo lililotumika kuthibitishia madai yake hayo1. na baadae ndio zikatumika istilaha (maneno) nyengine, na istilaha hizo ziliendelea kuenea siku hadi siku2.

Katika kitabu kitukufu cha Qur-ani vile vile hakujatabiriwa neno (خارق العادة) – khaariqul-addat – (yaani amali au matendo ambayo hakuna mwanaadamu yoyote anayeweza kuyafanya isipokuwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu (s.w), na Mitume huyafanya matendo hayo kwa uweza wa Mwenyeezi Mungu (s.w), na kwa idhini ya Mola wao). Kwa hiyo Istilaha neno – muujiza – ni miongoni mwa istilaha ambayo imeanzishwa na Maulamaa wa dini ya kiislamu.

Marhala ya mwanzo inayotokana na muujiza wa Qur-ani ni athari za wafasiri wa Qur-ani, wataalamu wa kilugha, na …, wataalamu hao walikuwa na itikadi ya kwamba  Qur-ani takatifu ni alama (nembo), na dalili inayothibitisha ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kwa kuzingatia historia ya tarehe kuhusiana na miujiza itaeleweka ya kwamba mabhathi (maudhui) yanayoelezea kuhusu muujiza wa Qur-ani yameanza katika karne ya pili3.

Maudhui ya mwanzo kabisa yameanzishwa na Maulamaa na wataalamu wa dini ya kiislamu, na walianzisha maudhui hayo baada ya kuja kwa watu waliojitahidi kuleta propaganda zao kutaka  kuipinga Qur-ani na kuikhalifu, kwa hiyo Maulamaa hao walijitahidi kielimu kuthibitisha utukufu wa Qur-ani na yaliyomo katika kitabu hicho, kitabu ambacho kinafuatana na maisha ya mwanaadamu na kinaelezea mfumo mzima wa maisha ya mwanaadamu, nidhamu na fani iliyotumika katika kitabu hicho haifanani na kitabu chochote duniani, maneno, mazungumzo, balagha, n.k… iliyomo katika kitabu hicho yote hayo yanaonyesha utaalamu wa kielimu na utukufu wa kitabu hicho. Kitabu ambacho elimu iliyomo humo sio ya mwanaadamu bali ni ya Mwenyeezi Mungu mtukufu mwenye elimu ya hali ya juu kabisa isiyokadiriwa na mwanaadamu yeyote ulimwenguni.

Mwishoni mwa karne ya pili, na mwanzoni mwa karne ya tatu ni karne ambazo wataalamu na maulamaa walianza kutoa nadharia zao za kuthibitisha muujiza wa Qur-ani na nadharia hizo ziliendelea siku hadi siku, na zilisababisha kuandikwa vitabu vingi vinavyohusiana na muujiza wa Qur-ani, miongoni mwa vitabu hivyo ni:-

Maanil-Qur-ani, kilichoandikwa na Yahya bin Ziyaad Farra-a (aliefariki 207), na kitabu kinachojulikana kwa jina la Majazil-Qur-ani, kilichoandikwa na Abuw-Ubeyda Maamari- ibni Mathna (aliyefariki 209).

Katika karne ya 3 bwana Is-haqa Ibrahiym yeye ni mfuasi wa madhehebu ya muutazaliy (aliyefariki .220) kuhusiana na maudhui ya nidhamu ya Qur-ani alikuja na nadharia inayojulikana kwa jina la (صرفه) – Sarfe -  (yaani mwanaadamu yeyote yule anayetaka kupingana na yale yaliyomo ndani Qur-ani Mwenyeezi Mungu hatompa nguvu mtu huyo za kufanya anayoyataka). Sheikh Is-haqa alikuja na nadharia hiyo ili kuithibitisha muujiza wa Qur-ani na utukufu wa kitabu hicho, na baadae mwanafunzi wake sheikh Is-haqa anayejulikana kwa jina la Abu Othmani Amru bin Bahr bin Mahbuwb maarufu kwa jina la Jaahidh (aliyefariki 255), akaipinga nadharia ya mwalimu wake, kwa kuandika kitabu kinachojulikanwa kwa jina la Nidhamul-Qur-ani4.

Abu Othmani ana kitabu chengine kinachojulikanwa kwa jina la Al-hayawani, katika kitabu hicho ameelezea maudhui kuhusiana na muujiza wa Qur-ani 5. Nadhari zake Sheikh Othmani kuhusiana na muujiza wa Qur-ani zilikuwa zikiwavutia Maulamaa na Wataalamu wengi katika zama zake.

Miongoni mwa wataalamu wengine ambao walijitokeza katika karne ya tatu ni sheikh Muhammad bin Omar bin Said Bahaaliy aliyefariki (300), bwana huyo ameandika kitabu kinachojulikana kwa jina la Muujiza wa Qur-ani (اعجاز القران) .

Mnamo karne ya nne maudhui kuhusiana na muujiza wa Qur-ani yalizidi kuenea na kusambazika sehemu zote, katika karne hiyo ya nne sheikh Muhammad bin Yazid Wasity aliyefariki (306) aliandika kitabu kinachojulikanwa kwa jina la I- ijazul-Qur-ani fiy nadhmihi wa Ta-aliyfihi (كتاب اعجاز القران في نظمه و تاليفيه).

Na Sheikh Aliy bin Issa Rumaniy aliyefariki (384), yeye ni mwanazuoni na mfuasi wa i-itizaliy, na ameandika kitabu kinachojulikanwa kwa jina la kitabu Nakth fiy I-ijazul-Qur-ani.

(كتاب النكث في اعجاز القران)6                                                                           

Ahmad bin Ibrahim Kahatabi aliyefariki mwaka (388), ujumbe kwa ufupi kuhusiana na muujiza wa Qur-ani, ujumbe huo ameuandika katika juzuu na akaelezea kwa ufupi kabisa kuhusu muujiza wa qur-ani, na ujumbe huo unajulikanwa kwa jina la Bayani I-ijazul-qur-ani, (بيان اعجازالقران).

Katika karne ya tano Abubakar Muhammad bin Tayyib Baaqalaniy aliyefariki (403), aliandika kitabu I-ijazul-qur-ani, ndani ya kitabu hicho alithibitisha muujiza wa qur-ani, na baadae Kadhi Abdul-Jabbar (415), katika juzuu ya 16 ya kitabu kinachojulikanwa kwa jina la  Almughni fiy Abwabi Tawhid Wal-adli (كتاب المغني في ابواب التوحيد والعدل), katika kitabu hicho ameelezea kuhusu muujiza wa qur-ani.

Ibni Saraqah (420), Sharifu Mur-tadha (436), Sheikh Tuwsiy (460), na Abdul-Qaahir Jarjaniy (471), ambaye ni mmiliki wa  kitabu Dalaili I-ijazu, (دلايل الاعجاز) wote hao walikuwa katika karne ya tano waliuelezea na kuuthibitisha muujiza wa Qur-ani, na walizidi kueneza na kuyasambaza maudhui hayo7                  

Katika karne ya sita Mahmuwd bin Omari Jaaru-llahi Zamakhshariy (538), mbali na vitabu vyake vyengine vya tafsiri, moja miongoni mwa vitabu hivyo ni kitabu kijulikanachwo kwa jina la Alkashaf, vile vile ana kitabu chengine kiitwacho I-ijazul-qur-ani ndani ya suratul-kawthar, na sheikh kadhi Ayadh (544), ndani ya kitabu chake I-ijazulqur-ani, na Ibni Atiyya Andalus (546), mwanzoni mwa tafsiri yake itambulikwanayo kwa jina la Almuharar Alwajiyz fiy tafsiri kitabul-aziyzi, (الوجيز في تفسير كتاب العزيز المحرر), sheikh Tabrasiy, amiynil-Islamu (548), katika utangulizi wake wa kitabu cha tafsiri Majmaul-bayani liulumil-qur-ani, na marehemu saidi bin Hussein Habbatu-llahi rawandi (573)       , ni mtowa hutuba na mawaidha mkubwa katika kitabu chake I-ijazul-qur-ani na tafsiri ya suratul-kawyhar ameelezea njia na vipengele vinavyohusiana na muujiza wa Qur-ani.

Katika karne ya saba hadi sasa hivi Maulamaa wengi vile vile wameendelea kufafanua na kuelezea muujiza wa qur-ani, miongoni mwa Maulamaa hao ni mfano wa Fakhru Razi (606), katika kitabu chake vI-ijazul-qur-ani, na dalili za muujiza wa qur-ani, sheikh Zamalakaniy (651), katika kitabu Tibyani fiy ilmi bayani Almutalaa alal-iyjazil-qur-ani, (ن في علم البيان المطلع علي اعجازالقران التبيا كتاب)

Abu-Is-haqa Khazraji (709), kitabu i-yjazu Albur-hanu fiy I-ijazul-Qur-ani, Abul-kheyri Jazriy Damashqiy (833), kitabu I-ijazul-Qur-ani fiy aya ya Ardhi Ab-aliy, (كتاب اعجازالقران في ايه يا ارض ابعلي)8.
Suyutiy (911), kitabu Muu-tarak al-aqraani fiy i-ijazul-qur-ani, (كتاب معترك الاقران في اعجازالقران), na sheikh Alame Tabatabai (1045), n.k… ameacha vitabu vingi alivyoviandika vyenye faida vinavyoelezea kuhusu muujiza wa Qur-ani.

UFAFANUZI WA NENO MUUJIZA

Neno muujiza kilugha asili yake linatokana na neno ajaza (عجز)  ajaza yaaani mwishoni mwa kitu, maana hiyo vile vile imekuja ndani ya Qur-ani, pale Allah (s.w.) anaposema:-

إِنَّا اَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحاً صَرْصَراً فِى يَوْمِ نَحْسٍ مُّسْتَمِرٍّ9

Hakika tuliwapelekea upepo mkali katika siku ya nuhusiniendeleayo (kwao mpaka leo).

تَنزِعُ النَّاسَ كَاَنَّهُمْ اَعْجَازُ نَخْلٍ مُّنقَعِرٍ10

Ukiwang’oa watu (katika ardhi kisha unawabwata chini, wamelala, wamekufa) kama kwamba ni magongo ya mitende iliyong’olewa.

 

  MWISHO

[1] Buharul-an-war, (kitabu Nubuwat), kimeandikwa na Sheikh Alame Majlis, juzuu 11, ukurasa wa 71

[2] I- ijazul-Qur-ani, kimeandikwa na Abi- Ubayda, ukurasa wa 208

[3] I-ijazul-Qur-anil-bayaani, ukurasa wa 48.

[4] I-ijazul-Qur-ani, ukurasa wa 152

[5] Al-hayawani, juzuu ya 3, ukurasa wa 4288, na feherest Ibn Nadiym, ukurasa wa 65

[6]  Almuujizal-kubra, ukurasa wa 84, na I-ijazul-bayani, ukurasa wa 88

[7] Al-iijazu fiy Diraasati Assabiqiyna, ukurasa wa 150- 372.

[8] Dar omadiy fi tarikh ulumul-qur-ani, ukurasa wa 254.

[9] Qamar,19

[10] Qamar, 20