UMUHIMU WA HIJABU KATIKA JAMII
  • Kichwa: UMUHIMU WA HIJABU KATIKA JAMII
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 4:5:58 2-9-1403

                                                                                                                       BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU
UMUHIMU WA KUVAA HIJABU KATIKA JAMII. NO.2

Katika makala zilizopita tulielezea umuhimu wa kuvaa hijabu katika jamii, na tukaashiria baadhi ya masuala ambayo yanahusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu, tunamshukuru Mola kwa kutupa nguvu za kuweza kuyajibu masula hayo, katika makala hii tutaendelea na mada yetu hiyo hiyo, tunategemea mtafaidika na tutakayoyaeleza yanayohusiana na umuhimu wa kuvaa hijabu.

Miongoni mwa masuala yaliyoulizwa ni haya yafuatayo:-

MIMI SINA MALENGO YA KULETA UFISADI WALA UPOTOSHAJI.

Katika barua yako umeniandikia hivi:

“Ingawaje mimi navaa nguo zinazokwenda na wakati mbele za wanaume, na nnajipamba lakini katu sina lengo la kuleta ufisadi au upotoshaji.

 Kabla ya mimi kutowa msimamo wangu kutokana na maelezo yako na jawabu zako kwanza nna masuala machache naomba kukuuliza, itokee siku umerudi kazini hali ya kuwa umechoka sana kwa kazi, na una haja ya kupata mapumziko, ama jirani yako akawa amefunguwa tivii au redio kwa sauti kubwa, na hana nia ya kukera amefanya hivyo kwa sababu tu anapenda, hivi ni kweli kwa kufanya hivyo hakutokusababishia wewe kutokupumzika?

 Jee! Hivi wewe imewahi kukutokezea siku katika msimu wa baridi ukapanda texi, lakini karibu yako kukawa kuna mtu nanataka kuwasha sigara, kwanza akaomba radhi na kusema kwamba hana budi kuvuta sigara kwa sababu anhisi baridi, hivi ni kweli moshi wa sigara hautokudhuru eti kwa kuwa kwanza ameomba radhi? Na wala hutokasirika?

Jee! Ikiwa mtu amenunuwa bakora mpya kasha akaijaribishia katika kichwa cha mtu ili aijuwe umadhubuti wake, jee kufanya kwake hivyo hakutamletea madhara mtu huyo aliyempiga? Kwa sababu tu yeye hakuwa na makusudio ya kumdhuru, alikuwa na makusudio ya kuijaribu bakora yake tu kama ni nzima.

Basi hivi sasa  baada ya utangulizi huo uliopita tunaweza kupata natija ya kwamba kitu chenye kuleta madhara huwa kinaleta madhara tu, hata kama mtendaji wa kitu hicho hakusudii kuwadhuru wengine, hapo sasa ndio tumefika jawabu ya lile suala lako lisemalo “mimi najipamba na vile vile sivai hijabu lakini sina makusudio ya kharibu jamii, vipi kwangu mimi nitalazimishwa kuvaa hijabu”

WENGI WALIOJE WASIOKUWA NA HIJABU KWANGU MIMI IMEKUWA AJABU?

Kwa kutokana na kwamba kuna watu wengi wasiovaa hijabu, taka usitake lazima jamii itaathirika nao hata kama mimi nitaamua kuvaa hijabu, kwa hiyo kuvaa kwangu au kuto kuvaa kwangu hijabu haina maana yeyote, au hakuleti athari yeyote katika jamii.

 Mimi nna itikadi ya kwamba hata kama wanawakle wote majiani hawatakuwa wakivaa hijabu basi wewe dalili ya kuvaa hijabu, kwani Mola ndie aliyekuamrisha kufanya hivyo.

KWANZA KABISA NI KWAMBA WEWE USIWE NDIYO MUHUSIKA AU MTUHUMIWA KATIKA MAKOSA YANAYOTENDEKA KATIKA JAMII.

 Kila mtu atakaefanya makosa basi yeye ndie mtuhumiwa katika makosa hayo, na ni lazima awe ni mwenye kuhojiwa mbele ya mahakama ya Mola wake.

 Iwapo mtu atakuwa ana habari kwamba usiku wa leyo wezi wana makusudio ya kuivunja nyumba ya jirani yake ambae amesafiri, na akawa na yakini kwamba bila ya shaka mazulio ya jirani yake yataibiwa, kisha katika moyo wake akasema kwa hali yoyote ile mazulia ya jirani yake yatamtoka tu kutoka katika mikono mwake,

 Basi mimi mwenyewe ntayachukuwa haya mazulia, na kabla ya kuja wezi nyumba ya jirani yeye akaenda akayachukuwa mazulia na kuyapeleka kwake, huku akisema nikiyawacha wezi watakuja kuyachukuwa, na nisipoyawacha nitafaidika mimi, kwa hiyo hakuna faida kuyawacha wewe mtu kama huyo utamuhukumu vipi katika tendo hilo alilolifanya? Ikiwa utasema iwapo wakiyachuwa au wasiyachukuwe kwa jirani ni sawa tu, kwani wengelikuja wakayachukuwa wezi kwa hiyo hakuna tofauti ya kuibiwa na jirani au kuibiwa na wezi, cha umuhimu ni kwamba usiku ule mazulia yataibiwa tu, awe ni jirani au mwizi, alipokwenda kuyachukuwa yeye mazulia hakuzidisha kitu katika uovu, ama hapa suala haliko hivyo, kwani hivi sasa baada ya kuyachukuwa yeye ndie atakayekuwa na jukumu, na ndiye atakayetakiwa kulipa hasara, na wangeliyachukuwa wezi basi wao ndiyo wangelikuwa na jukumu hilo.

 Katika upande wa hijabu ndiyo hivyo hivyo, kuwepo wanawake wengi wasiyovaa hijabu kwenye kuwapoteza watu katika jamii, na wewe ukawa miongoni mwao basi nawe vile vile utahusika katika upotoshaji wa jamii.

MWISHO