MAFANIKIO YA MITUME NO 5
  • Kichwa: MAFANIKIO YA MITUME NO 5
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 3:40:10 2-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MAFANIKIO YA MITUME

*Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu?

MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.4

Katika makala iliyopita, (makala namba tatu) tulielezea sababu na dalili zilizopelekea Mitume kupata mafanikio katika kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu, katika maelezo ya makala hiyo tulielezea dalili mbili, katika makala hii tutaelezea sababu nyengine zilizosababisha kuwaletea Mitume mafanikio katika malinganio yao.

5. KUTOISHI MAISHA YA KIFAHARI, NA KUWA MBALI NA ANASA ZA DUNIA.

Mitume ya Mwenyeezi Mungu iliishi maisha yasiyokuwa ya kifahari, na hii ni alama moja wapo iliyowafanya wasadikike (waaminiwe), na ukweli wao ulidhihirika pale walipojiweka mbali na anasa za dunia, na kufikiria maisha yao ya Akhera, na hii ni moja miongoni mwa siri za mafanikio yao, zilizowafanya watu wawaamini na kuwatii.

Mitume Mitukufu, sio wao tu waliojitosheleza kuishi maisha duni, bali familia zao na watu wa karibu yao pia waliwazuilia kuishi maisha ya kifahari, na waliwataka wasighilibiwe na anasa za dunia,kama anavyosema Allah (s.w) kumwambia Mtume Muhammad (s.a.w.w) :-

يَا اَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّاَزْوَاجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدْنَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيْنَ اُمَتِّعْكُنَّ وَاُسَرِّحْكُنَّ سَرَاحاً جَمِيلاً[1]

Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni mwachano mzuri.

Mitume ya Mwenyeezi Mungu, walikuwa na uhakika kuwa, anasa za dunia ni kidogo na zenye kupita (kumalizika) upesi, na kukusanya mali bila ya kuitumia katika mambo ya kheri ndani ya jamii,matokeo yake ni kuwa maghururi, na kughafilika katika dunia, na kupata adhabu kali iumizayo siku ya Kiama, kama walivyosema kundi la wafuasi wakweli na wasadikifu wa Nabii Mussa kumwambia Qaaruna, “ kwa mali ambayo Mwenyeezi Mungu amekupa usiifanyie ufisadi, na ifanyie amali njema ambazo zitakusaidia siku ya Kiama”

وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللهُ الدَّارَ الآخِرَةَ وَلاَ تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا وَاَحْسِن كَمَا اَحْسَنَ اللهُ إِلَيْكَ وَلاَ تَبْغِ الْفَسَادَ فِى الاَرْضِ إِنَّ اللهَ لاَ يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ

Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi Lakini Qaaruna aliwajibu:-

قَالَ إِنَّمَا اُوتِيتُهُ عَلـٰي عِلْمٍ عِندِى اَوَلَمْ يَعْلَمْ اَنَّ اللهَ قَدْ اَهْلَكَ مِن قَبْلِهِ مِنَ القُرُونِ مَنْ هُوَ اَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً وَاَكْثَرُ جَمْعاً وَلاَ يُسْاَلُ عَن ذُنُوبِهِمُ الْمُجْرِمُونَ[2]

Akasema: Kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya ilimu niliyo nayo. Je! Hakujua kwamba Mwenyezi Mungu kesha waangamiza, katika vizazi vya walio kabla yake, watu walio kuwa wenye nguvu zaidi kuliko yeye, na wenye makundi makubwa zaidi kuliko yake. Na wakosefu hawataulizwa khabari ya dhambi zao.

[1] Surat Al-Ahzaab Aya ya 28

[2] Surat Al-Qasas Aya ya 77-78

MWISHO