BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
MAFANIKIO YA MITUME
*Ni dalili gani zilizowasaidia Mitume kuweza kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu?
MAFANIKIO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.6
Katika makala iliyopita, (makala namba tano) tulielezea sababu na dalili zilizopelekea Mitume kupata mafanikio katika kufikisha ujumbe wao kwa wanaadamu, katika makala hii tutaelezea sababu nyengine zilizosababisha kuwaletea Mitume mafanikio katika malinganio yao.
8. KUSHAURIANA NA WATU NA KUWA PAMOJA NAO.
Sababu nyengine zilzopelekea mafanikio ya Mitume katika kuwalingania watu, ni kushauriana nao na kuwa pamoja nao katika harakati zake za kidini, hii ilipelekea watu kuwakuza kifikra, Mitume iliwashirikisha wafuasi wao katika mambo mbali mbali ya kidini, kijamii, kisiasa, n.k. kama tunavyoona katika harakati zake Mtume Muhammad (s.a.w.w.) baadhi ya wakati alishauriana na wafuasi wake katika mambo ya kupigana vita, au kusuluhisha, alikaa na wafuasi wake na kushauriana, na alikubali nadharia iliyotolewa na wengi, ijapokuwa baadhi ya wakati kulitokea matatizo wakati alipokubali nadharia ya wengi, kwa mfano katika vita vya Uhud, hii ilikuwa ni nadharia ya wengi, lakini kwa sababu mashauriano baadhi ya wakati huleta madhara, vile vile huleta baraka, kama anavyosema Allah (s.w):-
فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللهِ لِنتَ لَهُمْ وَلَوْ كُنتَ فَظّاً غَلِيظَ الْقَلْبِ لاَنفَضُّواْ مِنْ حَوْلِكَ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِى الاَمْرِ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلـٰي اللهِ إِنَّ اللّهَ يُحِبُّ الْمُتَوَكِّلِينَ[1]
Basi ni kwa sababu ya rehema itokayo kwa Mwenyezi Mungu ndio umekuwa laini kwao. Na lau ungeli kuwa mkali, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeli kukimbia. Basi wasamehe, na waombee maghfira, na shauriana nao katika mambo. Na ukisha kata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao mtegemea.
Kuhudhuria kwa watu, na kuwa pamoja na Mitume katika tabu, mashaka na vita kumeleta athari kubwa kwa watu hadi kufikia katika mafanikio na kupata ubingwa, kama tunavyosoma kuhusiana na Mitume na wafuasi wake:-
اَمْ حَسِبْتُمْ اَن تَدْخُلُواْ الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَاْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْاْ مِن قَبْلِكُم مَّسَّتْهُمُ الْبَاْسَاء وَالضَّرَّاء وَزُلْزِلُواْ حَتَّي يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُواْ مَعَهُ مَتَي نَصْرُ اللهِ اَلا إِنَّ نَصْرَ اللهِ قَرِيبٌ[2]
Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.
*Hapa Mwenyeezi Mungu anabainisha – kama mahala pengi pengine katika Qur-ani – kuwa Mwislamu apate misukosuko katika kuendesha Uislamu wake, hapana la faida lolote linalopatikana kwa urahisi, na hii misukosuko ndiyo inayomtengeneza mtu .
Maelezo kwa ufupi kuhusu makala zilizopita.
* Sababu zilizopelekea mafanikio ya Mitume katika kufikisha ujumbe wao ni:- Ukweli, upendo, ikhlasi, kutoishi maisha ya kifahari, ushujaa, kushauriana na kuwa pamoja na watu.
Masuala.
1. Mandhuri ya mafanikio ya Mitume ni nini?
2. Kwa nadharia yako, sababu muhimu ilipelekea mafanikio ya Mitume ni ipi?
3. Kwa kuzingatia Aya za Qur-ani, qur-ani takatifu imesifu vipi mapenzi ya Mtume kwa wanaadamu?.
4.Elezea, ikhlasi ya Mitume imeleta mafanikio gani katika kufikisha ujumbe wao?.
5. Kwa nini Mitume haikuchukua ujira wowote kutoka kwa watu wake kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa Mwenyeezi Mungu?
6.Mitume kutoishi maisha ya kifahari kunaonesha alama gani kwao?.
[1] Surat Aal-Imrani Aya ya 159
[2] Suratul-Baqarah Aya ya 214
MWISHO