MAKHALIFA WASIOPASWA KUTIIWA
  • Kichwa: MAKHALIFA WASIOPASWA KUTIIWA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 3:17:40 2-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MAKHALIFA WASIOPASWA KUTIIWA

Katika makala zilizopita tulielezea kuhusiana na wale makhalifa wanaopaswa kutiiwa. katika makala hii tutaendelea na mada yetu inayohusiana na maudhui hayo hayo.

5- Wale madhalimu.

ni wale ambao hawaji matawi ya chini katika kuhifadhi serikali zao na vyeo vyao, na huwa tayari kufanya dhulma yoyote waitakayo ili kufikia katika mahitajio yao. Kama anavyosema Allah (s.w):-

وَلاَ تَرْكَنُواْ إِلَي الَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللهِ مِنْ اَوْلِيَاء ثُمَّ لاَ تُنصَرُونَ[1]

Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.

*Imeelezewa kwa urefu katika Aya ya 85 ya Suratun Nisaa wema wa kusaidia kufanyika mema, na ubaya wa kusaidia kufanyika mabaya.

SIFA ANAZOTAKIWA KHALIFA KUWA NAZO.

Kutokana na maelezo yaliyopita tumefahamu kuwa watu pekee wanaostahiki kutiiwa na kuwa viongozi katika jamii ni lazima wawe na sifa njema, wawe wameepukana na kumuasi Mola wao, na wawe watu bora kielimu, kiadilifu, kishujaa, na wawe  thabiti katika kuzitekeleza hukumu za kiislamu, katika sehemu hii tutaelezea kwa ufupi sifa hizo moja badala ya nyengine.

1- elimu.

Sifa muhimu anayotakiwa kiongozi wa jamii kuwa nayo ni kuwa na elimu ya kutosha, elimu ambayo itamfanya yeye awe bora katika kuilingania dini ya Mwenyeezi Mungu katika jamii, kama alivyochaguliwa Talut kuwa ni kiongozi aliyeteuliwa na Mola wake. Allah (s.w) anasema:-

وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ اللّهَ قَدْ بَعَثَ لَكُمْ طَالُوتَ مَلِكاً قَالُوَاْ اَنَّي يَكُونُ لَهُ الْمُلْكُ عَلَيْنَا وَنَحْنُ اَحَقُّ بِالْمُلْكِ مِنْهُ وَلَمْ يُؤْتَ سَعَةً مِّنَ الْمَالِ قَالَ إِنَّ اللّهَ اصْطَفَاهُ عَلَيْكُمْ وَزَادَهُ بَسْطَةً فِى الْعِلْمِ وَالْجِسْمِ وَاللّهُ يُؤْتِى مُلْكَهُ مَن يَشَاءُ وَاللّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ[2]

Na Nabii wao akawaambia: Mwenyezi Mungu amekuteulieni Taluti (Sauli) kuwa ni mfalme. Wakasema: vipi atakuwa na ufalme juu yetu, na hali sisi tuna haki zaidi kupata ufalme kuliko yeye, naye hakupewa wasaa wa mali? Akasema: Mwenyezi Mungu amemteua yeye juu yenu na amemzidishia ukunjufu wa ilimu na kiwiliwili. Na Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mjuzi.

* Hapa Mwenyeezi Mungu anatia nguvu habari ya elimu na siha. Mwenye elimu na siha ndiye anayestahiki kupewa ukubwa wa kuendesha watu na mambo yao, na elimu haikamiliki katika kiwiliwili chenye siha mbovu, uislamu unahimiza sana katika – qur-ani na hadithi – juu ya kutafuta elimu na kurai (kuchunga) siha.

Baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) mtu aliyekuwa na elimu ya dini ya Mwenyeezi Mungu ni Imamu Aliy (a.s), kama inavyotuthibitishia elimu ya tarehe, na yale tunayoyasoma ndani ya Nahjul-balagha.

ایها الناس سلونی قبل ان تفقدونی[3]

Yaani Enyi watu niulizeni kila mnalolitaka kabla sijaondoka kwenu.

Imamu Ali (a.s) alikuwa na elimu ya hali ya juu kabisa, na wala sio katika mambo ya kidunia tu alikuwa ni m-bora kulinganisha na wengine, bali hata katika masuala ya akhera na uhakika wa siku hiyo alikuwa na elimu ya kutosha kiasi ya kwamba watu wengine hawakuwa na elimu wala uhakika wowote kuhusiana na siku hiyo tukufu. Kama anavyosema katika nahjulbalagha:-

فلانا بطرق السماء اعلم منی بطرق الارض[4]

Mimi nazielewa zaidi njia za mbinguni kuliko njia za ardhi.

[1] Surat –Huud Aya ya 113

[2] Suratul-Baqarah Aya ya 247

[3] Nahjulbalagha, Subhi salih, خ189, Nahjulbalagha faidhul-islaam 231.

[4] Nahjulbalagha, Subhi salih, خ 189, Nahjulbalagha faidhul-islaam 231.

MWISHO