QUR_ANI INATOSHA
  • Kichwa: QUR_ANI INATOSHA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 0:39:45 5-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

QUR_ANI INATOSHA

Kuna kauli inayosemwa na baadhi ya Waislamu kuwa Qur-ani inatosha  kuhukumu mambo ya Waislamu  yanayohusiana na dini. Hivi kweli kauli hiyo ni sahihi? wafuasi wakweli wa Mwenyeezi Mungu, ni wale wenye kuyafanyia amali maagizo ya Mola wao, watu hao hutii yale yaliyomo ndani ya Qur-ani, na vile vile hutii amri za Mwenyeezi Mungu na Mitume yake. Watu ambao husema :-

حسبنا کتاب الله.

"Kitabu cha Mwenyeezi Mungu kinatosha, kwa hakika wameipinga kauli ya Mwenyeezi Mungu, na hawakuzifanyia amali Aya za Mwenyeezi Mungu. kwa sababu ndani ya Qur-ani tunasoma hivi:-

وَاَطِيعُواْ اللّهَ وَاَطِيعُواْ الرَّسُولَ وَاحْذَرُواْ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُواْ اَنَّمَا عَلـٰي رَسُولِنَا الْبَلاَغُ الْمُبِينُ[1]

Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka basi jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe tu ulio wazi.

Na vilevile ndani ya Qur-ani kumeelezewa kuwa, hakuna ruhusa ya kukhalifu desturi desturi za Mtume Muhammad (s.a.w.w). jambo hilo ni muhimu sana kiasi ya kwamba nafsi ya Mtume ni bora zaidi kuliko nafsi yake mwenyewe mwanaadamu. Kama inavyosema Qur-ani:-

مَا كَانَ لِاَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ الاَعْرَابِ اَن يَتَخَلَّفُواْ عَن رَّسُولِ اللهِ وَلاَ يَرْغَبُواْ بِاَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِ ذٰلِكَ بِاَنَّهُمْ لاَ يُصِيبُهُمْ ظَمَاٌ وَلاَ نَصَبٌ وَلاَ مَخْمَصَةٌ فِى سَبِيلِ اللهِ وَلاَ يَطَؤُونَ مَوْطِئاً يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلاَ يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلاً إِلاَّ كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ إِنَّ اللّهَ لاَ يُضِيعُ اَجْرَ الْمُحْسِنِينَ[2]

Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio jirani zao kubakia nyuma wasitoke na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko yeye. Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa,kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapo waghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanao fanya mema.

*Katika Aya hii,  wanaambiwa Waislamu wa zama hizo , waliokuwa wakitaka  raha za nafsi zao na kumuacha Mtume katika taabu, Sio hivyo.  mchukulie tabu zake unayempenda, sio vyema yeye achukue tabu zenu. Bila ya shaka hayo si mapenzi Na wanatajiwa thawabu watazozipata watakapochukua taabu hizo,. Asali haiwezi kupatikana bila ya kupigwa na misumari ya nyuki. pata shida juani na ustarehe kivulini, au utakufa njaa.

Mtume (s.a.w.w) yeye ndiye mwenye majukumu ya kufikisha Wahyi wa Mwenyeezi Mungu kwa waja wake, na Yeye ndiye Mwenye kuhukumu kutokana na sheria za Kiislamu, kwa mfano:-

kutangaza vita au kutaka suluhu, n.k.... Na kila wadhifa alionao au hukumu anayotoa, anahukumu kutokana na Wahyi au maagizo yake Allah (s.w). kama tunavyosoma ndani ya qur-ani:-

إِنَّا اَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا اَرَاكَ اللّهُ وَلاَ تَكُن لِّلْخَآئِنِينَ خَصِيماً[3]

Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyo kuonyesha Mwenyezi Mungu. Wala usiwe mtetezi wa makhaaini.

Watu waliopuuza na kuacha kufuata desturi za Mtume na Ahlulbayt, kwa hakika wameipuuza na kuwacha Qur-ani takatifu. Kwa sababu kuamini Mwenyeezi Mungu, na kuwa thabiti katika hukumu zake , hapana shaka kunahitajika kuwa na imani na Mtume wake, kama inavyosema qur-ani;-

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللّهَ فَاتَّبِعُونِى يُحْبِبْكُمُ اللّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَاللّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ[4]

Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu.

Kwa hiyo, mtu anayedai kuwa anamuamini Mwenyeezi Mungu, hali ya kuwa hafuati mwendo wa  Mtume, wa kufanya mema na kuacha mabaya - mwongo.
Kutokana na maelezo hayo, imefahamika kuwa aya za qur-ani zimefafanua kwa uwazi kuwa, kumtii Mtume  (s.a.w.w), na vile vile kumtii kiongozi  baada ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu  ni jambo la lazima na muhimu katika dini ya Kiislamu. Na hakuna shaka yoyote kuwa kiongozi huyo ni katika Maimamu (a.s). yaani:- AHLULBAYT (A.S).

 

[1] Suratul-Maidah Aya ya 92

[2] Surat Tawba Aya ya 120

[3] Suratun Nisaa Aya ya 105

[4] Surat Al-Imraan aya ya 31

MWISHO