FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA
  • Kichwa: FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 3:51:34 2-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

FAIDA ZA KUIKUMBUKA SIKU YA KIAMA NO 1.

Kauli muhimu za Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni kuwalingania watu kuamini Mola mmoja na kuwakumbusha maisha baada ya mauti. Jitihada kubwa walizozifanya Mitume baada ya kuwalingania watu kuabudu Mola mmoja ni kuihuisha Siku ya Kiama katika nyoyo za watu. katika makala iliyopita tulielezea kuhusiana na umuhimu wa siku ya kiama katika makala hii tutaendelea na kuelezea faida za kuikumbuka siku hiyo takatifu.

 Faida za kuikumbuka siku ya Kiama.

Miongoni mwa faida za kuikumbuka siku ya Kiama ni kama ifuatavyo:-

1. Kuona upeo wa njia sahihi.

kujiwekea kumbukumbu za siku ya Kiama kunaweza kumsaidia mwanaadamu kuwa na upeo wa kuona njia iliyo sahihi. na hupigana na nafsi yake katika matamanio ya dunia na kuona nuru ya maisha yake ya milele. Na wakati huo mwanaadamu huyo hufanya jitihada zake zote na huwa na furaha na shauku ya kunufaika na maisha yake ya uhakika - yaani maisha yake baada ya kufa - .

Ndani ya quran Mwenyeezi Mungu anaashiria uhakika huo kwa kusema:-

وَمَا هَذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ لَهْوٌ وَلَعِبٌ وَإِنَّ الدَّارَ الآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ[1]

Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha khasa; laiti wangeli kuwa wanajua!

Tofauti baina ya mchezo ( pumbao) kwa dunia na kubatilika kwa dunia.

Kama inavyoeleweka kuwa watoto wana mahitajio yao katika maisha yao, na kugundulika yale matendo wanayoweza kuyafanya katika maisha yao wanahitajia mchezo na uhuru ili kuthibitisha yale matendo wanayoweza kuyafanya. Na watu wazima vile vile wana matendo yao ambayo yanawaletea athari nzuri katika maisha yao, kwa mfano kupenda mali, watoto au cheo na uongozi katika kuendeleza sayansi na technologia.

Ama ni lazima tufahamu kuwa yote hayo niya kupita tu, na hakuna hata kimoja kinachoweza kumfikisha mwanaadamu katika ukamilifu. Isipokuwa kwa yale ambayo yanaweza kumnufaisha mwanaadamu katika maisha yake ya Akhera, mbali ya hivyo mali, watoto au cheo hayatamletea faida mwanaadamu katika maisha yake. Na kwa sababu hiyo basi ndani ya Qurani Mwenyeezi

Mungu anawaambia wale ambao wamejitosheleza na maisha ya dunia na wamesahau Akhera. kwa kusema:-

يَعْلَمُونَ ظَاهِراً مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ[2]

Wanajua hali ya dhaahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.

2. Uhuru katika matendo na tabia.

Faida ya mwanzo ya kuitakasa nafsi humrudia mwanaadamu mwenyewe, na hii ni azma (nia) nzuri inayomfanya mwanaadamu awe huru katika matendo na tabia, lakini kuikumbuka siku ya Kiama kuwa makini na kuzingatia kuwa mwanaadamu atarejea kwa Mola wake, mara mbili zaidi humfanya mwanaadamu aweze kuidhibiti nafsi na maovu. Maelezo hayo yameelezewa ndani ya qur-ani:-

وَلاَ تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ اُخْرَي وَإِن تَدْعُ مُثْقَلَةٌ إِلَي حِمْلِهَا لاَ يُحْمَلْ مِنْهُ شَيْءٌ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَي إِنَّمَا تُنذِرُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالغَيْبِ وَاَقَامُوا الصَّلاَةَ وَمَن تَزَكَّي فَإِنَّمَا يَتَزَكَّي لِنَفْسِهِ وَإِلَي اللهِ الْمَصِيرُ[3]

Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Na aliye topewa na mzigo wake akiomba uchukuliwe hautachukuliwa hata kidogo, na angamwomba jamaa yake. Hakika wewe unawaonya wale wanao mcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu, na wanashika Sala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.

Vile vile kuwa na itikadi ya kuwepo siku ya Kiama kunaweza kumsaidia mwanaadamu kujiepusha na  matendo maovu.  Na mwanaadamu huyo hujilaumu yeye na nafsi yake pale anapotenda matendo mabaya. Na vile vile tunaweza kusema kuwa kuikumbuka siku ya Kiama kunaweza kumpelekea mwanaadamu huyo kuwa makini ili asije akapoteza fursa ya kuingia Peponi,na humtahadharisha kujiepusha na kufanya maovu ili asiwe miongoni mwa watu watakaoingia motoni.

Umuhimu wa kuikumbuka siku ya Kiama na kuizuilia nafsi na kutenda maovu, humsaidia mwanaadamu kufuata njia ya saada na kufikia katika ukamilifu. Mwenyeezi Mungu Mtukufu ameviweka vitu hivyo viwili pamoja kutokana na utukufu wake, Naye anasema:-

        .لاَ اُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ * وَلاَ اُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ[4]

Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!

Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!

[1] Surat Ankabuut Aya ya 64.

[2] Surat Ruum Aya ya 7.

[3] Surat Faatir Aya ya 18

[4] Surat Alqiyama Aya ya 1-2.

MWISHO