DINI INALETA AMANI NA SALAMA
  • Kichwa: DINI INALETA AMANI NA SALAMA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 23:41:7 4-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

DINI INALETA AMANI NA SALAMA
Uhakiki wa dini ni zana inayoleta maendeleo, amani, na usalama.

Miongoni mwa misingi mengine ya uhakiki wa dini ni kuwaletea wanaadamu amani na usalama na kuwaongoza katika njia iliyo sahihi, amah ii haimaanishi kuwa hadafu na malengo ya uhakiki wa dini ni kujenga mahusiano au kufanya suluhu na dini nyengine, bali hadafu asili ni kuondoa na kutokomeza fikra na mitizamo isiyo sahihi ya dini hizo, na kuwalingania wafuasi wa dini hizo katika dini moja tu ya haki, nayo ni dini ya Kiislamu, ujumbe wa Mwenyeezi Mungu uliomo katika dini hiyo unawabainishia wanaadamu wote ulimwenguni kuwa dini ya haki ni dini ya Kiislamu pekee, kwa hiyo hadafu ya ujumbe huo sio kitu chengine isipokuwa ni kuondoa na kutokomeza fikra za dini zisizokuwa sahihi. Kwa hiyo, ni lazima tuwe na imani ya kuwa uhakiki wa dini ni kwa ajili ya kuhukumu kuwa dini ya Kiislamu ni dini ya haki katika nidhamu na jamii zote duniani, na ikiwa kuna dini ambazo zimetungwa au kuletwa kutokana na tamaduni za watu basi tunaweza kutumia tamaduni hizo potofu kama ni nyenzo ya kuwatanabahisha wenye dini kama hizo kuwa wako katika njia potofu, na tamaduni za kiislamu ndio tamaduni pekee zinazoendana sambamba na saada ya mwanaadamu duniani na Akhera.

Hivyo waislamu wote inawapasa wasisahau kuwa; katika hatua ya mwanzo ni uhakiki wa dini ndio utakaorahisisha kuja kwa serikali na utawala wa muokozi wa mwisho, hadharati Mahdi Ajjala Llahu Taala Sharifu (r.a), na serikali ya Imamu Mahdi (a.s) haiendani sambamba na dini nyengine isipokuwa dini ya Kiislamu tu.

Na kwa sababu hakuna fungamano lolote baina ya dini ya Kiislamu na dini nyengine, basi vile vile hakuna fungamano lolote baina ya serikali ya Imamu Mahdi (a.s) na dini nyengine.

Ufumbuzi msingi wa kisaikolojia.
Msingi mwengine wa uhakiki wa dini ni kuwepo ulazima wa ufumbuzi wa kisaikolojia wakati unapofanywa uhakiki wa dini.
Miongoni mwa mambo muhimu ambayo ni lazima muhakiki kuyatambua, ni kuwa na elimu ya kuelewa taaluma na hukumu za dini kulingana na mwenendo na matendo ya watu wanaowahubiria wanajamii kuhusu dini hiyo, muhakiki inampasa kufanya uhakiki wake kwa kuitafutia utafiti mienendo ya jamii hiyo ya kuwa inaendana sambamba na ile elimu ya dini inayofanyiwa uhakiki? Kwa ubainisho mwengine tunaweza kusema hivi:

(muhakiki ni lazima aelewe ya kuwa hivi kweli mwenendo wa watu hao wenye dini unalingana na yale yanayolinganiwa katika dini yao)?. Kwa sababu hiyo basi muhakiki ni lazima ayafanyie utafiti na kuyapima yale yanayokubaliwa na jamii hiyo ya watu wenye dini, na alinganishe baina ya mienendo ya watu hao wenye kufuata dini fulani na mwenendo wa wale wasioifuata dini hiyo (wasiokuwa na dini), au wale wanaofuata dini nyengine, wakati huo basi dini hiyo inaweza kufanyiwa tahalili kupitia wataalamu wa elimu ya Saikolojia, na baadae kutafutiwa utafiti ili kutambulikana chanzo cha faida na madhara yanayojitokeza katika jamii, inawezekana chanzo cha faida na madhara hayo ikawa ni mwenendo na matendo ya jamii fulani, Basi hivi kweli hakuna tofauti yoyote baina ya mwenendo wa watu wenye kufuata dini ya haki, na mwenendo wa wale wasioifuata dini hiyo, au wale wenye kufuata dini nyengine?. Hapana shaka mwenendo na matendo ya watu wenye kufuata mtiririko wa dini ya haki ni yenye kukubalika zaidi kuliko mwenendo na matendo ya watu wasiofuata dini hiyo, kwa sababu hiyo basi ndio tukasema msingi huo wa kutafutiwa ufumbuzi wa Kisaikolojia ndio msingi muhimu katika uhakiki wa dini.


MWISHO