FUNGAMANO LA NASABU SIKU YA KIAMA
  • Kichwa: FUNGAMANO LA NASABU SIKU YA KIAMA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 3:37:39 2-9-1403

 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

FUNGAMANO LA NASABU SIKU YA KIAMA

* Mahusiano na mafungamano ya kidunia ya wanaadamu yatakuwa vipi siku ya Kiama?.

UHUSIANONA FUANGAMANO LA SABABU NA NASABU KATIKA SIKU YA KIAMA.

 Itakapofika siku ya Kiama hakutakuwa na uhusiano wala fungamano lolote baina ya wanaadamu, hata fungamano la nasaba pia litakuwa halina nafasi yoyote katika familia, mwanaadamu hatakuwa na hiyari yoyote katika familia wala nasaba, mlolongo wa muamala na ahadi ambazo watu waliahidiana hazitakuwa na nafasi yoyote katika jamii, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani takatifu:-

فَإِذَا نُفِخَ فِى الصُّورِ فَلاَ اَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلاَ يَتَسَاءلُونَ[1]

Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo,

wala hawataulizana.

Maelezo kuhusiana na aya.

Haya ndiyo yale yanayokaririwa katika Qur-ani na Hadithi sahihi za Mtume (s.a.w.w) kuwa nasabu haifai kitu huko Akhera. hakuna ya kweli zaidi kuliko ya Mwenyeezi Mungu, Nayo ni haya. Basi watu nawaseme uwongo wao, khiyari zao, yatawafika wenyewe. “Mtumaini cha ndugu hufa ali masikini”.

Jannatu Naimu Fil-Jinani                 Jini wa Insi waitamani

Jumla ya watu hawaioni                  Ila kwa amali kutaqadama.

Thamani ya pepo ukiitaka              Dhiki moyo wako kutozunguka

Thubutisha taa yake Rabuka          Ili akujazi majaza mema.

Katika siku ya Kiama fungamano, upendo wa uwongo na urafiki wowote ule mbaya hautakuwa na uhusiano wa fungamano lolote kama anavyosema Allah (s.w):-

الاَخِلاَّء يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلاَّ الْمُتَّقِينَ[2]

Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipo kuwa wacha Mungu.

Maelezo kuhusiana na Aya.

Hakuharibika mwanamume yoyote yule ila kwa kuchochewa na rafiki yake mbaya, wala hakuharibika mwanamke yoyote yule ila kwa shoga (rafiki) yake mbaya, basi natutahadhari na marafiki na mashoga (marafiki) wabaya,, mapenzi ya hapa tu duniani, kisha yatakuwa machukiano makubwa kabisa baina yao siku ya Kiama, kama anavyosema Mwenyeezi Mungu katika Aya ya 25 ya Surat Ankabuut, bali wataanza kuchukiana tangu hapa kwa mabaya yatakayowafika hapa kabla ya Akhera.

Fulani nalikwambiya      Wacha suhuba

Ya watu walo wabaya      Huo ukuba

Umekwisha kuingiya       Kwenye misiba.

Siku ya Kiama hakutakuwa na mtu yoyote atakayekuwa na hiyari ya kufanya jambo alitakalo, na hakutakuwa mtu yoyote atakayekuwa na uwezo au nguvu za kumsaidia mtu, isipokuwa yule ambaye atapewa idhini na Mwenyeezi Mungu (s.w), kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani takatifu:-

يَوْمَ لاَ تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئاً وَالاَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِلَّه[3]

Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.

Maelezo kuhusiana na Aya.

Yaani siku ambayo hapana mtu atakayeweza kumfaa mwenziwe kwa lolote, hata hakuna atakayekuwa na uweza wa lolote au kutoa amri yoyote isipokuwa Mwenyeezi Mungu peke yake.                      

Siku ya Kiama kila mwanaadamu atakuwa ni mgeni wa milele wa matendo yake aliyoyafanya, na kila mtu atalipwa malipo yake kulingana na hisabu ya amali zake, kama anavyosema Allah (s.w):-

وَكُلُّهُمْ آتِيهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَرْداً[4]

Na kila mmoja katika wao atamfikia Siku ya Kiyama peke yake Hayo yalikuwa ni masadikisho ya Aya za Qur-ani yanayothibitisha uhusiano na fungamano la duniani na Akhera, fungamano ambalo linakuja kulingana na amali za wanaadamu wanazozifanya hapa duniani, natija ya amali hizo baadhi watakwenda kuzikuta Akhera, na baadhi watazishuhudia hapa hapa duniani.

Katika sehemu hii natuzingatie uhusiano huo au fungamano hilo linatokana na nini?

 

[1] Suratul-Muuminuun Aya ya 101

[2] Surat Zukhruf aya ya 67

[3] Surat Infitar Aya ya 19

[4] Surat Maryam Aya ya 95.


 

MWISHO