HATUA NA MALENGO YA PLURALISM
  • Kichwa: HATUA NA MALENGO YA PLURALISM
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 4:10:11 2-9-1403

 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU.

HATUA NA MALENGO YA PLURALISM

Hatua ya kwanza:

Kubadilisha haki na uhakika wa dini kupitia nidhamu maalumu iliyopangwa, taaluma na maadili ya dini wameyabadilisha, taaluma ambayo ndio njia msingi itakayoweza  kumfikisha mwanaadamu katika ukamilifu, na wameondoa na kutokomeza taaluma na maadili hayo ya dini wakavumbua maadili yao ambayo hayana thamani yoyote katika maisha ya mwanaadamu na hayamfikishi mwanaadamu katika mahitajio yake wala katika ukamilifu.

Malengo ya hatua hiyo yanatekelezwa kupitia njia hizi zifuatazo:-

1.kuuarifisha ukamilifu na saada ya mwanaadamu chini ya misingi ya maendeleo ya kidunia, ili kuwapotosha watu katika uhakika halisi wa ukamilifu.

2. Kuifunga dini katika utakaso wa kimoyo tu, na taaluma isiyo ya kawaida, (hali ya kwamba dini mbali ya kuwa na nafasi katika kuutakasa moyo na maovu, vile vile ina nafasi katika nyanja nyingi tofauti katika maisha ya mwanaadamu ya duniani na Akhera. Kwa upande mwengine, watu hao walibuni taaluma, chini ya mfumo wa maendeleo ya duniani tu, na sio taaluma ya Mwenyeezi Mungu iliyojengwa katika mfumo maalumu, mfumo ambao unaendana sambamba na mahitajio ya mwanaadamu ya duniani na Akhera, na kwa mfumo wa elimu hiyo mwanaadamu hufikia katika saada ya duniani na Akhera. Mfumo huo ni tofauti na ule mfumo wa watu hao hauna sifa kama hizo za mfumo wake Mola Mtakatifu.

3. Kuondoa akida ya kuamini siku ya Kiama, kasumba hizo zilifanyiwa propaganda takriban mnamo karne ya kumi na nne miladi na kuendelea, kwa lengo la kuwashawishi watu kuamini na kukubali upotofu wao huo waliokuwa wakiwatangazia watu.

4. Kuondoa na kufuta akida ya kuamini Mitume ya Mwenyeezi Mungu na Maimamu (a.s), (Ahlulbayt a.s), ili kufikia katika lengo lao hilo walitumia njia za kuwaweka watu katika shaka na wasiwasi, kwa madai ya kuwa Mitume ya Mwenyeezi Mungu haina nguvu wala uwezo wowote ule wa kielimu, kwa upande mwengine wakadai kuwa Mitume hiyo ilitumia tajriba zao binafsi katika kuwalingania watu madai yao , na sio nguvu wala elimu yake Allah (s.w).

Hatua ya pili:

Katika hatua hiyo, badala ya kutambulikana kuwa saada ya wanaadamu inaweza kupatikana kwa kuitumia dini na Mitume ya Mwenyeezi Mungu kama na vigezo vitakavyowafikisha katika njia njema, basi kidogo kidogo walitoa kasumba zao na kudai kuwa udhahiri wa dini tu unatosheleza katika kumletea mwanaadamu saada, na kupitia udhahiri huo wa dini mwanaadamu anaweza akaokoka kutokana na ile imani yake aliyoipata kupitia taaluma ya dunia, au taaluma isiyo ya kawaida, yaani taaluma iliyobuniwa na watu hao, na sio taaluma na elimu aliyoiteremsha Allah (s.w) kwa ajili ya kuwaongoza waja wake katika njia njema yenye saada.

Kuhusiana na hatua hiyo ya pili, bwana Field Shawn ana kauli yake inayosema hivi:

“Basi kwa nini watu wote wasiende peponi, kwani tafakuri hizo hizo za kidunia zinatosha katika kupatikana saada ya kila mwanaadamu”.

MWISHO