PLURALISM NA DINI TOFAUTI
  • Kichwa: PLURALISM NA DINI TOFAUTI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 8:48:5 4-9-1403


 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

PLURALISM NA DINI TOFAUTI

5. Pluralism (dini nyingi tofauti).

Kwa mtazamo wa watu hao, dini zote na makundi yote yaliyomo katika jamii ni lazima yaheshimiwe na yathaminiwe, hata ikiwa dini hizo au makundi hayo yako katika njia potofu, au dini zilizoharifiwa na kupotoshwa, dini hizo zinaweza zikawa dini za Kikiristo, kiyahudi, dini za Buda, dini za Hindu, n.k. kwa upande mwengine hata zile dini ambazo kidhahiri zina rangi ya Uislamu kwa mfano kundi la mawahabi, zote hizo zinahitajiwa kupewa msukumo katika itikadi zao.

6. Miongoni mwa mipango mengine inayotumiwa na Pluralism kwa ajili ya kufikia katika malengo yao ni:-

Kuharibu nguvu na uwezo wa Wanafiqhi na Wanazuoni wa kidini ndani ya uongozi na usimamizi wa Serikali, kwa ajili ya kudhibiti misingi ya dini isienee katika jamii na Serikali, na natija ya hayo ni kuondoa na kutokomeza Yale ambayo wenye dini wanayatekeleza katika mwenendo na matendo yao, na waliyo na itikadi nayo.

7. kuondoa na kutokomeza kanuni na sheria za wana dini wenye kuitunza na kuithamini dini yao ndani ya jamii, na baadae kuitokomeza misingi ya dini ya watu hao, Pluralism huwatawala kifikra wale walioghafilika na dini yao katika jamii, na kuweka kanuni na sheria zao zinazoendana sambamba na malengo yao, kwa uwezo wake Allah (s.w) inawezekana katika kipindi kijacho watu waliolala kifikra na walioghafilika kuamka na kutambua mipango na programu za watu hao, basi kwa juhudi za watu hao na kwa mashirikiano ya waislamu wote inawezekana pakatokomezwa fikra hizo potofu za Pluralism.

8.Miongoni mwa mipango mengine inayotumiwa na watu wenye mtazamo wa pluralism, ni kuwapotosha watu wenye dini, kwa kudai kuwa Mitume haikopokea Wahyi wa aina yoyote kutoka kwa Mola Mtakatifu, na wao huufasiri Wahyi kama ni tajiriba ya Mitume wenyewe binafsi na hakuna fungamano lolote baina ya Wahyi na Mwenyeezi Mungu (s.w), natija ya madai hayo ni kupatikana hoja zitakazoweza kuthibitisha kuwa dini ya Kiislamu ni dini ya haki, na Mitume inayodaiwa kuwa imeteremshwa na Mola Mtakatifu haina uhusiano wala fungamano lolote na Mwenyeezi Mungu, basi hizo ndio hoja na dalili wanazotumia Pluralism ili kuutokomeza Uislamu na utume wa Mitume ya Mwenyeezi Mungu. Hoja hizo hutolewa kwa Waislamu na hata kwa wale wasiokuwa Waislamu .

9. Miongoni mwa mipango mengine iliyopangwa na watu hao kwa ajili ya kuitekeleza ni kuwa; Pluralism wanafanya jitihada zao zote ili kuthibitisha kuwa waislamu hawako katika njia iliyo sahihi, kwa sababu hawakutambua na wamekosea katika itikadi na imani zao juu ya Mitume na ahlulbayt (a.s), na dalili wanayoitoa katika kuthibitisha madai yao hayo ni kuwa Mitume haikupokea Wahyi wa aina yoyote kutoka kwa Mwenyeezi Mungu, bali jambo walilolifanya ni kutumia tajiriba zao za kibinafsi, hivyo hakukuwa na Wahyi wowote ule walioupokea kutoka kwa Mola Mtakatifu, natija ya madai hayo pia ni kuondoa na kutokomeza utukufu wa Mitume na Ahlulbayt (a.s), kwa kuwafanya watu wawe na shaka au wasi wasi katika nyoyo zao kutokana na itikadi zao juu ya kuwa na imani na Mitume, Maimamu, na Ahlulbayt (a.s).


MWISHO