MTAZAMO WA PLURALISM KUHUSIANA NA DINI
  • Kichwa: MTAZAMO WA PLURALISM KUHUSIANA NA DINI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:29:28 1-9-1403


 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MTAZAMO WA PLURALISM KUHUSIANA NA DINI

Watu walio na fikra za Pluralism (itikadi ya dini tofauti), wana imani ya kuwa;  Elimu ya tarehe inathibitisha kuwa njia na sheria zozote zile zitakazomuongoza mwanaadamu katika kumfikia mola wake zinakubalika na ni lazima ziheshimiwe, kwa hiyo wafuasi wote wa dini tofauti, ikiwa ni dini ya Mayahudi, Manasara, washirikina, mabuda, mapagani, n.k. ni lazima itikadi zao ziheshimiwe, nay ale waliyo na imani nayo yanawadhamini watu hao kuwa yatawafikisha katika saada.

Hayo yalikuwa ni maelezo kwa ufupi tu kuhusiana na dini tofauti chini ya mtazamo na fikra za pluralism, katika paragrafu hii tutaelezea chanzo cha fikra hizo ni nini, na wenye kuwa na fikra hizo wana malengo gani, hivi kweli malengo yao ni kumfikisha mwanaadamu katika saada? Kwa fikra hizo wanatafuta kitu gani? Au wanataka kuthibitisha nini?. Hebu natuendelee na mlolongo wa mada hiyo kwa kuzingatia masuala haya yafuatayo:-

- Chanzo na asili ya fikra za pluralism ni nini?

- Pluralism wanatafuta malengo gani kutokana na fikra zao hizo?

Hivi fikra na mitazamo ya Pluralism ni kuwaondoshea shaka na kuwapa utulivu

watu wenye kiu na maarifa ya dini ambao hawana imani na dini takatifu? Pluralism wanataka kuonyesha kuwa tafakuri za watu hao tafakuri za watu hao wenye kiu na maarifa ya dini ni dalili tosha inayoweza kudhamini saada ya siku ya Kiama ya watu hao, basi kwa nini watu hao wasipewe zawadi hiyo? Hapana, hayo sio malengo ya pluralism, na Pluralism hawana nguvu wala uwezo wowote utakaoweza kudhamini saada ya watu hao, bali Pluralism ana malengo mengine yasiyo hayo, yeye kulingana na tafakuri za watu hao ana mipango na program zilizo hatari alizozipanga kwa ajili ya saada ya watu hao na wanaadamu kwa ujumla. Hivyo ni lazima wanaadamu wote duniani wawe makini katika kutambua mipango hiyo ya Pluralism ili wasije wakaingia katika shimo hilo hatari lililochimbwa na watu hao wenye akida ya pluralism.

Ili kutambua zaidi fikra za Pluralism zimetokea wapi, ni lazima kuashiria utangulizi mdogo tu kuhusiana na maudhui hayo.

Moja: Malengo msingi ya kuanzishwa mipango ya kuwa na itikadi na dini tofauti yanatokana na jitihada za Phylosophy mabepari waliokuwa na nguvu na uwezo katika jamii au dunia ile ya nchi za kimagharibi, mafilosofi hao walikuwa wakifanya jitihada zao zote ili kunufaika au kupata manufaa yao binafsi kwa kujenga uhusiano madhubuti na mitandao au vyombo mbali mbali vya habari ili kuitangazia jamii yale waliyodai kuwa yanawaletea wanaadamu saada na mafanikio, hivyo waliweka nidhamu zao walizozihitajia katika ulimwengu ili kufikia katika malengo yao. Watu hao walishafahamu kuwa, hawawezi kukubalika katika jamii ile kupitia tamaduni ambazo zilikuwa zikiaminiwa, na wala hawawezi kukubalika kutokana na dini mahasusi waliyokuwa wakiamini philosophy hao, na tamaduni au dini hizo hazitoweza kuleta ule umoja wa kisiasa waliokuwa wakiuhitajia, hivyo bila ya kuweka program hizo hawakuweza kueneza yale waliyokuwa na itikadi nayo au waliyokuwa wakiyaamini, kwa sababu hiyo basi, walipanga kila mipango, na walitumia kila njia iliyowezekana – hata kutoa taaluma za elimu isiyo ya kawaida, elimu ambazo zilikuwa zikiwapotosha watu- ili kutokomeza ule uimara na umadhubuti waliokuwa nao watu wa kuwa na imani na dini maalumu, wakati huo basi waliana kutunga mashairi mbali mbali yaliyokuwa yakiashiria kutokuwepo umuhimu wa dini fulani, na kudai kuwa dini zote zitamfikisha mwanaadamu katika saada, hivyo hakuna ulazima wa kuleta vurugu wala ghasia katika dini, jambo la lazima linalokubalika kiakili ni kuwa na uvumilivu na ustahamilivu, na kwa sababu ya propaganda zao hizo basi waliweza kuzitawala jamii zile kifikra, utawala ambao ulisababisha jamii zile kuacha imani na itikadi za dini walizokuwa wakiziamini. Kwa mtindo huo waliweza kuwatia watu hamasa ya kuacha na kutokomeza dini yao, na kuwafanya wanaadamu badala ya kutekeleza maamrisho ya dini yao, watu hao wakaiangalia dini katika mtazamo wake wa kidhahiri tu bila ya kuwa na mazingatio yoyote kuhusiana na dini hiyo.

Basi Phylosophy hao mabepari waliwaweka wanaadamu mbali na dini na tamaduni zao, na wakaweza kufikia katika malengo yao ya kisiasa, kiutamaduni, na kiuchumi, hatimae wanaadamu wakabakia katika sehemu ile ile na upotofu ule ule walioandaliwa na mabepari hao wa kishenzi.

Mbili: Ikiwa katika kipindi cha falsafa ya Plato mpaka kabla ya karne ya tatu ilidaiwa kuwa mwanaadamu ni kiumbe atakayedumu na kubakia milele, (hana mwisho), na Mwenyeezi Mungu ni kiumbe kisichodumu na ana mwisho wake, na ikiwa misingi ya fikra ya kifalsafa katika kipindi kile iliifanya elimu na taaluma ya Mwenyeezi Mungu kama ni jambo lisiloweza kuthibitishwa katika ulimwengu uliopo- na hakuna ulimwengu wowote utokanao na elimu ya Mwenyeezi Mungu- (yaani dunia imekuja wenyewe kwa wenyewe na Mola Mtakatifu siye aliyeuumba ulimwengu huu).

Basi hapana shaka ya kuwa fikra hizo potofu za kifalsafa ndizo kizuizi kikuu kilichowasababishia wanaadamu wasinufaike na baraka na rehema zake Mtume (s.a.w.w) na Ahlulbayt (a.s), - mahasusi katika jamii ile ya nchi za kimagharibi na Mapadri ambao walitengeneza muungu wao wenyewe, katika kipindi hicho mwanaadamu mpotofu na asiye mtiifu kupitia kitengo cha Mapadri hao na kwa lugha ya dini ya Mapadri hao, katika kipindi kile cha (Rolisense) mwanaadamu mpotofu alikuja na madai ya kuwa yeye ana uwezo wa kuhujumu na kufosi kudra za Mola Mtakatifu, basi alieneza tafakuri za kuwa ulimwengu hauna mipaka yoyote, (yaani ulimwengu utabakia milele). Hivyo kwa madai yao hayo walipinga kuwepo mipaka katika ulimwengu.

Watu hao, katika hatua ya kwanza walidai kuwa Mwenyeezi Mungu ana mipaka, na walimuweka kando Mola huyo katika fikra za wanaadamu, badala yake wakavumbua mfumo mwengine wa fikra usemao “mimi ni mwanaadamu niliye na shaka basi nipo”. Hiyo ni kauli ya Decart, yeye alivumbua na kutengeneza mola wake, kwa mujibu wa kauli ya Poscol, mola ambaye alikuwa na tofauti msingi na Mola wa Ibrahimu (a.s) na Ismail (a.s).

Ikiwa kutokana na fikra hizo mwanaadamu alibadilika na kuwa kiumbe asiye na thamani yoyote kiasi ya kwamba aliziweka fikra zake hizo za kifalsafa ni bora na zina misingi madhubuti zaidi kuliko dini zake Allah (s.w), basi alizitumia fikra hizo kama ni silaha ya kukabiliana na dini za Mola Mtakatifu, hatimae akachukua umbile na itikadi za Ormanism, Ormanism nao wakazidi kumdidimiza mwanaadamu huyo na kumpeleka katika daraja ya chini zaidi, daraja ambayo ilimfanya mwanaadamu huyo awe dhalili na asiye na thamani yoyote, wala asiye katika amani wala usalama.

kipindi hicho cha Modrinism vile vile kilikuwa ni kipindi kibaya kwa Decart, kwa sababu yule mola wake aliyekuwa katika mipaka fulani pia alimtoa na kumtokomeza katika akida zake, natija ya hayo badala ya kunufaika na kuwepo kwa Mola, na kuibainisha dunia kulingana na utukufu wa vile vilivyomo katika dunia hiyo alianza kuufasiri ulimwengu kwa mtindo wa makanika usiokubalika kiakili ili kuipandisha juu na kuikuza na kuiweka daraja ya Secularism karibu yake, basi vipi inawezekana kuiarifisha dini chini ya mtazamo wa Phylosophy waliokuwa wanaipinga dini? Vipi inawezekana kuiarifisha dini kwa kumuweka Mola kando na mbali ya watu? Watu hao hata hawakuweza kunufaika na neema zake zinazoshuhudiwa ndani ya dini yake Allah (s.w) .

Watu hao walio na itikadi na Pluralism wana mipango muhimu iliyodhibitiwa kimaandiko, na wanaelekea katika malengo yao kwa mujibu wa mipango hiyo, na ili kuyafikia malengo hayo wameweka hatua, hatua ambazo tutazielezea katika makala inayofuata

 

MWISHO