BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
HATIMA YA WALIOWAKHALIFU MITUME
* Kwa nini baadhi ya watu walisimama kidete kuwakhalifu Mitume?
* Waliowakhalifu Mitume walitumia njia gani katika kupingana na Mitume?.
Katika makala iliyopita tulielezea sababu zilizowafanya baadhi ya watu kuwakhalifu Mitume, na tukaelezea njia walizotumia maadui hao katika kukabiliana na Mitume, na tukaashiria kwa ufupi tu hatima ya watu hao, katika makala hii tutaendelea kwa kuelezea kwa kina hatima ya wapotofu hao.
3. Kulaaniwa na Mwenyeezi Mungu na kupata adhabu kali siku ya Kiama.
Watu ambao waliwapa mateso na kuwaudhi Mitume hawatapata rehema zozote kutoka kwa Mola wao, na watapata adhabu kali siku ya Kiama, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-
إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللهُ فِى الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ وَاَعَدَّ لَهُمْ عَذَاباً مُّهِيناً[1]
Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehi.
4. Kulipwa duniani kutokana na matendo mabaya waliyoyatenda.
Miongoni mwa malipo watakayolipwa wale waliowakhalifu na kuwapa mateso Mitume, ni kudhalilishwa kwa watu hao na kuharamishiwa rehema za Mwenyeezi Mungu, baadhi ya wakati watu kama hao hulipwa hapa hapa duniani, na kuona natija ya yale waliyoyatenda. Kama anavyosema Allah (s.w):-
إِنَّمَا جَزَاء الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللّهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِى الاَرْضِ فَسَاداً اَن يُقَتَّلُواْ اَوْ يُصَلَّبُواْ اَوْ تُقَطَّعَ اَيْدِيهِمْ وَاَرْجُلُهُم مِّنْ خِلافٍ اَوْ يُنفَوْاْ مِنَ الاَرْضِ ذٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِى الدُّنْيَا وَلَهُمْ فِى الآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ[2]
Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
Maelezo kwa ufupi ya makala zilizopita.
*Sababu muhimu zilizowafanya baadhi ya watu kuikhalifu Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni hizi zifuatazo:- Kufuata mwenendo na sifa za shetani, kughilibika na anasa za dunia, kuwa na kibri, na kutokubali haki.
* waliowakhalifu Mitume walitumia njia mbali mbali katika kupingana na Mitume hiyo, miongoni mwa njia hizo ni hizi zifuatazo:- Kuwauwa Mitume, kuwatuhumu kwa sifa mbaya, kuwapa mateso, n.k.
* wanafiki walitumia njia mbali katika kupingana na Mitume, miongoni mwa njia hizo ni: Kuwavunja nyoyo watu, kupinga desturi za dini,n.k.
* Hakuna malipo yoyote kwa wale waliowapinga Mitume isipokuwa kudhalilika, kupotea kwa amali zao bila ya kupata malipo yoyote, na kulaaniwa na kuewa adhabu kali duniani na Akhera.
Masuala.
1.Elezea kwa ufupi sababu zilizowafanya baadhi ya watu kuwakhalifu Mitume.
2. Kikawaida ni njia gani ya mwanzo waliotumia wale waliowakhalifu Mitume katika kupingana nao?.
3.Waliowakhalifu Mitume waliwatuhumu Mitume ya Mwenyeezi Mungu kwa tuhuma gani?
4.Kuna tofauti gani baina ya njia walizotumia wale waliowakhalifu Mitume na wanafiki katika kupingana na Mitume?.
5. Wana malipo gani wale waliowakhalifu Mitume?.
[1] Surat Al-Ahzaab Aya ya 57
[2] Surat Almaidah Aya ya 33
MWISHO