SIKU YA KIAMA
  • Kichwa: SIKU YA KIAMA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 16:53:51 3-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

SIKU YA KIAMA.

Kauli muhimu za Mitume ya Mwenyeezi Mungu ni kuwalingania watu kuamini Mola mmoja na kuwakumbusha maisha baada ya mauti. Jitihada kubwa walizozifanya Mitume baada ya kuwalingania watu kuabudu Mola mmoja ni kuihuisha Siku ya Kiama katika nyoyo za watu. Na Allah (s.w) ameielezea siku hiyo ya Kiama kuwa ndio madhumuni muhimu ya kuwapa Mitume wake Utume. Pale aliposema:-

رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِى الرُّوحَ مِنْ اَمْرِهِ عَلـٰي مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلاَقِ[1]

Yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye A'rshi. Hupeleka Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya kwa Siku ya Mkutano. Kufahamu sifa na nidhamu ya siku ya Kiama, kuelewa neema na daraja za peponi, na kufahamu daraja za adhabu ya siku ya Kiama, kunaweza kumsaidia mwanaadamu kuchagua njia sahihi na kuwa na madhumuni katika maisha yake,  wakati huo  mwanaadamu hujisikia kuwa maisha yake yote yana faida. Katika sehemu hii tutaelezea athari za kuikumbuka siku ya Kiama, kuwekwa  wanaadamu katika makundi tofauti, hali watakayokuwanayo siku ya Kiama kutokana na matendo na amali zao walizozifanya duniani,na madhara yanayopatikana katika kuipinga siku ya Kiama. Na tutathibitisha hayo kwa kuwatolea dalili za quran.

KUMBUKUMBU ZA SIKU YA KIAMA

* Kumbukumbu za dunia baada ya mauti zinaleta athari gani katika maisha ya mwanaadamu?. Kukumbuka Siku ya Kiama. Kuikumbuka siku ya Kiama kunamfanya mwanaadamu aweze kustahamili tabu na mashaka, kumfanyia wepesi na kuwa tayari kukabiliana na matatizo yote ili kufikia katika faida za maisha ya milele. kukabiliana mwanaadamu na matatizo kunaweza kumsaidia yeye kufikia katika ukamilifu, kiasi ya kwamba Mwenyeezi Mungu amewapa vyeo Mitume yake na kuwanufaisha au kuwahusisha wao na sifa tukufu kutokana na kuikumbuka siku ya Kiama, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:-

إِنَّا اَخْلَصْنَاهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَي الدَّارِ[2]

Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera Na kwa sababu hiyo basi katika makala ifuatayo tutaelezea athari na faida za kuikumbuka siku ya Kiama.

[1] Surat Ghaafir Aya ya 15

 

[2] Surat Saad Aya ya 47.

MWISHO