MALIPO NA ADHABU ZA SIKU YA KIAMA
  • Kichwa: MALIPO NA ADHABU ZA SIKU YA KIAMA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 17:7:43 3-9-1403

 

 BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UBORA WA NIDHAMU YA AKHERA KULIKO DUNIA NO.4

MALIPO NA ADHABU ZA SIKU YA KIAMA

* Ni nidhamu gani iliyo bora? nidhamu ya duniani au nidhamu ya Akhera?

* Ni dalili gani zilizo bora zinazoonesha maendeleo ya ubora huo wa nidhamu?.

Dunia ni madrasa na shule ya mpito, dunia ni sehemu inayomkuza mwanaadamu na kumzidishia kiwango chake cha fikra, dunia ni sehemu inayompeleka mwanaadamu katika ukamilifu na kumfanya awe mcha Mungu, dunia ni sehemu ya biashara ya kuitakasa nafsi na maovu kwa wale Mawalii wa Mwenyeezi Mungu.

HATIMA YA STAREHE ZA MILELE NA ADHABU ZA SIKU YA KIYAMA.

Miongoni mwa utukufu mwengine unaoonyesha ubora wa nidhamu ya siku ya Kiyama kuliko nidhamu ya duniani ni kuwepo malipo mema ya Pepo kwa wale ambao walifanya mema, malipo ambayo ni starere itakayodumu milele. Ama kwa wale waliofanya maasi na uovu watapata malipo yao ya moto, tuliposema kuwa watu wema watapata starehe ya milele tunakusudia kuwa; watu hao waliishi duniani na wakafanya jitihada zao zote, wakastahamili tabu na mashaka ili kupata mema ya duniani na Akhera, kwa hiyo, malipo hayo mema watakayopewa siku ya Kiyama na malipo halisi, yaani huko tena hawatapata tabu wala mashaka yoyote, kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani:

مُتَّكِئِينَ فِيهَا عَلـٰي الاَرَائِكِ لاَ يَرَوْنَ فِيهَا شَمْساً وَلاَ زَمْهَرِيرا[1]

Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.

Watu hao watapata kila neema wanayoitaka bila ya kupata tabu zozote,

يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ[2]

Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.

Ama wale waliofanya maovu watawekwa motoni, watakuwa na hofu iliyopita kiasi, adhabu zitawazunguka katika kila pembe, kiasi ya kwamba wakipata uakisi wa moto hupiga kelele kwa maumivu makali.

إِنَّهَا تَرْمِى بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ[3]

Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!

MAISHA NA HISIA ZA MILELE ZA SIKU YA KIYAMA.

Miongoni mwa utukufu mwengine unaoonyesha ubora wa nidhamu ya siku ya Kiyama kuliko nidhamu ya dunia, ni kuwa viumbe waliofanya mema watalipwa Pepo, na kuishi maisha ya mafanikio na starehe za milele, katika nidhamu ya Akhera hakuna kufa wala hakuna kuumwa, kama anavyosema Allah (s.w).

وَمَا هَذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ لَهْوٌ وَلَعِبٌ وَإِنَّ الدَّارَ الآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ[4]

Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha khasa; laiti wangeli kuwa wanajua!

na kuhusiana na maisha ya milele ya watu wema, na neema watakazonufaika nazo tunasoma hivi:-

لاَ يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلاَّ الْمَوْتَةَ الاُولَي وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ[5]

Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu.

Na kuhusiana na adhabu ya wale waliohalifu, adhabu ambayo haitakatishwa hata kwa sababu ya mauti yao anasema:-

إِنَّهُ مَن يَاْتِ رَبَّهُ مُجْرِماً فَإِنَّ لَهُ جَهَنَّمَ لاَ يَمُوتُ فِيهَا وَلاَ يَحْيى[6]

Hakika ataye mjia Mola wake Mlezi naye ni mkhalifu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi.

Siku ya Kiama viungo vya wanaadamu pia vitazungumza na kutoa ushahidi wa matendo yaliyofanywa na wanaadamu.

يَوْمَ تَشْهَدُ عَلَيْهِمْ اَلْسِنَتُهُمْ وَاَيْدِيهِمْ وَاَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ[7]

Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao kwa waliyo kuwa wakiyatenda.

Siku ya Kiama Mwenyeezi Mungu atazungumza pia moto, na moto nao utazungumza kumjibu Mola wake.

يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلاَتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ[8]

Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada?

 Maelezo kwa ufupi kuhusiana na makala zilizopita.

* Siku ya Kiyama hisia za mwanaadamu hazitakuwa katika mipaka maalumu, bali mwanaadamu atakuwa na uwezo wa kufahamu na kudiriki kila jambo, kwa hiyo hisia za mwanaadamu za duniani zinatafautiana na zile hisia atakazodhihiri nazo katika uwanja wa nidhamu ya Akhera, hisia za mwanaadamu katika uwanja wa Akhera ni halisi na zina upeo zaidi.

* Siku ya Kiyama pazia lililozuia uoni wa wanaadamu litaondolewa, na uhakika wa amali na matendo yote ya wanaadamu utadhihirika.

* Malipo mema watalipwa wale waja waliotenda mema, malipo hayo ni starehe itakayobakia milele, waja hao watalipwa Pepo na hawatapata mashaka wala tabu zozote kutokana na malipo yao hayo.

* Maisha ya siku ya Kiyama, ni maisha ya milele, katika maisha hayo hakuna mauti wala maradhi ya aina yoyote ile.

Masuali.

1. Nidhamu ya dunia ina nafasi gani na ile nidhamu ya Akhera.

2. Uhakika na haki ya mambo utadhihirika vipi katika nidhamu ya Akhera?.

3. Aya hii يَوْمَ تُبْلَي السَّرَائِرُ ina maana gani?

4. Matendo na amali za wanaadamu zitadhihirishwa vipi siku ya Kiyama?.

5. Malipo ya starehe na adhabu katika siku ya Kiyama yatakuwa katika namna gani?.

6. Ni Aya gani inayothibitisha kuwa katika nidhamu ya Akhera hakutakuwa na mauti?

 

[1] Surat Dahr Aya ya 13

[2] Surat Ad-Dukhaan Aya ya 55

[3] Surat Mursalaati Aya ya 32.

[4] Surat Ankabuut Aya ya 64

[5] Surat Ad-Dukhaan Aya ya 56.

6] Surat taha Aya ya 74.

[7] Surat Nuur Aya ya 24.

[8] Surat Qaf Aya ya 30

MWISHO